George W Bush avunjika shingo

George W Bush avunjika shingo

Jambazi

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2014
Posts
16,654
Reaction score
18,792
Aliyekuwa rais wa Marekani George HW Bush amelazwa hospitalini baada ya kuvunjika mfupa wa shingoni alipoanguka nyumbani kwake huko Maine.

Msemaji wake amesema kuwa kwa sasa yuko katika hali nzuri na kwamba kulazwa kwake huenda kukachukua muda mfupi.

Bwana Bush aliye na ugonjwa wa kutetemeka na hawezi kutumia miguu yake alisheherekea siku yake za kuzaliwa mwaka uliopita kwa kuruka angani.

Alilazimika kwenda hospitalini mwishoni mwa mwaka uliopita akiwa na tatizo la kupumua. Msemaji huyo Jim Grath amesema kuwa Bush huyo ambaye ndiye mkubwa miongoni mwa marais wanne wa zamani wa Marekani kutoka familia hiyo atalazimika kuvaa kifaa cha kuzuia shingo kutokana na kuanguka kwake hapo siku ya jumatano.
 
Aliyekuwa rais wa Marekani George HW Bush amelazwa hospitalini baada ya kuvunjika mfupa wa shingoni alipoanguka nyumbani kwake huko Maine. Msemaji wake amesema kuwa kwa sasa yuko katika hali nzuri na kwamba kulazwa kwake huenda kukachukua muda mfupi. Bwana Bush aliye na ugonjwa wa kutetemeka na hawezi kutumia miguu yake alisheherekea siku yake za kuzaliwa mwaka uliopita kwa kuruka angani. Alilazimika kwenda hospitalini mwishoni mwa mwaka uliopita akiwa na tatizo la kupumua. Msemaji huyo Jim Grath amesema kuwa Bush huyo ambaye ndiye mkubwa miongoni mwa marasi wanne wa zamani wa Marekani kutoka familia hiyo atalazimika kuvaa kifaa cha kuzuia shingo kutokana na kuanguka kwake hapo siku ya jumatano.
Wako wanne au wawili? George W H Bush na George W Bush. Mwingine John Eric Bush a.k.a Jeb ndo katangaza tu nia ya kutaka kupewa ridhaa na Wana-Republican agombee urais wa USA.
 
Mkuu huyu si ndio yule aliye sabsbisha vita vya ghuba? Yeye na Bush mdogo mikono yao yanuka damu
 
VITA YA GHUBA INATUHUSU NINI? SiSI tunataka katiba ya Warioba. Full stop.
 
Wako wanne au wawili? George W H Bush na George W Bush. Mwingine John Eric Bush a.k.a Jeb ndo katangaza tu nia ya kutaka kupewa ridhaa na Wana-Republican agombee urais wa USA.

Sio John Eric Bush,ni JOHN ELIS BUSH a.k.a JEB Bush.
 
Biblia imeandikwa aonywae mara nyingi akishupaza shingo atavunjika ghafla na asipate dawa!
 
Biblia imeandikwa aonywae mara nyingi akishupaza shingo atavunjika ghafla na asipate dawa!

Mkuu ni sawa lkn si dhani km Biblia ina maana km unavyofikiria wewe maana Nukuu yako haina uhusiano na huu uzi,Hapa inaonyesha kuwa ilikuwa ni ajali tu!,Kushupaza Shingo Kibiblia haina maana ya kukaza Shingo bali ni Kutotaka kubadilika kimatendo au kimtazamo,au ni kuifanya mioyo yetu migumu na hivyo kutoisikia sauti ya Mungu kupitia Wajumbe wake.
 
Huyu shetani kumbe bado yuko,, Damu za watoto aliowaua Iraq zinamlilia sasa hivi
 
Natamani afe kifo cha mateso makali kutokana na uovu mwingi alio fanya.

HAPO WANADAMU TUJIFUNZE, HATA UKIWA NA CHEO KIKUBWA KIASI GANI AU NGUVU KIASI GANI, MWENYEZIMUNGU AKIAMUA AKUTIE KATIKA MKONO WAKE UTAJUTA.


WENGI WETU TUNAJISAHAU NA KUWAFANYIA WANADAMU WENGINE USHENZI KAMA VILE SISI HATUTO KUFA
 
Mtakufa nyie mnaomuombea afe, some people their brain are insanity, bush kaua mama zenu??????? Insanity mind
 
Back
Top Bottom