ukawa2020
JF-Expert Member
- Apr 1, 2016
- 339
- 1,314
John Mnyika, Patrobasi Katambi, Conchester Rwamulaza na Tumaini Makene wako kituo cha polisi Geita wakihojiwa kwa kosa la kuweka Bendera za CHADEMA kwenye gari zao.
# Huu ni utawala wa kuwekwa kwenye kumbukumbu
======
Maelezo haya ya ziada ni kwa mujibu wa Tumaini Makene
MSAFARA WA MNYIKA ZIARA VIKAO VYA NDANI WAKAMATWA NA POLISI GEITA
Msafara wa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, wakati unajiandaa kuondoka hotelini mjini Geita kwenda kwenye ziara ya vikao vya ndani, umekamatwa na Jeshi la Polisi na kuamriwa kwenda Kituo cha Polisi kuonana na OCD.
Kwa maelezo ya maaskari waliokuwa wamejaa gari nzima wakiwa na silaha za moto, wakiongozwa na OCCID, wamesema kuwa wamepewa maagizo ya kuwapeleka kituoni Mnyika na msafara wake kwa sababu eti wametumwa kuwakamata kwa sababu ni makosa kwa gari kupeperusha bendera ya kibunge katika jimbo la mbunge mwingine.
Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge zinazotoa maelekezo ya matumizi ya bendera za kibunge, Mbunge yeyote anaweza kupeperusha bendera mahali popote isipokuwa Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar. Kanuni ya 151 (2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge.
Msafara wa Mnyika uliokamatwa na kupelekwa polisi ulikuwa una magari mawili yenye bendera hizo ambazo polisi wanasema ni kosa.
Mnyika aliambana na Mwenyekiti wa BAVICHA Patrobas Katambi, Ofisa Habari wa CHADEMA Tumaini Makene, Katibu wa Mkoa wa Kagera Conchesta Rwamlaza (MB), Mkiti wa BAVICHA Mkoa wa Geita Neema Chozaile, Kamanda Anarose na makada wengine.