Geita: Mahabusu 17 watoroka Mahakamani

Geita: Mahabusu 17 watoroka Mahakamani

Good Father

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2014
Posts
10,320
Reaction score
18,599
Jumla ya watuhumiwa 17 wa makosa mbalimbali waliokuwa wamehifadhiwa kwenye ukumbi wa jengo jipya la Mahakama ya Mkoa wa Geita kusubiri mashauri yao kutajwa mahakamani, wametoroka katika mazingira ya kutatanisha.

Awali Mahabusu hao walikuwa wamehifadhiwa katika Ukumbi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Geita kabla ya kuhamishiwa katika ukumbi wa jengo jipya la mahakama hiyo linaloendelea kujengwa ili kupisha kikao cha Mahakama Kuu kinachoendelea mbele ya Jaji Ismail.

Mkuu wa Mashitaka, Ofisi ya Mashitaka Mkoa wa Geita, Bibiana Kileo, ameeleza kuwa mahabusu waliotoroka hawahusiani na kikao cha Mahakama Kuu kilichoanza mei 20 hadi Juni 16 mbele ya Mhe. Jaji Ismail kwa ajili ya kusikiliza na kutolea maamuzi kesi za mauaji.

Mkuu wa Magereza Mkoa wa Geita, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Robert Rumanyika amesema Jeshi hilo halijaanza utaratibu wa kupeleka mahabusu mahakamani kama ilivyo kwa baadhi ya Mikoa hapa nchini na kwamba tukio la kutoroka kwa mahabusu hao haliko chini yake.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo, akizungumza kwa sharti la kutokupigwa picha, amesema asingependa kuzungumzia tukio hilo kwa sasa kwa hofu ya kuvuruga upelelezi.

Inasemekana mahabusu hao walikua chini ya ulinzi wa polisi.

Chanzo: EATV

 
Wakati wenzako wanatoroka ole wako ubaki nyuma yaani wenzako wanasepa halafu ww useme una case ndogo usisepe, aisee hicho kichapo utachochezea mpaka utachakaa watakuwa wanakuuliza wakati wenzako wanatoroka kwa nini hukupiga yowe!
 
Mbona huwa kuna ulinzi mkali imekuaje watoroke kirahisi namna hiyo? Inamaana hao askari waliwaacha watoroke kwa makusudi
 
Askari wana njaaaa na haya ndio matokeo yake,hapo hamna cha nini wala nini hamna kufichiana aibu Mahabusu 17 hawawezi kuondoka kirahisi hivyo Kuna askari kala mtonyo kawaachia..Hao mahabusu walikua na mpunga wame ji organise na askari wa zamu alikua mwenye tamaa Kapokea mpunga kawaachia.

Hamnaga watu wanatoroka kizembe hivyo TANZANIA hiii...semeni tu mmewaachia MMESHINDWA gawana mtonyo mmezulumiana huko mnajitia wametoroka..Kwendeniiii kuleee
 
kuna asikari was lmagereza kazoa mpunga mzuri, katika ile kuwakabidhi polisi ndipo akatoa ishara wasepe.
hapo hela si pungufi ya m20 imetembea na kama huenda wengine tutatangaziwa wameuawa na polisi walipoambia SISIMA wakakaidi.
safisha jeshi la polisi
 
Back
Top Bottom