Gavana wa BoT dhidi ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, cheo kipi ni kikubwa?

Kila nikiandika nafuta.
Nakupa mfano mdogo tu jibu utalipata mwenyewe.
Mkuu wa majeshi (CDF) anajulikana na kupewa heshima kubwa sana jeshini na pia yupo karibu sana na raisi wa nchi.
Lakini anapokutana na Katibu Mkuu wizara ya ulinzi kiitifaki yeye ndio anatakiwa kumpa heshima Katibu wa wizara (kumsalute) kwa sababu jeshi analoliongoza lipo chini ya wizara ya ulinzi, na katibu mkuu ndio mtendaji mkuu wa shughuli zote za wizara hiyo.
Yaani BOT ipo chini ya Wizara ya Fedha. Automatically Gavana ni mdogo kwa Katibu wa Wizara.
Maana miongozo yote inatokea Wizarani na mtendaji mkuu wa wizara ni Katibu.
 
Kuna ukubwa na unyeti.

Kiutawala, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha ni mkubwa kwa Gavana. Ila Gavana ana nafasi nyeti zaidi kuliko Katibu wa Wizara..

Swala lingine ni security ya kibarua. Ugavana una muda unaopaswa kutimilika na hupaswi kutumbuliwa kwa Mkuu wako kujisikia tu.

Maelekezo,
Katibu Mkuu anapokea maelekezo ya moja kwa moja kutoka kwa Rais na Waziri wake. Wakati Gavana huitwa kumshauri Mh Rais juu ya namna gani ya kufanya ili kutatua jambo mahususi kwa uchumi wa nchi.
 
ni dhambi kubwa sana kuchochea mambo baya la kufarakanisha watu

Tutuba si Msukuma, ni Muha lakin hata kama angekuwa Msukuma si dhambi

Wasukuma wana hali kama waliyo mayo Wagogo acheni roho na tabia za kibaguzi
Waha awamu hii ya mama wana manafasi makubwa makubwa labda washindwe wenyewe kuusaidia Mkoa wao.
 
hata DC anaongea direct na Rais japo juu yake kiutawala wapo RC, Waziri wa Tamisemi na PM

Nyerere alijua sana kuisuka hii Nchi wallah
Kwa mtazamo wangu.
Bot ni taasisi inayojitegemea ndani ya wizara.
 
Back
Top Bottom