Gazeti la mtanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gazeti la mtanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sulphadoxine, Jul 8, 2011.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Gazeti la mtanzania la leo tarehe 8/7/2011 front page kuna maoni kuwa Dr.Slaa hamtendei haki Andrew chenge.
  Sasa sijaelewa hawa mtanzania wana nia gani?
  Sijui wanajamvi mnalionaje hili swala,au ndio kazi ya mapacha wa tatu.?
   
 2. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hii inanikumbusha thread tulikuwa tunaichangia jana humu jamvini, kuhusu mfanyakazi wa Habari Corporation kulalamika kutolipwa mishahara yao na makato yao kutofikishwa PPF. Mimi niliwaambia kwamba haya wameyataka wenyewe kwa kumfurahisha mmiliki na washirika wake na huku upande mwingine wakiyaua magazeti hayo na kujiua wenyewe bila kujua. Gazeti kama hilo nani atalipa uzito kama habari zenyewe ni za kipuuzi namna hiyo. Leo ukienda kwa wauza magazeti watakuambia gazeti hilo wananunua nakala chache sana lakini ndilo linaloongoza kwa nakala zake kurejeshwa bila kuuzwa.

  Hainishangazi sana kusikia hili likiwa limetoka kwenye gazeti la Mtanzania ambalo sasa limegeuka kua kijarida cha udaku na mipasho. Kichefuchefu kitupu na kama kuna mtu alidhani kwamba linaweza kunukuliwa basi alikosea sana.
   
 3. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  "Katibu mkuu wa wa chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) Dr W.P.SLAA kwa kushirikiana na mbunge wa singida masharika TUNDU LISSU, wanaendelea kumshambulia mbunge wa bariadi magharibi na mwanasheria mkuu wa zamani andrew chenge.
  Msimamo wa viongozi hao bila shaka ndiyo msimamo wa CHADEMA juu ya chenge na sakata la rada"
  Hayo ni baadhi tu ya maneno kwenye hilo gazeti la mtanzania.
   
 4. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 741
  Trophy Points: 280
  Hili gazeti huwa sina haja ya kuangalia vichwa vyake vya habari.
   
 5. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  mkuu mbna ujasoma mpka ndani au kama vp weka link hapa ili tuweze kuona
   
 6. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kitu kinacho nishangaza wameweka kama maoni front page,hivi wao awauhi ufisadi wa mzee wa vijisenti au inakuaje hapa,maana kama vile wanapinga kushambuliwa kwa chenge,na kwa mtindo huu ufisadi utaendelea vizazi na vizazi kama wapuuzi wachache(waandishi wa habari) wataendelea kutetea maovu.
   
 7. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu link bado sijaipata nimeingia kwenye web yao bado awajaweka,hila haya ni maoni ya mhariri Deodatus Balile,na kama unakumbuka juzi nape alitembelea pale habari corporation na alikutana na huyu balile pamoja na bashe.
   
 8. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kha! Hili gazeti nalikumbuka, ni la zamani!!! Kwani bado linaendelea kuchapishwa! Nilishalisahau. Sasa mtatuletea mpaka habari za gazeti la Motomoto au Mfanyakazi.
   
 9. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Tanzanian media is very biased because most media houses are either owned by politicians, parties or businessmen with political agendas. It is very hard to find an unbiased media outlet in Tanzania.
   
 10. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #10
  Jul 8, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mkuu ungetuambia wameandika nini maana wengine tupo mbali kidogo.
   
 11. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Na mwisho kabisa huyu balile anasema"Tunatoa rai kwa watanzania kuwa makini na kauli za ghiliba za kujenga uchonganishi.Ikumbukwe kuwa Dr.Slaa amekwisha kusema maneno mengi ya uongo,yakiwamo ya makontena ya kura.Kama kweli kuna ushahidi wa kumbana chenge ,huu ndiyo wakati wa kumbana.Kama Dr. Slaa hawezi kudhibitisha madai yake,anyamaze.Uongo, chuki,uzandiki na kujitafutia umaarufu mwepesi wa siasa vitalihgarimu taifa"

  BADO NINAMSHAKA NA HUYU BALILE KAMA NI MTU MWENYE UWEZO WA KUFIKIRI AU LAAHAAA!KWASABABU HILI SWALA LIPO WAZI NA YEYE KAMA MHARIRI NADHANI ILE BARUA YA SFO ALIIPATA SASA SIJUI LEO ANATUMIA NINI KUFIKIRIA JE NI TUMBO AU MIGUU?


   
 12. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #12
  Jul 8, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  umelitafuta ukalisoma? Au untafuta sifa tu kuwa nawewe leo umepost kitu humu?
   
 13. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #13
  Jul 8, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Nadhani utakuwa unamatatizo,either unafikiri kutumia tumbo au bodi.
   
 14. PAS

  PAS JF-Expert Member

  #14
  Jul 8, 2011
  Joined: May 3, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mmiliki wa mtanzania ni rostam.. Na mkurugenzi ni husen bashe.
  Ivo picha halisi inaonekana


   
 15. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #15
  Jul 8, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Najuzi nape alienda pale kukutana na bashe pamoja na huyo balile.
   
 16. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #16
  Jul 8, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwa uelewa wangu finyu, bado sijapata kuelewa unamaanisha nini. Balile ndiye Mhariri Mtendaji wa gazeti hili. Yeye ndiye anayetoa mwelekeo wa gazeti na falsafa yake. Sasa unawezaje kutofautisha Balile na msimamo wa gazeti? Then Nape kutembelea Habari Corporation, kama ambavyo ametembelea vyombo vingine vya habari, kunabadilishaje msimamo wa gazeti?

  Hawa jamaa hawakuwa na dhamira ya kutengeneza faida kwenye magazeti haya. Walitaka kufanikisha ajenda yao. Hata hivyo ni masiktiko kwamba hata hiyo ajenda hawataifanikisha kwa sababu magazeti yao yamebaki kuwa na faida ya kufungia maandazi tu, na siyo kama chanzo cha habari. Sasa unadhani kuna mtu anajua kwamba Chenge ametetewa, kama hata kununuliwa halinunuliwi?
   
Loading...