Gazeti la 'udaku' Uingereza kufungwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gazeti la 'udaku' Uingereza kufungwa

Discussion in 'International Forum' started by sulphadoxine, Jul 8, 2011.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  [​IMG]

  Gazeti la kila Jumapili la News of the World la Uingereza lilatoka kwa mara ya mwisho siku ya Jumapili, siku chache baada ya tuhuma nzito kuliandama gazeti hilo.

  Mwenyekiti wa kampuni inayomiliki gazeti hilo la News International, James Murdock amesema toleo la Jumapili ndio litakuwa la mwisho.
  Gazeti hilo la kila wiki linatuhumiwa kufanya udukuzi wa simu kwa waathirika wa uhalifu, watu mashuhuri na wanasiasa.

  Siku ya Alhamisi, polisi wa Uingereza walisema watawatafuta watu wapatao 4,000 ambao wametajwa kufanyiwa udukuzi katika nyaraka ambazo zimepatikana.

  Gazeti hilo ambalo linasomwa zaidi nchini Uingereza limekuwa likitoka kwa miaka 168.

  News of the World ambalo huuza nakala takriban milioni 2.8 kila wiki, limepata umaarufu kwa kutoa habari motomoto za watu maarufu na kufichua kashfa mbalimbali.

  Ofisi ya waziri mkuu wa Uingereza imesema haihusiki kwa njia yoyote katika uamuzi wa kulifunga gazeti hilo.

  Bw Murdoch amesema hakuna matangazo yoyote yatarushwa katika gazeti hilo wiki hii, badala yake nafasi za matangazo zitatolewa kama sadaka, na hata mapato ya gazeti hilo yatatolewa kama msaada.

  Kampuni ya News International imegoma kusema lolote kuhusiana na uvumu kuwa huenda gazeti lake la Sun sasa litatoka kila siku hadi Jumapili.
   
 2. m

  menny terry Senior Member

  #2
  Jul 10, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 187
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  bado mwanahalisi siku si nyingi litafungwa limezidi Umbea.
   
 3. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #3
  Jul 10, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mambo ya wazungu bwana!.Utayaweza?.
  Jambo doogo linafanywa kuubwa halafu akina sie tunalidakia
  .Hujawahi kuona ukurasa wa mbele habari za paka aliyefia ndani ya pipa la taka.
  Hebu fafanua hapo.Ina maana gani ikiwa gazeti limefungwa halafu linatoka na pesa ya matangazo itatolewa kama sadaka.
  Kweli wewe unaamini hili gazeti la miaka 168 linafungwa kwa shutuma tu ati za kujipenyeza kwenye simu za watu na kutafuta habari !.
   
 4. L

  LENIN'S Member

  #4
  Jul 10, 2011
  Joined: Mar 13, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Elewa,chapisho la mwisho la leo matangazo yake fedha itatolewa sadaka
   
 5. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kusema uwongo na kutoa visingizio wanaposhindwa na jambo ni moja ya tabia kubwa ya wazungu hasa waiengereza.Kumbuka viongozi wakuu wa Marekani ni ndugu sana na waiengereza.
  Mambo yalipokuwa magumu kwenye biashara ya watumwa wakajifanya wanapinga biashara hiyo inayoendeshwa na waarabu.Walipotaka kuiba mafuta Iraq wakasema wanakwenda kukamata silaha za maangamizi.Libya nako ati Gadafi anauwa watu bure pamoja na watoto na akinamama.
   
 6. S

  Sharo hiphop JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 662
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Magazeti yetu ya udaku yameegemea upande wa wasanii zaidi. Kwa hiyo inaamika wanaweza wasiwe na ubavu wa kutisha kushawishi utawala kufungia, mfn kiu ya jibu, ijumaa, risasi, etc.
   
Loading...