General tyre yageuzwa ukumbi wa harusi!! Hii ni laaana?

mujungu

Senior Member
Nov 1, 2010
143
55
Kwa sisi wa humu humu huwa tunapata story kuwa Ulaya Nyumba za Ibada zilikosa waumini, zikageuzwa Nyumba za starehe nk. Hapa kwetu leo viwanda tumegeuza sehemu za kufanyia harusi , video shoo , maghala na sehemu za kupata vyuma chakavu!!! inatisha sana. Mara kadhaa nikelekea nyumbani njiro, huwa naumia roho sana nionapo ndani ya Kiwanda cha General Tyre Kumepambwa kwa ajiri ya harusi na mengineyo mengi, Kwangu mimi hii ni laana. hatuoni haibu hata kidogo. Kweli sehemu ya kuzalisha ajira na kuchangia uchumi kukua tunafanya ukumbi wa harusi. TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, NA TUTAENDELEA KUWA MASKINI.

NAWASILISHA .
 
Mkuu hiyo ni tisa lakini kumi ni pale utakapoona sehemu hiyo hiyo inakuwa na sehemu ya kufanyia makongamano ya vifo. Tanzania kwishney.
 
viongozi wako busy na matamasha. wadogo nao wako busy kuchonga michongo kutengeza mafurana, caps, scaff, na tenda ya vyakula na vinywaji, VIWANJA VYA MNAZI MMOJA VIMEGEUZWA SEHEMU YA KUHALALISHA UFUJAJI WA KODI ZA WATANZANIA.
 
pole sana mzee. ila mi naona bora ya hayo kwa kuwa ndo tunayoyaweza kuliiko kulazimisha jengo litumike kwa kiwanda huku haiwezekani. Mpoto alisema hata madarasa ikibidi tuondoe wanafunzi ili tufuge kuku. duh. kama wamejimilikisha ndo tatizo ila kubadili matumizi poa tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom