Safi sana Serikali,
Mwalimu Nyerere aliisha sema UHURU BILA MIPAKA NI SAWA SAWA NA WENDAWAZIMU. Hakuna serikali duniani ingeweza kukubali uchonganishi na uzushi wa habari za MWANAHALISI. Na wameisha onywa zaidi ya mara 10 hawasikii, hiyo ndio dawa yao. Sasa Kubenea atafute kazi nyingine, hii ya uandishi amekiuka maadili yake
kweli kabisa mkuu Taharir square ni muhimu sana tena kwa kupigania haki na ukombozi wa nchi wameona hawana jinsi, sasa wanatumia mbavu. Lakini wanacho ni shangaza wamesema gazeti limechapishaa habari zinazo hatarisha amani ya nchi wakashindwa kueleza ni habari gani, kwakweli hapa naona serikali ya mwabepande inazidi kujichanganya yenyewe na kuwafanya watu wafungue macho.
Yaani nyie mmekuwa kama mimi vile.
Nimemchukia sana Kubenea toka ile makala ya tarehe 18/07/2012 kani anapenda sana sifa kwa kusema ukweli kuhusu Serikali.
Anajifanya anajua sana upelelezi sasa si angelienda kuomba kazi Usalama wa Taifa tujue moja kuwa ni mpelelezi.
Kisha upelelezi wake siku zote ni kuivua nguo hadi ya ndani Serikali ya CCM tu, kwanini asipelelezi Majambazi????
SIMPENDI HUYu!!!!!!!!
MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
duh,kweli tanzania tumethubutu tukashindwa,
source ya ukweli ntapata wapi tena.
Nitakutumiajamani mwenye makala za uchunguzi ziivyoandikwa na gazeti hili juu ya Dr Ulimboka anitumie kwenye PM maana akiziweka hapa mods hawakawiikuzifuta hata kama kuna blog ambayo imeweka naomba link tafadhali...
Serikali inadai kuwa Mwanahilisi limekuwa "linachapisha habari na makala zenye kueneza na kujenga hofu kwa jamii".
Hivi nini kimeeneza na kujenga hogu kwa jamii, kutekwa na kuteswa kwa Dr Ulimboka na baadae movie ya Kova au taarifa za kichunguzi za gazeti la mwanahilisi?
mbona radio imani inayohubiri chuki za kidini kila siku haifungiwi?? kuna double standards kwenye media???