kunena
JF-Expert Member
- Nov 29, 2016
- 506
- 717
Kikosi maalum cha mashambulizi ya kutatua kero za wanyonge kijulikanacho kama GDK (Gambo, Daqqaro, Kihamia) kimeanza kazi hiyo kwa kishindo kila mmoja akitumia staili yake lkn wote wakilenga kutatua kero kwa wananchi wa Arusha . GDK ilianzia na mheshimiwa Mrisho Gambo ambaye ni RC Arusha kutembelea wilaya zote 6 za mkoa wa Arusha wiki nzima kila wilaya kusikiliza na kutatua kero hizo kwa kufanya ziara na kukaa huko huko vijijini walipo wananchi ambapo ufanisi wake ni mkubwa mno.
Baadaye mkurugenzi wa jiji la Arusha Athumani Kihamia kufanya ziara za vikao vya kazi ktk kata 23 kati ya 25 za Jiji la Arusha kuongea na watendaji wa kata, mitaa, maafisa afya, Maendeleo ya jamii, kilimo na mifugo, waratibu elimu kata, wakuu wa shule za sekondari na walimu wakuu wa shule za Msingi pamoja na waganga wakuu wa vituo vya afya na zahanati zilizopo ktk kila kata
Alisisitiza utendaji kazi kwa bidii uaminifu na weledi ktk kuwatumikia wananchi hasa wa hali ya chini bila kuwabagua kwa itikadi ya aina yoyote huku akitoa tahadhari kwa watumishi watakaozembea kuwa hawatabaki salama kamwe.
Kabla ya ziara hiyo mkurugenzi huyo alifanya vikao vya kazi na watumishi wa makao makuu ya Halmashauri hiyo kwa idara za utawala na utumishi, sheria, ardhi, fedha na biashara, Maendeleo ya jamii, afya, elimu, ujenzi na barabara, kilimo na mifugo, maji uchumi pamoja na manunuzi akiwakumbushia wajibu na majukumu yao hasa kwa kuzingatia ilani ya chama cha mapinduzi na hotuba ya Nov 2015 ya mheshimiwa rais aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa bunge. Ambapo vikao hivyo vimeleta matokeo chanya ya uwajibikaji wa watumishi wa jiji waliokuwa baadhi yao wakifanya kazi kwa mazoea ikiwemo kuchelewa kazini na kutoa lugha chafu kwa wananchi wanaohitaji huduma serikalini.
Na sasa mheshimiwa mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Fabian Daqqaro ameanza ziara kwa kishindo ktk kata zote akisikiliza na kutatua kero na matatizo yanayowakabili wananchi wa wilaya hii. Ziara zake zimekuwa na faida kubwa sana kwa wananchi.
DC huyo anaongozana na baadhi ya wataalam wa halmashauri ya jiji la Arusha na kamati ya ulinzi na usalama pamoja na katibu tawala machachari anayetanguliza uzalendo sikuzote ndg David Mwakiposa. Maelekezo ya RC anayoyatoa ktk mikutano ya wananchi yanafuatiwa na mheshimiwa DC kutoa msisitizo na ufafanuzi mtaa kwa mtaa ktk mikutano ya hadhara kisha mheshimiwa mkurugenzi wa jiji kufanya usimamizi wa utekelezwaji wa maagizo mbalimbali hatua kwa hatua kwa uangalifu mkubwa.
Utendaji wa wateule hawa wa rais pia unaratibiwa kwa ustadi mkubwa na katibu tawala mkoa ndg Richard Kwitega na katibu tawala wilaya ndg David Mwakiposa. Ushirikiano huo wa viongozi hao wakuu 5 na wengine wa jijini Arusha umewafanya wananchi kuondokana na hali ya kuchanganyikiwa wanapotafuta huduma ktk taasisi za umma na hivyo kuwa na imani kubwa na serikali yao ya awamu ya 5 ambapo hapo awali ilionekana kupotea.
MY TAKE:
TUTAONGEA MKONO VIONGOZI HAWA NA KUWAOMBEA ILI WAZIDISHE NA KUDUMISHA KASI HII YA KUWATETEA WANANCHI WA ARUSHA ILI KUHARAKISHA MAENDELEO