Gazeti la Majira: CUF walaani Udini unaodaiwa kuenezwa na Mwenyekiti wake

Huu ni upuuzi, sisi tunachotaka na kulilia ni mtu kuchaguliwa kwa misingi ya kikatiba sio misingi ya msikiti au kanisa ndio maana tuna kina Pengo na Shaban Bin Simba kama kadinali na Sheikh Mkuu wa Tanzania kwa mfuatano

Muongeze na katibu mstaafu wa baraza la maaskofu Padre Slaa
 
Tumia akili kidogo tu kufikiria na acha ukada wa Chama chako:

Mtoto wa Kanisa na kiongozi wa kanisa kwa miaka kumi natakapokuwa Ikulu yenye Waislamu na Wakristo wenye idadi karibu sawa,tene waislamu wakiwa wamepigika tokea uhuru,hivyo hali itakuwaje

Mimi sijui CHADEMA walitumia busara na hekima gani kumfanya Padre na katibu mkuu mstaafu wa baraza la maaskofu tanzania kuwa mgombea wao uraisi na katibu mkuu wa chama katika nchi kama hii zaidi ya kutafuta mteremko wa kisiasa.

Sijatoka nje ya mada,alichooropoka Lipumba ni ukweli aliouongea mahala pasipo stahiki kwa kuwa waislami ndi mtaji wake,na uropokaji huu ni zao la busara na hekima za CHADEMA.

Ahadi alizozitoa Dr. Slaa kama angekua Rais hata mimi muislam ningefaidika nazo kama bei ndogo ya saruji ningeweza kumalizia kibanda changu kinyerezi, au kuboresha usafiri wa treni na reli zake mi ningeweza kufaidi ugali na dagaa walioshuka bei toka Kigoma. Hebu fikiria mfano kiwanda cha saruji wazo kinatumia gesi inayotoka Songosongo inayoletwa na Songas lakini katikati kuna mtu mwingine anaitwa Pan African gas naye anadalalia bei hivyo kuongeza gharama ukitia na ujanja wa wawekezaji tunanunua saruji 13500/= kwa Dar ingekua 5000 au 6000 mi ni singekua najidai kwenye kibanda changu hebu angalia bei ya saruji ya Luck inavyouzwa Pakistani Cement Prices In Pakistan | Cement Rates In Pkr | Prices in Pakistan ( 1usd= 98.46 pakistan rupee) au hii link Price Of Cement In China-Price Of Cement In China Manufacturers, Suppliers and Exporters on Alibaba.comCement inayoonesha bei ya tani 1 ya saruji China (mifuko 20 ya kilo 50) ni kati ya USD 50-80 kwa tani sawa na usd 2.5-4 kwa mfuko ( weka kwenye madafu mwenyewe harafu tumia law ya one price Law of one price - Wikipedia, the free encyclopedia hapa mwenyewe kisha uniambia huyu DR. Slaa tuliyeona eti Padre asingenisaidia kumaliza kibanda changu kinyerezi? Acheni udini jamani tuchague viongozi wacha mungu wenye kuweza kututetea sisi kama watanzania sio kama waislamu au wakristo
 
CUF ni waasisi wa udini , ni waasisi wa siasa za kuwagawa watu, na ccm aidha kwakutambua ama kutotambua wamekuwa nyuma yao daima.
kama alivyosema kuwa ilifikia mahala akamsupport Kikwete sio kwa ushindi wake kumbe kwa maslahi ya dini yake. huyu ni kiongozi hamnazo kuliko wote ambao cuf imewahi kuwa nao...mdini , mdini , mdini
mkuu sio yeye tu wapo wengi, mfano yule mwarabu koko kutoka zanzibar, sijui anajiita Ismail jussa, aliwahi kutoa kauli za kuwagawa watu kwa dini zao! Cuf ni janga kwa mshikamano wa taifa letu!
 
Prof.Ibrahimu Haruna Lipumba siasa zikishafikia hapo ndiyo kwa heri mzee wangu, tutakusahau katika majukwaa haya siasa.
 
Ahadi alizozitoa Dr. Slaa kama angekua Rais hata mimi muislam ningefaidika nazo kama bei ndogo ya saruji ningeweza kumalizia kibanda changu kinyerezi, au kuboresha usafiri wa treni na reli zake mi ningeweza kufaidi ugali na dagaa walioshuka bei toka Kigoma. Hebu fikiria mfano kiwanda cha saruji wazo kinatumia gesi inayotoka Songosongo inayoletwa na Songas lakini katikati kuna mtu mwingine anaitwa Pan African gas naye anadalalia bei hivyo kuongeza gharama ukitia na ujanja wa wawekezaji tunanunua saruji 13500/= kwa Dar ingekua 5000 au 6000 mi ni singekua najidai kwenye kibanda changu hebu angalia bei ya saruji ya Luck inavyouzwa Pakistani Cement Prices In Pakistan | Cement Rates In Pkr | Prices in Pakistan ( 1usd= 98.46 pakistan rupee) au hii link Price Of Cement In China-Price Of Cement In China Manufacturers, Suppliers and Exporters on Alibaba.comCement inayoonesha bei ya tani 1 ya saruji China (mifuko 20 ya kilo 50) ni kati ya USD 50-80 kwa tani sawa na usd 2.5-4 kwa mfuko ( weka kwenye madafu mwenyewe harafu tumia law ya one price Law of one price - Wikipedia, the free encyclopedia hapa mwenyewe kisha uniambia huyu DR. Slaa tuliyeona eti Padre asingenisaidia kumaliza kibanda changu kinyerezi? Acheni udini jamani tuchague viongozi wacha mungu wenye kuweza kututetea sisi kama watanzania sio kama waislamu au wakristo

Yako wapi Maisha bora kwa kila Mtanzania tuliyoahidiwa 2005?

Ni ngonjera za kisiasa tu za kuwapeleka watu Ikulu ili wakafanye mabo yao,hemu amka wewe mfu wa akili.
 
So kama ni maoni binafsi CHADEMA waliyakubali au waliyapinga? That is the question. Lipumba na yeye alienda pale kama muumini tu! Tatizo liko wapi?
lipumba ana tatizo la kupenda sifa, anapenda kujionyesha kwa waislamu kuwa yeye ni bingwa wa kuwatetea waislamu kuliko kikwete, ndo maana muda wote hupenda kuwaangukia masheikh ili wamuonee huruma, kumbukeni redio imani ilikuwa inapenda kumuita lipumba kama rais mtarajiwa, na tabia hii masheikh wameiingiza mpaka msikitini! Hii ni hatari kwa taifa letu!
 
Kuwa politician kwa muislam hakumfany awe kafir labda atake mwenyewe kwani mmesahau kwenye uchaguz wa mwaka 2010 maaskofu walisema nini kuhusu uasi wa padri slaa kwa kanisa na kuanza kumtetea hadharani. Go on professor ikulu yako 2015

Lipumba kwenda ikulu kwa kusaidia ujinga? Uuwi Yesu wangu
 
my observation and lesson meant from the video
1. Lipumba yupo kwa ajili ya maslahi ya dini yake na siyo maslahi ya watanzania wote
2. Lipumba ni adui no. 1 wa wakristo kwani hata pale alipoona ameshindwa ilibidi wachakachue matokeo ili mwilislamu mwenzake JK atangazwe mshindi. Ina maana JK hakushinda uchaguzi.
3. Lipumba anataka sasa kutumia dai la waslamu kuhusu mahakama ya kadhi, na geographia ya waslamu walio wengi ambao ndo wapo ukanda wa pwani, ili waslamu wamchague this time kwani JK hakuweza kufanya vizuri yale waliyokua wamekubaliana
3. Lipumba anajarinu kutumia matatizo ya waslamu ambayo siyo tofauti na ya wakristo, na kujifanya yeye ndiye mkombozi wa hayo matatizo na hiyo wafanye juhudi wamweke madaraka hata kwa kuchakachua kama walivyofanya kwa JK
4.Lipumba anajaribu kupandisha joto la waslahimu kwa kuwadanganya kuwa eti upande wa wakriso wamejiandaa, bila kutoa ushahidi wamejiandaa vipi
5. Lipumba amedhihirisha yeye yupo kwa ajili ya kutetea imani yake na waislamu zaidi, na kukosa kabsa utaifa
6. Lipumba amedhihirisha bila shaka yeyote kuwa CUF ni chama cha Waislamu na kipo kwa ajili ya maslahi ya waislamu, ndo maana hata kampeni zake huwa zinaishia ukanda wa pwani
7.Lipumba ameendelea kudhihirisha ya kuwa JK ni mdini, na walikua na deal ya udini na yeye
8. Lipumba aliongea kama mwenyekoti wa CUF , na kutangaza sera za CUF
 
Serikali ya ccm ilimkamata LWAKATARE kwa eti alipanga ugaidi,lakini mchana kweupe mr Lipumba amehamasisha waumini pale msikitini Dar wasichague mtu wa dini nyingine.Huyu ni mtaalamu aliyebobea eti kwenye uchumi,polisiccm kama hawaoni huu ni ugaidi basi wasubiri kuona mengi b4 2015.CUF kama huyu ndie mwenyekiti wao basi hiki chama hakina uhalali wa kuwepo kisheria,Lipumba inabidi ahamie SOMALIA au sudan kwa AFRICA NDIZO NCHI ZINAZOONGOZWA kwa mfumo na uelekezi wa imani yake.Wana CUF inabini chama kitoe tamko au ndio mwisho wa ushirika wenu na ccm.Sasa tumeona kwa nini wabunge wa CUF ni mabubu bungeni wanaamini kuwa ipo siku Tanzania inaongozwa kwa misingi ya dini moja tu.Mungu ibariki tanzania na tuepushe na viongozi kama akina LIPUMBA.
cc to ritz,zemaclopolo,zombi na wenzenu wote.
 
Tukisubiri hadi mtu atuembie kuwa sasa nafanya siasa hapa kanisani au msikitini tuntakuwa tumekosa uwezo aliotupa Mungu wa kufikiri. Tunaweza kutambua mambo si kwa kusikia matamshi tu, bali pia kwa kuona vitendo vya watu na kuvipima. Mathalani, ukiona mtu anaingia nyumbani kwako na kuchukua vitu sebuleni, huitaji akutamkie kuwa "nimekuja kuiba". Tusijifanye hatujui wala hatuoni mienendo ya wanasiasa wanaotumia makanisa kujijenga.

so jk akiingia masjid kuswali nae ameenda kunadi uislam au kuabudu?acha u akili za u kitmoto bana
 
Tokea zamani inajulikana ya kwamba mtaji wa CUF ni Waislamu,ukipinga ujue utakuwa na matatizo ya akili.

CHADEMA nao wakatumia Busara na Hekima kumfanya Padre awe katibu mkuu wa Chama,hakutosha wakamsimamisha kuwa mgombea Uraisi kupitia chama chao 2010 kwa vile katiba anamruhusu ili wapate umaarufu wa kisiasa na kweli mtaji wao ulikuwa mzuri sana.

Masheikhe nao sio wendawazimu hawawezi kukubali kuona Ikulu inaongozwa na Padre hivyo wale waislamu ambao ndio mtaji wa CUF wakatumia busara na hekima zao wakampigia kura Kikwete aka Mr.Dhaifu kwasababu kama wangempigia kura Lipumba walidhani Padre angeshinda na kuongoza nchi.

Na maaskofu nao sio wendawazimu wakatumia busara na hekima zao kumuunga mkono mchung kondoo mwenzao ambaye alishawai kuwa katibi mkuu wa baraza la maaskofu Tanzania.

Na hii hali itakuwa mbaya zaidi kama huyu Padre na katibu mkuu mstaafu wa baraza la maaskofu tanzania ataingia Ikulu.Huyu Padre haitaji kupiga kampeni makanisani kama anvyofanya Lipumba,historia yake tu huyu padre na katibi mkuu mstaafu wa baraza la maaskofu Tanzania inampigia kampeni makanisani.

Hivyo basi wale wanaodai Video ya Padre Slaa akifanya kampeni makanisani video yake ni historia yake inatosha sana.

Najua kuna watu watakuja kusema hapa mimi ni CCM,hizo akili ndogo zisizokubali ukweli.
mengine umejitaidi, ila mambo mengi umeyaweka kihisia zaidi! Pia huwezi kumzuia dr. Slaa kugombea urais eti kwa sababu alikuwa padre, hayo yatakuwa mawazo ya kibaguzi! Lipumba all in all, katereza, alipaswa kujiuzulu!
 
Kama umemsikiliza vizuri Lipumba anadai kauli ya Edwin Mtei kuhusu tume ya katiba inahusu wakristo kujipanga.... very poor reasoning ni bora angesema linahusu chadema kwa mbali lakini pia Mtei yuko nje ya jukwaa la kisiasa angalau unaweza kusema ni mawazo yake binafsi tofauti na pale angesema akiwa mwenyekiti wa chadema. Maoni ya Mtei aliyatoa kibinafsi zaidi kama ulimnukuu vema lakini Lipumba anakifungamanisha chama chake na siasa za kupanga njama za kidini kumpa mgombea mwingine. Namheshimu lakini amenivunja sana MOYO.
Kama hukusoma tamko la maaskofu ni bora ukakaa kimya hata watu wa imani yako waliosoma watakucheka. Ni bora kama matamko ya kidini hayatakiwi tuzungumze lakini sio kusingizia kuwa tamko lile lilikuwa na maneno ya kuwapanga wakristo dhidi ya uislamu. Acha maneno ya kuambiwa lipo hapa Jf jisomee utaelewa kilichomo.



Wewe unanirudisha nyuma sana. Ilani ya uchaguzi ya TEC (Baraza la maaskofu) 2010 hii hapa. Isome ukimaliza niambie kama ni uwongo wakristo hamkuambiwa muchague viongozi watakaweza kutimiza malengo ya kanisa na ya wakristo.

Yaani kauli yenu mbiu kwenye uchaguzi wa 2010 mliambiwa ukristo kwanza siasa baadaye.

Acha porojo, jipange kwanza kabla yakuingia kichwa kichwa!
 
Hata hizo pesa zinazotengwa kwa ajili ya huduma za makanisa, makanisa HUHUDUMIA WANANCHI WOTE BILA KUBAGUA. Ni tofauti na Waislam. JK ameamuru minimum entrance qualification kwa kupata Degree kwa Waislam watakao apply MUM iwe principle moja tu. Huoni kama huo ni Ubaguzi?

Kwa hiyo tujadili pamoja na kama jumuiya za kanisa ni lazima tujifunze kuhimiza mahitaji yetu yazingatiwe na wenye maamuzi. Maoni yetu yasikilizwe na kufanyiwa kazi, tunu za kikristo tunazosimamia zionekane katika sera na katika mgawanyo wa bajeti ya serikali.

Kama huduma zinatolewa kwa watanzania wote bila ubaguzi, kwanini TEC wanasema mahitaji yetu yazingatiwe badala ya kusema mahitaji ya watanzania?
Hata kama huoni basi hata masikio huna?!
 
Wacha maneno ya hovyo
hovyo hiyo ni haki yake watu wamesha amka chadema wamefanya udini mara
ngapi au munafanya siri tunajua yote LIPUMBA BAEREZE BAELEWE wamemwaga
mboga na wewe mwaga ugali kama mbaya wacha iwe mbaya.
umesahau ccm walivokunyoa hiyo midevu yako jela......!!???una comment ka pimbi vile
 
mengine umejitaidi, ila mambo mengi umeyaweka kihisia zaidi! Pia huwezi kumzuia dr. Slaa kugombea urais eti kwa sababu alikuwa padre, hayo yatakuwa mawazo ya kibaguzi! Lipumba all in all, katereza, alipaswa kujiuzulu!

Niliyojitahidi ni yale yanayoendana na Itikadi yako na niliyoweka hisia zaidi ni yale yanayopingana na Itikadi yako.

Nani asiyejua kwamba CHADEMA walitumtumia/wanamtumia Padre Slaa ili wapate umaarufu wa kisiasa kwa kutumia historia yake katika kanisa.

Kwani hawa CDM wamekoasa mtu mwingine asiyekuwa na historia ya kidini kama Padre Slaa?Mbona wanataka kutuharibia nchi hawa kwa maslahi yao ya kisiasa kama anavyofanya Prof.Lipumba.
 
Hata Mimi sipendi kabisa tabia ya viongozi wetu aw dini kutumika ktk harambee za kusaka pesa. Watazilipaje? Lakini hata Kikwete ni mkristo? Simamia haki katika kusema kwako.

View attachment 95331

Umenena sahihi sana Mchumia Rungu. Kimsingi, hatukatai watu kuchangia taasisi za kidini. Ila ni lazima kupima kwa makini malengo ya wachangiaji. Si wote wanaofanya hivyo kwa malengo ya kisiasa. Ila wapo ambao wanaonekana wazi katika mbio za kupata madaraka na wanafanya kila wawezalo kutumia taasisi za kidini. Hao ndio tunatakiwa kuwatambua na kuwakataa. Si lazima mtu aseme hadharani kuwa "sasa nafanya harambee kwa nataka kugombea urais". Lakini Mungu katupa binadamu akili za kutambua mambo kutokana na matendo ya watu. Kwa mfano, ukimuona mtu usiyemfahamu anachukua vitu sebuleni kwako, huitaji akutamkie kuwa "ninakuibia" ili ujue kuwa ni mwizi. Ni sawa na hao wanaotumia misikiti na makanisa. Sio wote wanasema moja kwa moja kama Prof. Lipumba alivyofanya. Lakini nia yao ni moja tu: kutumia udini kutimiza malengo yao ya kisiasa.
Picha uliyoweka inaonesha mfano mzuri kabisa. Katika hili kiongozi hatumii udini bali anatekeleza wajibu wake katika kuchangia jamii. Sina shaka na hili.
Nimefurahia sana sentensi yako kuwa "simamia haki katika kusema...". Na hili ni muhimu sana katika kubaini mienendo sahihi na potofu. Tusiwazuie watu kufanya harambee, lakini pia tusiruhusu udini utumike kwa kisingizio cha harambee.
Tupo pamoja.
 
Walaani chokochoko za udini unaonezwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Chama cha wananchi CUF kimepinga na kulaani kile kilichoandikwa na Gazeti kukishutumu chama/mwenyekiti wake kuwa kaongea habari za siasa katika nyumba ya ibada na ilitafsiriwa kuwa ni kueneza siasa za kidini katika nyumba za ibada.

Chama hicho kimesema hakihusiki kama chama kwa upotoshaji huo na kama Lipumba alienda mskitini ni kama mwumini mwingine hakuwa pale kama chama hivyo chama kisihusishwe na kauli yoyote ya kuwagawa Watanzania kwa misingi ya Udini.

Source: Gazeti la Majira

acheni kutumia akili ndogo,
ni kweli alikwenda msikitini kama muislamu, ila aliongea kama mwanasiasa tena ametambulishwa kama mwenyekiti wa cuf na
rais mtarajiwa
tafuteni kingine cha kujitetea ila Mungu atawaumbua wote kabla ya 2015 bila kujali vyama vyao.

mwanzo niliunga mkono madai ya Mtwara lakini sasa ninasitasita baada ya kumsikia Lipumba kumbe ile sio swala la maslahi ya mtwara bali kuna kadini kameingia humo, too sad.


Sasa ninaelewa kwa nini viongozi hawutumii ushauri wa wataalam aina ya Lipumba simply because hana mapenzi ya kweli na nchi yake ila anazuga kwa manufaa ya dini yake.
 
Katiak hali ya kawaida sitegemei mkristo mkereketwa aseme kwamba TEC ilikosea, lakini ukweli ni kwamba TEC ilikuwa ina walead wakristo. Take it or leave it lakini truth has to be exposed.

Ili Tanzania irudi katika umoja na mshikamano, wote tunatakiwa kuhubiri kwa staili moja. Ukisema upendo, uwe na maana moja iwe kwa muislam au mkristo na wala sio kutoa tafsiri mbili kwenye neno moja.

Mtei alipotamka kwamba tume ya katiba ina waislamu wengi, aliongozwa na ukristo wake na wala sio utanzania. Wote wakati ule ilibidi kusimama na kusema, hapana mzee hapa umekosea.

Mnaponyamaza kimya halafu watu watawa expose.

Hivi kumbe wewe uko kwenye kutetea? Pole sana maana mimi sitetei mtu wala taasisi bali naangali facts with objective mind. Nilisoma nyaraka zile nikazirudia kwa lugha zote-Kiswahili na Kiingereza sikuweza kuona ni wapi alitamkwa Dr.Slaa bali nilichokiona ni Catholick acedmicians wanawafundisha Watanzania kupitia waraka wao namna ya kuchagua viongozi waadilifu na watakaowaongoza sio kuwatawala kufikia Tanzania yenye matumaini-sio yenye chuki maana vipaumbele vya maendeleo bila mshikamano na maelewano na Watanzania wa madhehebu na dini nyingine hata hivyo viapumbele kama vitakuwepo ni kazi bure.

Kuhusu Mtei naona umeenda nje ya mada maana Mzee Mtei na Lipumba are two characters diametrically opposed. Mzee Mtei hakuongelea maswala kinzani ndani ya Kanisa au kwenye mimbari ya Kanisa. Na Professor alipokosea ni kauli tata ndani ya ya nyumba ya ibada ingawa bado nashikiria msimamo wangu kuwa aliyoongea ni ya kwake labda taasisi inayowakilisha Waislamu wote isem huo ndio msimamo wa Waislamu na alitumwa kusema hayo. Kama ilivyo kwa Lipumba ndivyo kwa MTEI alitoa maoni yake tena si kwanza kwa nyakati tofauti huwa anatoa maoni yake mengine ya kupotosha mengine ya kweli lakini hatuwezi kusema katumwa na Kanisa au CDM
 
Wakati mwingine si mbaya kwake kuongea msikitini ila anaonyesha wazi kuwa anachofanya ni cha kidini.

Mfano:
1. Bwana Mkubwa ameshidwa kusaidia
2. Waislamu tumekuwa Daraja la Nne
3. Mwaka 2010 hali ilikuwa mbaya sana na Masheikh mnajua
4. Uchagunzi haukuwa wa haki ila nilifanya vile ili kuokoa jahazi
5. Raslimali zote ziko ukanda wa Waislamu na wanajipanga kuchukuwa
6. nk
Haya maneno si ya kidini bali ni ya kinafiki ambayo yanafanya awe mtu anayeeneza siasa za kidini.

Me naona aangalie na kupima kauli zake kama kiongozi wa jamii yote aliyewahi kusema anataka kukutanisha maaskofu na Masheikh.

Kwa kauli hizi nini ilikuwa nia yake kama alikuwa anajua anachofanya nje ya anachosema?


Huo unafiki mliorithi toka kwa waarabu ndio umesababisha somalia kuwa magofu ,iraq ,syria, afghanistan etc ,hakuna kitu kibaya kama unafiki
 
Back
Top Bottom