Gazeti la Uhuru: CHADEMA waingiza vijana msituni

Gazeti la Uhuru: CHADEMA waingiza vijana msituni

Basi hatua stahiki zichukuliwe,au ndio serekali legelege?
 
Kenya hakuwahi kutokea fuka/ kenge kuiba mali za umma kuhama chama na kugombea uraisi, hakuwahi mtu kufanya haya yanayo jiri hapa infact hayo mawazo ni ya kiwaki! Je unayakumbuka ya LIBYA

Huo upuuuzi wako peleka Lumumba,sisi tumeshaamua mabadiliko na kuitupa jalalani ccm
 
Hivi jamani hao CHADEMA hawana kitengo cha wanasheria kuwapeleka ili gazeti la UHURU mahakamani...hata kama mahakama haitafanya kitu baadaye wanaweza fanya utaratibu wa kuwaandikia mahakama ya ICC - The Hague kama angalizo. nadhani ambao mko karibu na hao CHADEMA mnaweza saidia kuwapa ushauri wasikae kimya kabisa na ikibidi waandike barua hata kwa umoja wa mataifa.
 
Gazeti la Uhuru limeendelea na propaganda chafu kuvuruga amani ya nchi.Gazeti la leo uk.5 limeripoti kuwa CHADEMA imeingiza vijana msituni kwa ajili ya kujiandaa kufanya vurugu uchaguzi mkuu.Cha ajabu ni kwamba hata jina la msitu wameshindwa kutaja,kwa kuwa ni kosa la kuhatarisha amani wameshindwa hata kuonyesha kama wameripoti polisi
Naona gazeti hili inachotaka kusema ni kuwa hatuna vyombo imara vya ulinzi na mpaka itokee vile watu waende msituni. Hii ni kudharilisha vyombo vy ulinzi. Naamni tuna vyombo vya ulinzi imara na swala la watu kwenda msituni niuzushi wa gazeti lililoamua kujitoa weledi na kuleta uchochezi nchini.
 
Najaribu kumpigia huyu mwandishi kwa ile namba yake.,amezoea namba ya TIGO kama sikosei.naambiwa mamba nayopiga inatumika.Naona hili gazeti linachochea vurugu.limekuwa lakichochezi zaidi.serikali inafanya nini?
 
Mambo haya ndiyo yalileta vurugu Kenya. Kulikuwa na redio na magazeti yaliyoaminisha watu mambo ya uongo. Mi nahisi wao ndo wana andaa jeshi. Tumeona ya Masaburi juzi, lakini hata Polisi na NEC walikaa kimya. Kimya hiki kinaashiria Luna jambo linapikwa kwa pamoja. Likitokea LA kutoka, lawama zote watabebesha UKAWA. Ndo zao. Tumeona msbslozi na waangalizi wamezibwa midomo tayari.
CHADEMA ni kweli wana vikundi wanaviandaa kwa ajili ya kuendesha mauji. Kama Dr Slaa CHADEMA walitaka wamuue ila sasa kakimbia, kwani watashindwa kuwa na vikundi? Kama Bishop Gwajima anatoa walinzi kwa Dr Slaa je CHADEMA watakosa makundi ya vijana wauaji? CHADEMA mwisho wenu ni 25/10!
 
CCM na battalion za GREEN GUARDS wanaendeleaje na mazoezi?
 
Tunatarajia CHADEMA wachukue hatua kukanusha na hatua zingine za kisheria, la sivyo tutaamini kuwa ni kweli. Lakini pia NEC, Polisi na TCRA pamoja na chombo kinachowaunganisha waandishi wa habari kwenye maadili tunasubiri ufafanuzi wao.
 
Back
Top Bottom