Gari yangu vibali vimeisha muda mrefu

Gari yangu vibali vimeisha muda mrefu

mabwiku

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2015
Posts
447
Reaction score
392
Msaada ndugu zangu,

Gari yangu nilikua siitumii muda sasa na mazingira nayofanyia kazi ni kambi so waweza tumia hata miaka kumi bila kulipia maadam usifike town ukakumbana na trafic,road licence pamoja na bima ni karibia 1500000.

Nashindwa kuhimili gharama izo na kuna jamaa alinambia anisaidie kuchakachua nilipe kidogo lkn nasikia ni feki na hazitambuliki kwenye system so naitaji msaada wa mawazo pamoja na ushauri nini nifanye angalau nisilipe gharama kubwa ivyo

Nawakilisha
 
Unataka ushauriwe nini? Wakati we mwenyewe umesema hivyo feki havitambuliki? We baki huko huko kambini usije mjini kujaza hewa ukaa
 
nenda TRA wamtoa tangazo kwmba magari ambayo hayatumiki yakaripotiwe ili yatolewe kwenye system...nenda kalitoe, waambie lilikuwa juu ya mawe
 
Katia road licence ya
pikipiki ubandike.....huwa hawaangili plate number kuhakikisha ni sawa na zile kwenye leseni.
 
Inaonekana mkuu unapenda vya bure sana yaani kulipa 1,500,000/=TZS ndio kunakufanya uanzishe uzi hapa,huku ukijua wazi ni haki yako kulipa kodi za serikali.Hii nchi itaendeleaje ikiwa kila mtu hataki kulipa kodi? Na inawezekana hata mshahara wako unatokana na kodi,ninachokushauri ni uza hilo gari lako kama chuma chakavu kuepuka usumbufu,au ichinje na uuze spare parts.Naona hakuna namna nyingine.Wewe ni poti nini?


msaada ndugu zangu,gari yangu nilikua siitumii muda sasa na mazingira nayofanyia kazi ni kambi so waweza tumia hata miaka kumi bila kulipia maadam usifike twn ukakumbana na trafic,,road licence pamoja na bima ni karibia 1500000,,nashindwa kuhimili gharama izo na kuna jamaa alinambia anisaidie kuchakachua nilipe kidogo lkn nasikia ni feki na hazitambuliki kwenye system,,so naitaji msaada wa mawazo pamoja na ushauri nini nifanye angalau nisilipe gharama kubwa ivyo,nawakilisha,
 
Karipoti TRA kama Viva89 alivyokushauri.
Kwisha mchezo.
 
Last edited by a moderator:
Halafu anakuambia yupo Kambi,sasa huyu ni Mwanajeshi Jambazi.

Kwani uliponunua gari ulinunua kwa kutegemea nini.

Na sio kwamba ulikuwa hulitumii,ila unatafuta namna ya kuambiwa watu wanaibaje.

Huu uvivu wa akili kufikiria ni janga kweli aisee.
We chukua feki halafu ndio utajua jiji la Dar watu wanavyopiga hela.
Kuna mtu aliwekewa vibali feki yule yule aliemuwekea ndio huyo huyo aliweka mchongo wa jamaa kukamatwa ikatomka hela kibao na jamaa akapata commission yake.

Mjini hapo
 
Kuwa na gari ni k2 kimoja na kulimiliki ni kitu kingine. Wengi hawafikilii sana gharama ya uendeshaji wa magari radha than only acquisition cost. Kabla ya kumiliki hivi vitu yatubidi tuangalie hayo. Tanzania tunayoitaka ni ile ya watu kuwa na uchungu wa kuchangia maendeleo yake na sio wajanja wajanja wanaofikilia kuihujumu. Ushauri uza gari kama screpa uondokane na mawazo ya kuchakachua TRA.
 
Back
Top Bottom