MWITONGO MAARIFA
JF-Expert Member
- Aug 11, 2018
- 276
- 1,428
Ipo clip inasambaa ikionyesha Gavana wa BOT akiondoka mbele ya waandishi wa habari kabla ajaulizwa maswali, lakini pia waandishi wanasikika wakimwomba asubiri maswali anaendelea kuondoka huku wasaidizi wake au watu alioambatana nao wakicheka.
Ikumbukwe pia kuwa huyu ni kiongozi mkubwa nchini na analipwa fedha nyingi na walipakodi hivyo anatakiwa kutoa ufafanuzi kutibu majeraha ya kibiashara na kiuchumi yaliletekezwa na operesheni iliyofanywa na ofisi yake.
Huyu pia Ni msomi na mwalimu mwenye watu wengi nyuma yake ambao aliwajenga kuheshimu na kujijengea mazingira yakujibu hoja, alikuwa anatunga mitihani watu wanajibu, alikuwa anaendesha na kusimamia malumbano ya kitaaluma chuoni yote haya akiyafanya kwa kuzingatia misingi ya taaluma.
Leo yeye anaondoka mbele ya vyombo vya habari ambavyo ameviita yeye tena bila hata kuaga, anatoa tafsiri gani kwa viongoz wengine?Wengi wa waandishi wa habari ni sawa na watoto wake, je yeye angewaita wakaanza kuondoka kabla hajamaliza na bila kumsikiliza angejisikiaje?
Nadhani tunapaswa kuheshimu taaluma za watu lakini pia ukiwa kiongoz simama kama dira kwa wengine.Kesho usishangae akaibuka mtu akafanya Kama gavana na akihojiwa Sana akajitetea mbona Gavana alifanya hamkupiga kelele?