PostGE2025 Odemba ambana Faris kauli ya "Tukiwapoteza msiwatafute", Faris aomba radhi

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,329
Reaction score
4,174

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Kagera Faris Buruhan amesema kauli yake aliyoitoa katikati ya mwezi Aprili mwaka 2024 ‘Tukiwapoteza wanaomtukana Rais Samia polisi msiwatafute”, ilitafsiriwa tofauti akidai kipande cha video kilichosambaa mitandaoni kilikuwa ni sehemu tu ya mazungumzo yake aliyoyazungumza kwa kirefu

Burhan ameyasema hayo akizungumza na mtangazaji Chief Odemba wa kipindi cha Medani Kuu cha runinga ya Star TV siku ya Jumamosi ambapo hata hivyo ametumia fursa hiyo kuwaomba radhi Watanzania waliokwazika na kauli hiyo na kurejea msemo wa ‘Yaliyopita si ndwele tugange yajayo’

​
 
Odemba kamuingiza kwenye 18 akajaa akampiga kwenye MSHONO.
 
Baada ya mauaji ya kimbari ya Rwanda, watuhumiwa na washitakiwa walikuwa pia wale waliotoa kauli za shari na chuki zilizopelekea mauaji hayo.
 
Odemba yupo vizuri sana,Huyu jamaa alitaka kukwepa akajikuta anabanwa kwenye kona mpaka akakosa pakutokea
 
Nimeona hivi karibuni yule mnyambo wa uvccm aliyesema kuwa yeye na genge lake akipoteza watu polisi wasiwatafute akiwa amekula uteuzi wa kundi la uvvccm, sasa swali langu kitendo cha huyo mpoteza watu kupewa uteuzi huo ni kiashiria kuwa genge lililojipachika madarakani bila idhini ya watu limekufa hivyo linasubiri maziko tu baada ya Lissu kutoka tarehe 06/11/2026? naomba majibu wadau hasa wenye akili timamu.
 
nonsense 🐒
 
CCM UKIWEZA KUUWA UNAPEWA CHEO,UKIWEZA KUWATUSI WAPINZANI UNAPEWA CHEO, BADO MWAIPOPO,MWASHAMBAAAA HAWAJAPEWA VYEO
 
Back
Top Bottom