Gavana wa BoT dhidi ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, cheo kipi ni kikubwa?

ni dhambi kubwa sana kuchochea mambo baya la kufarakanisha watu

Tutuba si Msukuma, ni Muha lakin hata kama angekuwa Msukuma si dhambi

Wasukuma wana hali kama waliyo mayo Wagogo acheni roho na tabia za kibaguzi
Kwahyo
 
Ukitaka kujua angalia tu ukubwa wa mjengo kaangalie bank kuu ile migorofa na mpaka chini ya ardhi kule kuna mbonge wa korido kuelekea gogoni katibu mkuu hawezi kumzidi governor kwa majukumu na unyeti. Pili angalia ulinzi wa gavana mzee baba.
 
Gavana wa benki kuu ni nafasi nyeti kwa Taifa.
 
Unamfananisha CDF na nini wewe..?😳🤠🤠
Kwenye utumishi katibu mkuu siku zote ni mkubwa, japo kiutendaji mkuu wa taasisi anaweza kuwa na majukumu nyeti na muhimu zaidi.

1. Mfano Katibu Mkuu wizara ya fedha (ambaye pia ni paymaster general) vs. Governor wa BoT

2. Katibu mkuu wizara ya ulinzi na JKT vs. CDF

3. Katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani vs. IGP

N.K

Katibu mkuu ni mkubwa kwa mkuu wa taasisi yoyote. Na kuna mambo lazima yeye aidhinishe 😃. Heshima lazima iwepo.

BTW, zote ni nafasi za kumsaidia Mheshimiwa Rais, kwahiyo yeye ndiye anapanga nani anafaa wapi
 
ni dhambi kubwa sana kuchochea mambo baya la kufarakanisha watu

Tutuba si Msukuma, ni Muha lakin hata kama angekuwa Msukuma si dhambi

Wasukuma wana hali kama waliyo mayo Wagogo acheni roho na tabia za kibaguzi

..kweli zama zimebadilika.

..2016 to 2021 watu walikuwa wanakanyagana na hata kulilia kuwa Wasukuma, wakati sio.

..ilikuwa fahari kuitwa Sukuma gang.

..JPM alikuwa mbaguzi na aliwatumia vibaya ndugu zetu Wasukuma.
 
BOT ipo chini ya wizara ya fedha
Hivyo kimamlaka katibu mkuu ni mkubwa kuliko Gavana
Ila Gavana anamuacha mbali kimshahara na marupurupu katibu mkuu

Ni kama vile ilivyo kwa mkurugenzi wa TPDC anavyokunja mpunga mrefu kuliko katibu mkuu nishati
 
Permanent Secretary wa Wizara na Gavana wa Benki Kuu ,cheo kipi Ni Kikubwa?
Kila nikiandika nafuta.
Nakupa mfano mdogo tu jibu utalipata mwenyewe.
Mkuu wa majeshi (CDF) anajulikana na kupewa heshima kubwa sana jeshini na pia yupo karibu sana na raisi wa nchi.
Lakini anapokutana na Katibu Mkuu wizara ya ulinzi kiitifaki yeye ndio anatakiwa kumpa heshima Katibu wa wizara (kumsalute) kwa sababu jeshi analoliongoza lipo chini ya wizara ya ulinzi, na katibu mkuu ndio mtendaji mkuu wa shughuli zote za wizara hiyo.
 
Back
Top Bottom