Gawio la shs. kwa hisa CRDB

Leo nimepewa taarifa kuwa katika kikao cha Wanahisa kilichokaa mjini Arusha imeamuliwa kuwa gawio la kila hisa iwe shs. 10. Haingii akilini kwangu kutokana na faida ya Tshs.75bn iliyopatikana gawio inakuwa shs.10 kwa hisa moja. Ninatarajia kuuza hisa zangu zipatapazo 3500 ili nichukue ustaarabu mwingine. Ina maana katika hisa zangu 3500 gawio langu ni shs.35,000 bado kodi. Kwangu naona kama tusi. Hata akaunti yangu nitahamisha kutoka CRDB.
Mkuu siku ya kwenda kuchukua hiyo hundi yako nenda na kadi yako ya ATM kabisa maana wakikukata na kodi ya zuio (withholding tax) balance haikutoshi nauli na lunch ya siku hiyo. Hamna jinsi utaingia ATM tu. Labda ujiongeze uwe na hisa angalau 500,000
 
Duuh Mkuu.. Afadhali hata ungefungua fixed deposit ac lol.. Ndo maana hisa za Vodacom, wananchi wengi walikuwa very reluctant kuzinunua..
Nani alikwambia Fixed diposit wanachukua sh.800,000? Na Utapata Faida Kubwa?

Rate ni Hizi hapa tena Mnajidiliana inaweza Kuwa Chini
CRDB Bank 1 Year Fixed Deposit 7.50%
CRDB Bank 6 Month Fixed
Deposit 5.50%
CRDB Bank 3 Month Fixed
Deposit 4.50%
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Samahani wakuu, hivi kodi inayokatwa kutokana na faida ya kuuza hisa au gawio ni asilimia ngapi?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Aliyekwambia hisa ni asset nani? huna elimu juu ya umiliki wa hisa, huwezi kununua hisa ili kupata gawio, hisa ni kama bidhaa unaangalia asubuhi wapi inapatikana kwa bei ya chini, unanunua mchana ikipanda unauza unahesabu balance iliyobaki, unatafuta bar yenye warembo wazuri unatulia kusubiri siku nyingine. Hiyo ndi biashara ya hisa.
Mkuu bhana, umeniacha nacheeeeeeka
 
Faida ya hisa siyo kwenye gawio. Ni "kuspeculate the best time to sell your shares". Faida iko kwenye mauzo. Unanunua kwa bei ndogo na unauza wakati share price imepanda.
Well said mkuu, na hyo ndo maana ya faida ya hisa
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kweli watu hamfikirii na inawezekana hamtumii akili zenu vizuri share moja thaman ya 185 tshs alafu unataka ulipwe faida ya 1000 per share kama gawio lazima utakua chizi Investment imevamiwa
 
Leo nimepewa taarifa kuwa katika kikao cha Wanahisa kilichokaa mjini Arusha imeamuliwa kuwa gawio la kila hisa iwe shs. 10. Haingii akilini kwangu kutokana na faida ya Tshs.75bn iliyopatikana gawio inakuwa shs.10 kwa hisa moja. Ninatarajia kuuza hisa zangu zipatapazo 3500 ili nichukue ustaarabu mwingine. Ina maana katika hisa zangu 3500 gawio langu ni shs.35,000 bado kodi. Kwangu naona kama tusi. Hata akaunti yangu nitahamisha kutoka CRDB.
vihisa vyenyewe vichache unatokwa na povu
 
Nani alikwambia Fixed diposit wanachukua sh.800,000? Na Utapata Faida Kubwa?

Rate ni Hizi hapa tena Mnajidiliana inaweza Kuwa Chini
CRDB Bank 1 Year Fixed Deposit 7.50%
CRDB Bank 6 Month Fixed
Deposit 5.50%
CRDB Bank 3 Month Fixed
Deposit 4.50%
CRDB wametikisika kweli miaka hii miwili, maamuzi ya kutoweka hela za serikali huko yamewagusa sana.
Banc ABC wanatoa fixed deposit 13% hadi 16% sasa hivi kutegemea una kiasi gani.
 
Wakati serikali inazivuruga benki tulikuwa tunachekelea,sasa ni msimu wa mavuno

" when they came for the Jews,I kept silent because I was not a Jew......"

Dunia sio mbaya kwa sababu kuna watu wabaya,bali kwa sababu watu wema wanakaa kimya wakati ubaya unafanyika........."
Word!
 
Leo nimepewa taarifa kuwa katika kikao cha Wanahisa kilichokaa mjini Arusha imeamuliwa kuwa gawio la kila hisa iwe shs. 10. Haingii akilini kwangu kutokana na faida ya Tshs.75bn iliyopatikana gawio inakuwa shs.10 kwa hisa moja. Ninatarajia kuuza hisa zangu zipatapazo 3500 ili nichukue ustaarabu mwingine. Ina maana katika hisa zangu 3500 gawio langu ni shs.35,000 bado kodi. Kwangu naona kama tusi. Hata akaunti yangu nitahamisha kutoka CRDB.
Biashara ya hisa ni ngumu sana inahitaji uvumilivu sana, some time wataki faidi sana ni watoto wako, weww unaweza usiwe Duniani kipindi sasa faida kubwa inaonekana.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Mkuu uwekezaji mzuri ni kununua viwanja vilivyopimwa, kwa sababu ardhi inaongezeka thamani kila siku, mimi nilikuwa na viwanja vinne hapa dar ambavyo nilivinunua miaka miwili iliyopita kwa milioni nane nimeviuza majuzi kwa milioni 40
Hivyo viwanja havina fofauti na kununua hisa, Hivi unanunua kiwanja Milioni 3 unakuja kukiuuza milioni 50 baada ya miaka 20 unaona umefaidika sana?
Huwa hatupigi calculationa ndo tatizo, no time value of money.
 
Mkuu siku ya kwenda kuchukua hiyo hundi yako nenda na kadi yako ya ATM kabisa maana wakikukata na kodi ya zuio (withholding tax) balance haikutoshi nauli na lunch ya siku hiyo. Hamna jinsi utaingia ATM tu. Labda ujiongeze uwe na hisa angalau 500,000
Kwani kwenye gawio la Withholding tax.
 
CRDB wametikisika kweli miaka hii miwili, maamuzi ya kutoweka hela za serikali huko yamewagusa sana.
Banc ABC wanatoa fixed deposit 13% hadi 16% sasa hivi kutegemea una kiasi gani.
Izo bank zinaongopa kwa wateja wao. Bank inayotoa hisa kubwa ni exim bank na wenyewe 8%.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Hisa watalaam hawasubiri gawio......wataalam wanacheza mchezo wa kununua na kuuza ....unanunua 100 kwa hisa unauza shs 500 kwa hisa.... mtu anaweza kununua hisa asubuhi jioni hali ikibadilika anauza kama kuna faida.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Back
Top Bottom