Gavana Ndullu aliingia ofisini mwaka 2008 akichukua nafasi ya Balali wakati huo Us$1 ilikuwa sawa na tshs 1100/= leo hii us$ 1 ni sawa na tshs 2182/= na haonyeshi kuwa anazo mbinu mpya za kusimamia soko letu la fedha. Wakati akikabidhiwa ofisi ya umma riba za mabenki zikiwa 8% hadi 12% leo hii riba za mabenki ziko 25% hadi54% na haoni haja ya kuingilia kati yeye kwake sawa tu. Hapana hatuwezi kwenda kwa mtindo huo.
Leo anaambiwa ahakiki invoice aone kama ziko sawa anaonekana kusitasita, inamaana anajua madudu yapo ila hataki kuwa mhanga wa hayo madudu kama alivyo hepa yale madudu ya escrow.
Ukweli uchumi wetu hauwezi kuimarika kama tunae Gavana asiyekuwa na weledi wa kusimamia hazina yetu. Gavana ambaye hajui idadi ya wafanyakazi wake anawezaje kujua usalama wa hazina yetu? Mbele ya media wenzie walikiri wapo watumishi kanyaboya halafu yeye anasema tumwambie ni nani kweli?