Halafu kuna watu wanasema Askari hawapendwi, hongera kwa wana Geita mliomuokoa Askari
Chuki dhidi ya Polisi imechangiwa 98% na ccm!
Just imagine vile chama cha majambazi wamegeuza jeshi letu la polisi kama tawi lao, wanalitumia kihuni kufanikisha malengo yao ya kisiasa wakati huo huo maslahi ya askari hao kubaki duni, yani wanatumika kama toilet paper.
Hapa ndipo umuhimu wa katiba mpya unapoonekana, hatuwezi kuwa na Igp anayeteuliwa na mwanasiasa(rais), maRPCs wanaoteuliwa na ikulu(kwenye kivuli tunaona wameteuliwa na jeshi la polisi), na maOCDs wanaowekwa kwa utaratibu huo huo. Upandaji wa vyeo wa hawa watu umekaa kisiasa zaidi, RPC ili apande cheo lazima "awasulubu" na kuwasingizia kesi wapinzani, OCD ruhusu mikutano ya wapinzani wilayani kwako uone kama utapanda cheo!
Tunahitaji katiba mpya ili kuondoa huu ushenzi wa matumizi ya kihuni ya jeshi letu la polisi, hatutaki tena taasisi hii kutumika kisiasa, tunahitaji uteuzi wa viongozi wake usihusishwe wala kuingiliwa na wanasiasa! Sheria ya jeshi la polisi na wasaidizi wake irekebishwe, waziri wa mambo ya ndani asitoe maelekezo yake ya kisiasa kwa polisi!
Jeshi la polisi liwe autonomous, hao askari ni wazazi, ni ndugu zetu, ni jamaa na marafiki, tunawapenda kama tu wataacha kufungamana na wahuni wa kijani!