Gazet la Mwananchi: 'Pinda azima uasi'

Gazet la Mwananchi: 'Pinda azima uasi'

JUST

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2010
Posts
552
Reaction score
236
Ndugu Wana JF,

Ni matumaini yangu nyote mu wazima wa afya. Kichwa cha Habari hapo juu ni maandishi makubwa meusi yaliyoandikwa kwenye kurasa ya mbele ya gazeti la mwananchi la leo tarehe 30/01/2013. Jambo la kushangaza katika andiko hilo, ni matumizi ya neno UASI. Kwa sababu hiyo ningependa wanaJf tujadiliane yafuatayo:

1) UASI NI NINI?
2) JE WANAMTWARA WALIFANYA UASI?
3) JE WANAMTWARA WADI VIPI HAKI YAO ILI WASIWE WAASI?

Nadhani gazeti la mwananchi halikudhamiria kuuza habari bali kuridhisha tabaka fulani la watu.
 
Hili gazeti linapaswa kupingwa na wana kusini wote, walipige marufuku kuuzwa huko ili wajitambue.....
 
Hili gazeti linapaswa kupingwa na wana kusini wote, walipige marufuku kuuzwa huko ili wajitambue.....

kwa mtazamo wangu nadhani gazeti la mwananchi ndio waasi maana wameacha kufuata maadili ya uandishi wa habari. yaliyotokea mtwara ilikua ni vurugu na si uasi. nijuanyo mimi uasi ni hali ya kuachana au kukataa na fungamano fulani na kuanzisha fungamano lingine ili kupinga fungamano la awali, kitu ambacho mtwara hakipo.
 
Huo ndio ukweli kama hamuamini subiria kuona gesi ikija Dar
 
Wamebakiza miaka miwili ya kuandika vichwa vyote vya habari wanavyovipenda. Hii nchi imefika hapa tulipo sababu ya propaganda chafu, na bado hazikomi. Kama ni makosa ya muandishi ama ni maelekezo ya serikali/chama basi hicho kichwa cha habari hakijengi, tunapalilia chuki na kuona kumbe tukijieleza matakwa yetu ni UASI.
 
Gazeti la kweli ni TANZANIA DAIMA pekee kwakuwa linaitumikia chadema maana maadili ya uandishi wa habari ni kuandika habari za kuisifia cdm na kuiponda serikali iwe kwa habari za kweli au uwongo.haa haaa
 
Huo ndio ukweli kama hamuamini subiria kuona gesi ikija Dar

nafikiri hujaelewa mantiki ya mada yangu ambayo haihusiani na gesi kwenda Dar bali lugha iliyotumika na gazeti husika. Kwani wangesema Pinda azima Vurugu wasingeeleweka?
 
Gazeti la kweli ni TANZANIA DAIMA pekee kwakuwa linaitumikia chadema maana maadili ya uandishi wa habari ni kuandika habari za kuisifia cdm na kuiponda serikali iwe kwa habari za kweli au uwongo.haa haaa

Hoja hapa ni matumizi ya neno UASI badala ya neneo Vurugu. Mfano watu wakilalamika na kudai haki ya uchaguzi huru kwa kukoseshwa uongozi ndani ya chama kwa sababu ya rushwa nao watakuwa ni WAASI?
 
Nimepata kusoma mahala fulani et ni la CHAMA
 
Hapa wanataka kuamisha umma kuwa wananchi wanaodai haki zao ni waasi , na dawa ya waasi ni moja ni dhambi ya kufungwa kifungo cha maisha , hawa jamaa tayari wameshasema mtwara kulikuwa na waasi hivyo washitakiwe kwa sheria ya uasi .

Gazeti limepotoka moja kwa moja hili.....
 
Nimepata kusoma mahala fulani et ni la CHAMA

ningependa kukuelewa zaidi maana umeniacha kwenye hisia, lakini CHAMA ndio wanayoruhusa ya kutumia maneno makali namna hiyo? huoni tutafikia mahala watu watandikwa kuwa ni wahaini?
 
Katika hali inayoonekana ni ya kushangaza ni vyombo vya habari kuendelea kuiripoti ziara ya pinda ya kuja mtwara eti kwamba amefanikiwa kuumaliza mzozo wa gesi na kutuliza taharuki kwa wananchi kwa ujumla wake,

hivi ni vitu vya ajabu sana,tujiulize pinda katika ujio wake kaongea na wananchi au kaongea na wawakilishi?,na je ana uhakika gani ya kwamba hao wawakilishi wakija kwa wananchi kuleta mrejesho watapata kueleweka na kuaminika?,

Pinda katika mazungumzo yake kajaribu kuelezea ya kwamba taarifa ambayo wananchi walipewa haikuwa sahihi na
kwamba mchakato wa kusafirishwa kwa gesi sharti kiwanda cha kuchakatwa gesi kijengwe mtwara katika
kijiji cha madiba, ili mabaki yatokanayo na ujenzi huo yazid kuvutia viwanda mbali mbali kutoka kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, sawa,hii si mara ya kwanza kwa serikali hii kutoa ahadi kama hizo,imetoa ahadi kama hizo kilwa,lakini hadi leo hii hakuna chochote kilichofanyika huku gesi hiyo ikiendelea kusafirishwa,

Ieleweke wazi ya kwamba gesi hii n nyingi na wanamtwara na kusini kwa ujumla msimamo wao ni kuhakikisha gesi hii inanufaisha watanzania wote na si Dar es salaam pekee,

Ruvuma hawana umeme wa kutosha,hawapo katika grid ya taifa,tabora,kigoma n.k huko kote hawana umeme wa uhakika na hawapo katika grid ya taifa,lini sisi mtwara na hao wenzetu tutaingizwa kwenye plan kuu ya grid ya taifa kwa kutumia rasilimali gesi hii,pinda kashindwa kutolea ufafanuzi hilo.

Ni kukosa hekima kwa pinda na wengine kusema ya kwamba amefanikiwa kutuliza vurugu za kusini,kwani kusini tuna vurugu zisizo na mashiko?kabla ya pinda kuja huku watu walikuwa tayari na utulivu huku wakiendelea na shughuli zao za kila siku,pinda kaja na yake tuh,na wananchi hakuna chochote walichoipata kwa ujio wa pinda,

Pinda kasema ya kwamba..

1.kiwanda cha kuchakata gesi kitajengwa kijiji cha madiba na kwamba gesi hiyo haitasafirishwa hadi kujengwa kwa kiwanda hiko,swali kwake ni kwamba plan ya kujenga hiko kiwanda iliwepo au haikuwepo?na kama ilikuwapo kwanin haikusemwa,walikuwa walificha nini?,kiwanda kitajengwa ili kisafirishe gesi hiyo,,sasa cha kujiuliza plan ya gesi ni ndan ya miez 18,sasa je hicho kiwanda kinachosemwa kitajengwa ndan ya hiyo miez 18 pia au imekaaje kaaje?

2.plan ya ujenz wa bomba ipo au haipo?kama ipo watanzania hawapingi plan ya ujenz huo tuh.,la hasha,wanataka kujua mkataba huo ukoje?mbona uko kisiri?bunge halijui chochote kuhusu mkataba huo,je hauna ufisadi?una maslahi ya nchi au kwa watu binafsi?
Sio mara moja ama mara mbili kuona nchi hii ikiingia kwenye mikataba mibovu inayopelekea watu kuish maisha ya udhalili.
Pia,plan ya bomba kama ipo,mbona hajajibu ipi ni bora kati aya kusafirisha umeme na kusafirisha gesi kwa maslahi ya nchi hii?

Ndugu zangu tusiwe ni watu wa kukubali kupokea majibu mepesi mepesi kwa hoja zinazostahili majibu ya uhakika kama yahusuyo gesi yetu,pinda alichokifanya ni kuja kuitetea serikali na boss wake,na SI kuja kusimama kwa masilahi ya wananchi,hilo lieleweke wazi.
Hakuna wa kutengua ile kauli ya jk kwamba gesi lazima itoke kwa namna yoyote ile zaid ya mwenyewe jk,hawa wote kina pinda ni wachumia tumbo tuh,,

tunawatadharisha hao wawakilishi waliokwenda kuongea na pinda kwamba wao hawawez kutusemea sisi,,na kama wanataka kutusemea sisi basi watusemee mambo yenye mantiki na sio blah blah kama hizo na pinda wao,tbc siku zote ilikuwa haitaki kuliport habari hii leo inapokuja kusema ya kwamba pinda kafanikiwa kutuliza mgogoro wa kusini,mgogoro upi?

Wao wameanza lin kuutangaza mgogoro huu?ni unafiki tuh,tena wa hali ya juu..
Sasa hao wawakilishi wa asasi mbali mbli,wanaharakati na viongoz wa dini wawe makini kwa hilo,sisi hatuendeshwi kwa hulka za kishabiki,bali tunaendeshwa kwa hoja za maana na fact za kueleweka,tunawasubiri waje watupe mrejesho,kama wamesaliti tutaanza na wao kwanza.

Kwa ufupi,hatuna imani na pinda kwa ahadi zake,na hakuna alichokiongea tuh,na yeye hajaongea na wananchi,kaongea na hao wawakilishi ambao wanaweza wakasimamia ukweli ama upotofu.

Na kwa kuwa speaker wa bunge mama makinda kaahidi kuteua tume ya bunge ili ije kutusikiliza na kwenda kupeleka hoja hii bungeni,sisi tunatamka rasmi ya kwamba tuna imani na hiyo kamati inayokuja na si huu ujio wa pinda,pinda kazid tuh kupinda pinda na kujipindua pindua,aende zake na hatuna imani nae,,

hili suala haliwezi kuisha kirahis rahisi kama wanavodhania,sisi tunahoja za maana,wao wanazikwepesha na kuleta ahad ambazo siku zote wamekuwa si wenye kuzitekeleza..

Tegemeeni kuskia mengi sana kutoka huku,the game is not over..!

Gesi kwanza uhai baadae...
 
Gazeti la kweli ni TANZANIA DAIMA pekee kwakuwa linaitumikia chadema maana maadili ya uandishi wa habari ni kuandika habari za kuisifia cdm na kuiponda serikali iwe kwa habari za kweli au uwongo.haa haaa

Kwa mfano issue gani? Hata mtumie mabango yote nchini,hamponi.
 
ndugu wanaJF yeyote mwenye maana kamili ya neno UASI atusaidie wote kwa manufaa ya ufahamu, mwenye kamusi atusaidie haraka ili mada iwe nzuri
 
UASI-TENDO LA UVUNJAJI WA KANUNI,SHERIA AU AMRI,UHALIFU-Cheki kamusi ya Kiswahili sanifu toleo la pili(Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili Dar es salaam)
ndugu wanaJF yeyote mwenye maana kamili ya neno UASI atusaidie wote kwa manufaa ya ufahamu, mwenye kamusi atusaidie haraka ili mada iwe nzuri
 
Kuna mhariti/ wahariri wa gazeti hili wanajifanya ni wasemaji wa wizara ya nishati na madini , hili lilitokea tulipoalikwa dinner ....
 
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amefanikiwa kutuliza jazba za wakazi wa Mkoa wa Mtwara baada ya kueleza jinsi watakavyonufaika na gesi itakayozalishwa mkoani humo kabla ya kusafirishwa kwa bomba hadi Dar es Salaam.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Joseph Simbakalia amewaomba radhi wananchi wa mkoa huo kutokana na kauli Desemba 21, mwaka jana akiwakebehi baada ya kumwomba apokee maandamano yao ya kupinga mpango wa kusafirisha gesi hiyo.

Akizungumza katika mkutano wa majumuisho uliofanyika jana baada ya kusikiliza madai ya wananchi hao kwa siku mbili mfululizo, Pinda alisema hakuna tone la gesi ghafi itakayosafirisha kwa njia ya bomba na kusema kiwanda cha kusindika gesi ghafi kitajengwa katika Kijiji cha Madimba, mkoani humo ili mabaki yatokanayo na gesi hiyo yatumike kuvutia uwekezaji wa viwanda.

“Wataalamu wanasema gesi haiwezi kwa namna yoyote ile kusafirishwa kama ilivyo, lazima ibadilishwe kuwa hewa au barafu… kiwanda cha kusafisha gesi kitajengwa Madimba. Gesi yote itakayotoka Mnazi Bay itasafishwa hapo na masalia yote yatabaki huku ili kuvutia viwanda vya mbolea na vingine vinavyotumia malighafi hizo,” alisema Pinda na kuongeza:

“Kama tungekuwa tunasafirisha gesi ghafi basi hata kiwanda cha Dangote kisingejengwa hapa… gesi itakayopelekwa Dar es Salaam ni ile iliyosafishwa kwa ajili ya matumizi ya kuzalisha umeme… tusaidieni wenzetu kuliokoa Taifa na tatizo la umeme.”

“Gesi lazima isindikwe Mtwara, haitoki hadi viwanda vije… nadhani hili ni jambo jema lazima tuliwekee utaratibu. Nikawauliza wataalamu wangu kwani kiwanda cha kusafisha gesi kinajengwa wapi, wakanijibu Madimba… nikasema kumbe tatizo kubwa ni kutowaeleza vya kutosha wananchi suala la gesi.” alisema Waziri Mkuu huku akipigiwa makofi... “Nafikiri tatizo ni sisi Serikali hatukuwa na mpango mzuri wa kuwaelimisha wananchi.”

Awali, madai ya wakazi wa Mkoa wa Mtwara yalikuwa ku pinga usafirishaji wa gesi ghafi kwenda Dar es Salaam wakieleza kuwa mpango huo utafukuza uwekezaji wa viwanda mkoani humo ambao ungechochewa na upatikanaji wa malighafi baada ya kusafishwa kwa gesi.

Pia wananchi walipinga uje nzi wa mitambo ya kuzalisha umeme Kinyerezi, Dar es Salaam wakiitaka Serikali kujenga mitambo hiyo mkoani Mtwara.

Alitoa wito kwa wabunge wa Mkoa wa Mtwara kufuta tofauti zao za kisiasa ili waweze kuharakisha maendeleo ya mkoa huo... “Purukushani hizi ndani ya chama hazina tija, tuseme basi… wabunge hawaelewani, sasa bungeni wanakwendaje... kila mtu na lake … hebu tuseme watu kwanza mimi badaaye,” alisema Pinda huku akishangiliwa.

Katika siku hizo mbili mkoani Mtwara, Waziri Mkuu alikutana na viongozi wa vyama vya siasa, dini, wafanyabiashara, madiwani na wenyeviti wa mitaa na wanaharakati mbalimbali.
RC aomba radhi
Katika hatua nyingine, Mkuu wa Mkoa, Simbakalia aliwaomba radhi wakazi wa Mkoa wa Mtwara akisema alipotoka kuwaita wananchi hao wapuuzi na baadaye wahaini kauli ambazo ziliwaudhi wengi

“Kupitia hadhara hii nawaomba radhi kwa kuwakwaza, nimesikitishwa kwa kauli yangu ambayo imepokewa kwa hisia kwamba niliwadharau,” alisema Simbakalia.

Baadaye Waziri Mkuu aliwasihi wananchi wa Mtwara kumsamehe Mkuu wao wa Mkoa wa Mtwara kwa kauli hiyo aliyoitoa 21 Desemba, mwaka jana katika kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa, (RCC), pale alipoombwa kuyapokea maandamano ya wakazi wa mkoa huo Desemba, 27, mwaka jana.
 
Back
Top Bottom