Gari la Mpendazoe lakamatwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gari la Mpendazoe lakamatwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jun 3, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Msemaji wa Chama Cha Jamii (CCJ), Fred Mpendazoe.  Polisi katika kituo cha Karume jijini Dar es Salaam, imelikamata na kulishikilia kwa muda, msemaji wa Chama Cha Jamii (CCJ), Fred Mpendazoe.
  Gari hilo lenye namba T 776 BAE, aina ya Corolla, lilishikiliwa jana kwa takribani saa sita, kwa madai kuwa kibali cha kuendesha kilikuwa kimeisha.
  Wakati gari hilo likikamatwa, lilikuwa linaendeshwa na dereva wake, Vitalis Henzi Mpendazoe, anayesadikiwa kuwa mtoto wa Mpendazoe.
  Akizungumza na gazeti hili jana nje ya kituo hicho, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, alisema mtoto huyo alikamatwa eneo la Msimbazi Centre, wakati akitokea Kigogo kuelekea Ilala-Boma.
  Alisema askari wawili waliokuwa kwenye pikipiki, walilitilia shaka na kuanza kulikagua, ambapo ilibainika bima yake ilikuwa imemalizika muda wa matumizi.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Si habari ya kushangaza, mtu yoyote akihama CCM huwa anafuatiliwa na kuwa-harrased. Tunajua yaliyomkuta Mrema, Kolimba etc lakini sasa huenda hali inaweza kuwa tofauti, opposition wengine ni very useful, si hopeless kama zamani. Hapo naona ilikuwa inatafutwa njia ya kum-blackmail wameikosa. watatafuta nyingine.
   
 3. m

  muheza2007 JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 233
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 60
  Ukifuatiliwa kwasababu umetenda kosa kuna ubaya gani? Kama yeye anakosoa wenzake lazima na yeye ahakikishe hana makosa.


  I don't care about the motive, so long you committed or you are committing a crime, it fine with me if police decide to put you behind bars.
   
 4. G

  Godwine JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  kama anamakosa basi sheria ichukue mkondo wake jamii isianze kuangalia kila kitu kinachofanywa na serikali kwa mabaya zaidi kwani si kwamba ukiwa kiongozi wa upinzani basi gari lako liendeshwe hata kama vibali vyake vimeisha muda usiambie lolote, cha msingi kwa wao wanaotaka kuwa viongozi wa baadae wawe mstari wa mbele katika kufanya mema na si kutaka sheria ziwapendelee
   
 5. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Am sure that is a cheap excuse they might have used to reach their motive. Am as well sure that our police officers have better and much more efficient ways of doing that, than motobike chase. Kuna kitu walikuwa wanatafuta walikosa, hichi walitumia kisingizio, ambacho mimi naona ni kizuri sana. Lakini subiri tu uone yanayofuata.
   
 6. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,064
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu
  Mbona kosa hilo ni la kawaida sana hasa hapa Dar?????? Tunakamatwa sana kuhusu bima kutokana na kutokuwa makini na expiry dates.
  Wasomi wangu, si mnajua athari ya kuendesha gari bila bima????? mbona mnalifanya suala hili kuwa kubwa kuliko linavyostahili????
  Au kwa sababu ni Mpendazoe???????? Jee ndugu yako akigongwa na gari lisilokuwa na bima unaijua adha yake?????????????
  Tuache ushabiki usio na msingi. This is a traffic case and thats' it.
   
 7. Eng. SALUFU CA

  Eng. SALUFU CA Senior Member

  #7
  Jun 3, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi ni vitu vya kawaida jamani, kwani bima/Motor vehicle licence kuisha muda wake sio inshu wala nini, kakate Mpendazote uachane na hao jamaa.
   
Loading...