Gaudence Lyimo kugombea udiwani Kimandolu(CCM)

Gerad2008

JF-Expert Member
Jun 9, 2009
583
287
Gaudence lyimo ameteuliwa na CCM kugombea udiwani katika kata ya Kimandolu ambako uchaguzi umepangwa kufanyika January 2018.

Gaudence sijajua kwa nini unadanganyika au umelazimishwa kaka? una nini unachokikosa haswa? una kampuni kubwa ya ujenzi na ukandarasi na kwa ufupi unajitosheleza. Hizi dhambi za siasa mbona unalazimisha kuziokota?

Wewe ni mtu mwema sana ila nafikiri uko addicted kwenye CCM au hujui kusema hapana au unaogopa ukikataa utafanywa ndivyo sivyo;. hii ndiyo assumption yangu.

Huyu bwana anaishi Oloriani na alikuwa diwani wa huko miaka ya 2010 wakati akina Lema walikataa kumtambua kama Meya ingawaje mwishoni mwa 2015 walipatanishwa wakawa friends na Lema na wakafanya kazi pamoja. Tena sasa amerudishwa kugombea udiwani kata ya kimandolu ambayo siyo yake. Kata ngumu sana kwa CCM kupata ushindi.

Naona lyimo amesahau matusi, laana za marehemu Askofu Laizer and now he is back kutusiwa na kupotezewa heshima tena kwenye siasa za udiwani ambazo hazimwongezei chochote zaidi ya kumdhalilisha. Lyimo kama mahaba yako yamerudi baada ya kugundua utashinda hata bila ya kupiga kampeni kwa sababu kuna aliyekubeba mgongoni basi ujue hiyo ni dhambi kubwa unataka kurudi na ni sawa na kula matapishi. Ningekuwa na uwezo ningekushauri achana na huu ujinga uendelee na business zako kwani huko utapata heshima zaidi. watu wako kimya ila wana reservations nyingi ndani ya mioyo yao hivyo huu ukimya usikudanganye kuwa CCM imekubalika Kimandolu au Arusha Mjini bali freedom of expression imeminywa na watu kuamua kubaki na wanachokiamini ndani ya mioyo yao.

Unaweza kushinda udiwani kwa kupewa ila maboss wako wakasema naachia sanduku la kura kuamua bila interference ujue utabaki na aibu ya miaka. Kumbuka Cheap is expensive na dhuluma haijawahi mwacha mtu salama
 
Ukiona hivi ujue ushindi anao la sivyo nimjuavyo huyu bwana asingekubali kwenda kugombea kama hana uhakika na ushindi
 
mtanzania anaruhusiwa kisheria kugombea wapiga kura wakiona inafaa wanampa
 
Back
Top Bottom