Sakata la aliyeuawa na Gari la Magereza, ndugu wamkomalia Mkuu wa Gereza

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,323
7,963
SAKATA la ndugu wa Richard Bukombe mkazi wa Miyuji jijini Dodoma, aliyefariki dunia kwa madai ya kugongwa na gari la Jeshi la Magereza limechukua sura mpya baada ya wanafamilia kumtaka mkuu wa jeshi hilo kutowakingia kifua wahusika.

Pia wameiomba Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kuingilia kati sakata hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapo kwa niaba ya familia, mdogo wa marehemu, Bukombe Bulole, alisema pamoja na kuzika mwili wa ndugu yao, hawatakata tamaa ya kupata haki ya ndugu yao.

Baada ya kuuzika mwili wa ndugu yao, alisema walifuatilia katika Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Dodoma na kubainika kuwa mwili wa ndugu yao ulipelekwa na kutelekezwa katika chumba cha kuhifadhia maiti na askari Magereza.

“Kamishna (Jenerali) anapaswa kulifanyia kazi hili kwani liko mikononi mwake. Asiwape kazi viongozi wake wa juu kwa ajili ya kuwalinda wahusika. Tunamwomba sana atusaidie, hakuna haja sisi kumfuata Waziri Mkuu au Rais Samia Suluhu Hassan afanye kitu ambacho ni jukumu la mteule wake,” alisema Bukombe.

Alisema kuendelea kukaa kimya kwa Jeshi la Magereza kunazidi kuwapa hofu kuwa ndugu yao alipogongwa na gari hakuwa amekufa bali wao ndio waliommalizia ili kuondoa ushahidi.

“Ndugu wanahabari, Sheria ya Usalama Barabarani kifungu cha 57 (ii) (b) kinamtaka mtu yeyote atakayesababisha ajali aripoti kituo cha polisi ndani ya saa 12 ila sheria itamsamehe akichelewa endapo kutokana na ajali hiyo atakuwa hawezi kutimiza takwa la sheria hiyo.

“Lakini kifungu cha 40 sura ya 168 kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002 inasema mtu yeyote atakayesababisha majeruhi au kifo kwa mujibu wa Sheria ya Usalama Barabarani atakuwa ametenda kosa la jinai,” alisema.

Bukombe alisema kwa kuwa Magereza ni miongoni mwa vyombo vinavyohakikisha sheria za nchi hazivunjwi na kwa kutoripoti ajali ile kituo cha polisi, wamevunja sheria.

“Hivyo askari Magereza ambao ni wasimamizi wa sheria za nchi wametenda kosa la jinai na tunawaomba viongozi wao wawafikishe mahakamani mara moja bila kusumbua vyombo vingine vya usalama kuchunguza jambo hilo,” alisisitiza.

Pia alisema familia inamwomba Mkuu wa Magereza aige mfano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene, alivyoruhusu sheria ifuate mkondo wake kwa mtoto wake ambaye alivunja sheria za nchi.

Bukombe alisema tangu ajali ilipotokea Septemba 13, mwaka huu, hadi sasa zaidi ya siku 14 zimepita bila kuona chochote kilichofanywa na jeshi hilo zaidi ya danadana za kivuta muda ili wasahau na kuacha kufuatilia jambo hilo.

Richard Bukombe, maarufu kwa jina la Baba Paroko, anadaiwa kugongwa na gari la Jeshi la Magereza (Landcruiser pickup) Septemba 13, mwaka huu, jirani na eneo la Hoteli ya Twiga, Msalato jijini hapo.

Kwa mujibu wa ndugu zake, aligongwa na gari hilo majira ya saa 12:30 jioni na baadhi ya askari wa jeshi hilo walimchukua na kuondoka naye kisha baadaye mwili wake kukutwa umetelekezwa mochwari.

Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Kenneth Mwambije, alipoulizwa kuhusu tukio hilo, alikiri kuwa analifahamu kama ambavyo watu wengine wanavyolisikia lakini akasisitiza kuwa watu wa kulitolea ufafanuzi ni makao makuu ya jeshi hilo.

Wiki iliyopita, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yussuf Masauni, alipoulizwa kuhusu tukio hilo, alisema anaomba kwanza kukutana na wanafamilia ili kusikiliza malalamiko yao.
 
Kosa kubwa mlilofanya ni kukubali kumzika malehemu.
Hizi mnazofanya kwa sasa no kelele tupu.
 
Tupo kwenye nchi ya DICTATOR genge la polisi linabaka,magereza wanabaka,genge la polisi linaandaa maandamano ya kupongeza kubaka ni hatari
 
Kususia maiti sioni kama ni busara sana maana baada ya muda ataenda kufukiwa na Manispaa (badala ya kuzikwa kwa heshima zote na familia yake).
Wanaofukiwa na manispaa ni waliokosa ndugu zao. Wenye ndugu hata akae miaka 10 hawawezi mzika.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom