Genius & Kichwa Panzi!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Genius & Kichwa Panzi!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MartinDavid, Jun 30, 2011.

 1. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Jana nchi yetu ilitembelewa na mmoja wa matajiri wakubwa duniani lakina hili siyo la kushangilia sana.. kwani nchi hii ni tajiri kuliko kichwa panzi anavyofikiria... na wala hatuitaji huo msaada kwa kinga ya malaria kama tungejipanga vizuri..

  Genius kaja kuangalia mabilioni ya dola yanavyofanya kazi kwenye miradi ya malaria... huku akiwa ameweka wazungu kusimamia hiyo miradi kwa imani na mafisadi wa nchi hii hata hata chembe... LOlll

  wakati hayo yakiendelea kesho Julai MOsi bei ya kila kila kitu inapanda nchi nzima...

  Maswali ya kujiuliza kwa kila Mtanzania>>

  1. Je ni kweli uchumi wetu unategemea Bia, Soda, Sigara??
  2. Je kodi za utalii na madini zinaenda wapi??
  3. Je nchi hii haina vijana wasomi wenye uwezo wa kuendesha ATL & Tanesco??
  3. Je Kupanda kwa faini za Polisi hadi elfu hamsini kutapunguza ajali barabarani.?? Au kutawanufaisha polisi kwa rushwa???
  4. Je Elimu yetu itatufikisha pale walipo wenzetu wa nchi jirani kwenye soko la ajira??
  5. Je malumbano ya kisiasa na itikadi kwenye Bunge letu chini na Mama makinda yana tija..


  Yako mengi sana na mengi yanamfanya masikini azidi kuwa maskini... Je nini kifanyike.....

  Jioni hii nilikuwa nimekaa duka moja hapa Mwanza kijana mmoja wa mwendesha toyo kaja kununua sigara kaambiwa 150 amelalamika wazi kabisa... Namnukuu jamani sigara zinapanda kesho nyie mmepandisha leo kutoka 100 hadi 150 kweli tutafika kwa hali hiii.. kimeniuma sana alivyokuwa akisema maneno hayo..

  Nikajiuliza hivi kupanda kwa bei kwa vitu nani anaumia?? Mfano BIa ikipanda mnywaji hawezi acha ataendelea ila bajeti ya home itazidi kushuka kwani mshahara haujapanda.. je nani anaumia....

  Mafuta ya kula ile ndoo ya lita 20 sasa ni 60 thao... toka 40 thao dec mwaka jana....

  Watanzania wenzangu tufanye nini kuikombia nchi yetu katika janga la umaskini, kuombaomba, maradhi,, na UFISADI???
   

  Attached Files:

 2. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,255
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  ha ha haaaa, kwa hiyo mkweree ndio kichwa panzi, duh! Hiyo kali!
   
Loading...