George Job: Simba haiwezi mechi za mtoano

Ngoja tuumize vichwa kuiwazia simba ambayo Kabla ya kutinga makundi huwa inacheza mechi za mtoano na inazishinda.

Mtu hujifunza kulingana na makosa.Sidhani kama watarudia makosa ya nyuma.

Tusubiri , usiku wa deni huwa haukawii kucha.
 
Huyo mtangazaji alichotaka kumaanisha ameshindwa kukiwasilisha, angesema Simba hawawezi kucheza nusu fainali. Na sio kama alivyotamka yeye kuwa Simba hawawezi kucheza mtoano.
Maahindano ya CAF kwanzia unaanza ya kwanza unaanza katika hali ya mtoano sasa timu inayotinga makundi kama hawawezi mechi za mtoano wanafikaje makundi? Ukija kwenye makundi nako ni mechi ya mtoano na ndio maana zipo zinazofuzu na zipo zinazobaki.
.Alipaswa kusema Simba hawana timu ya kuifukisha nusu fainali.
 
Mimi ni Simba damu, ila sina ninachomdai mpaka sasa huko CAF kwa hatua aliofika na kikosi chake.
 
Hawana Team Ya Kufika ¼ fainali wakati ndio hatua walioko mpaka Sasa?
 
Nilimaanisha nusu fainali
Sawa Mkuu.
.
Halafu hawai ndio hao wachambuzi wanalalamika mpira wetu unauliwa na uSimba na uYanga.
.
Wakimaliza malalamiko yao wanatumia robo tatu ya vipindi vyao redioni kuongelea Simba na Yanga.
.
Mwenzangu na mie Namungo au Kagera Sugar hata ushinde 7, utajadiliwa kwa sekunde thelathini tu.
.
Hawa watakuwa wanapata bahasha kutoka kwenye team Kubwa?
 
kitu gani cha Ajabu hoo, Simba hawana wachezaji wakutoa matokeo mazuri ugenini!
 
ila kumbuka mwaka juzi vs ud songo. mwaka huu vs galax, sema vile alikuwa na nafasi ya kuwa akitoka anashuka shirikisho. na hata kwenye mechi za makundi mara nyingi huruhusu magoli mengi ugenini na kufunga machache nyumbani kwa timu nyingi. kwa msimu huu kama ingekuwa ni head to head kwenye kundi lake angemtoa USNG pake ake. . japo mwaka jana alicheza mechi za makundi za ugenini vizuri sana, sema akabweteka game ya mtoano vs kaizer chief. na hata hii ya jumapili labda ashinde kwa range ya 3. vinginevyo itakuwa ngumu sana kwake kupita.
 
Wachambuzi ni wengi sana mpaka atuwaelewi, kwani hatua ya makundi sio hatua ya mtoano?,ni mtoano wenye mzunguko wa mechi sita home & away.

hatua iliyopo Simba ni hatua nyepesi kwa timu yeyote kuliko hatua iliyopita.
Unataka kusema kurekebisha makosa kwenye mechi mbili tu ya ugenini na nyumbani ni rahisi zaidi kuliko kerekebisha makosa kwenye mechi sita za kucheza nyumbani tatu na ugenini tatu?.Ngumu kumeza.
 
Si ndio yule aliyewahi kuwa kwenye Technical Bench la Real Madrid au sasa mnakiri kwamba zile zilikuwa ni promo tu.
 
Si ndio yule aliyewahi kuwa kwenye Technical Bench la Real Madrid au sasa mnakiri kwamba zile zilikuwa ni promo tu.
Kwani tofauti nn mkuu kwani wamedanganya?Ni hali ya kawaida hususani afrika tofautisha miundombinu ya kule na ya huku unadhani Pep Guardiola akija hapo Yanga mtachukua klabu bingwa ?Umeiona CV ya Kaze? Aliwapa Ubingwa gani kama si kumtimua
 
Kwani tofauti nn mkuu kwani wamedanganya?Ni hali ya kawaida hususani afrika tofautisha miundombinu ya kule na ya huku unadhani Pep Guardiola akija hapo Yanga mtachukua klabu bingwa ?Umeiona CV ya Kaze? Aliwapa Ubingwa gani kama si kumtimua
Sasa mnawachukua wa nini kama ndio hivyo.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…