Mwanajeshi wa Congo, cheo cha Generali, alikabidhiwa majukumu na kupewa kanda yake ya uongozi.
Kanda hiyo, ikawa ni moja wapo wa maeneo yenye watutsi waitwao wanyamlenge.
Alivyoenda huko, akatembelea maeneo mbali mbali. Kufika huko, akakutana na wazee wa eneo hilo, kumuelezea changamoto wanazokumbana na zo.
Baada ya maongezi, kama inavyoonekana, maana hao watu ni wafugaji, walijikalia chini kwenye nyasi, wakapigwa na picha.
Sasa hili sakata la vita lilipoanza, nae akawa amekimbilia Uvira.
Wakakumbuka aliwahi kupiga picha akiwa na watutsi. Moja kwa moja ikatafusiliwa kuwa ni usaliti, hakutakiwa hata kuonana nao. Kosa likawa ni hilo, na likapelekea kuuliwa na kundi la wazalendo.