Gari la Lema lashambuliwa na UVCCM - Arusha

Gari la Lema lashambuliwa na UVCCM - Arusha

Mkuu watu walikuwa na Imani na LEMA ila baada ya kubaini ulaghai, ufisadi, uhuni wake! kila mtu anamuona wa ajabu!
akinamama wa sokoni pale NMC hawataki hata kumuona, na ndio waliokuwa supporters wake wakuu!
Nawewe ni mmoja wa hao kina mama etiee
 
Lema avamiwa na ‘UVCCM’, gari yake
yasuliwa vioo; alazimika kufyatua risasi
tatu hewani kujiokoa!

Gari la Godbless Lema lililovunjwa kioo huko Clock
Tower, Arusha

Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema amekubwa
na tukio la aina yake maeneo ya Clock Tower Jijini hapa
ambapo vijana wanaoaminika kuwa vijana “wafuasi wa
UVCCM” walishamshambulia kwa mawe na kufanikiwa
kuvunja kioo cha nyuma ubavuni cha gari la Mbunge
huyo.

Tukio hilo la kustaajabisha na kutiasha katika swala la
amani na usalama kipindi hiki cha kampeni za Serikali za
mitaa lilitokea kwenye Sheli iliyopo mkabala na New
Arusha Hotel majira ya jioni saa moja ambapoMbunge
Lema akiwa na dereva wake na mtu mwingine mmoja
walijikuta wakishambuliwa vikali na watu ambao Mh
Lema amethibitisha ni vijana waliokuwa kwenye msafara
kampeni.

Blog hii ilifanikiwa kufika Kituo Kikuu cha Polisi Jijini
Arusha usiku wa saa tatu na kumkuta Lema na wafuasi
wa Chadema zaidi ya 200 wakiwa na viongozi wao katika
kituo hicho kikuu kwa ajili ya kutoa maelezo na taratibu
nyingine za kipolisi zifuate.

Akisimulina namna ilivyokuwa, Lema alisema kuwa
muda huo akiwa garini kuelekea nyumbani alimuona
kijana mmoja anapigwa sana na vijana hao wa CCM
wakiwa na sare za chama. Anasema kijana huyo alikuwa
anapigwa mno na kuburuzwa kupelekwa maeneo ya
mtoni ambapo alihisi angeweza kuuawa.

Lema akamuamuru dereva wake kusimaiisha gari na
mtu mwingine waliyekuwa nae kwenye gari akashuka
kumuokoa kijana yule. Baada ya kufanikiwa
kuwatenganisha na kuwashikilia vijana wawili wa CCM
waliokuwa wanampiga yule kijana, kundi kubwa la vijana
wengine wakiwa na silaha na mawe walishuka kutoka
kwenye Lori walilokuwa wakisafiria kutoka kwenye
kampeni na kumvamia wakijaribu kuwaokoa wenzao
kuondoa ushshidi. Lema akalazimika kupiga risasi ya
kwanza hewani wakarudi nyuma kama hatua kadhaa.

Baada ya sekunde kadhaa wakarudi tena kumzonga
Lema huku wakirusha mawe na silaha nyingine. Mawe
yale yalijaeruhi baadhi ya watu waliokuwa jirani pamoja
na mhudumu wa Sheli hiyo kupigwa marungu na Lema
hakujua hali yake ikoje.

Walivyozidi kumshambulia na mawe na silaha nyingine
na kufanikiwa kuvunja kioo cha gari yake, Lema alifyatua
tena risasi ya pili na ya tatu kuwatawanya na
akawasiliana na Polisi ambapo kituo hakiko mbali lakini
anasema simu ya OCD na OCS hazikuweza kufanya
mawasiliano.

Akalazimika kuwafuata askari Kituo Kikuu na kwa
pamoja wakarudi eneo la tukio na kuwakuta vijana wale
bado wako wanaimba nyimbo za kusifu chama chao.

Lema anasimulia kuwa vijana wale walimdhihaki OCD
wakimuimbia nyimbo kwa shangwe ambaye pamoja na
askari wake hawakuweza kumkamata hata mtu mmoja
wala kukamata gari hilo.

Baadae ndio akarudi kituoni kutoa maelezo huku wafuasi
wa Chadema wakishinikiza kama Polisi hawawezi
kuwakamata watu hao usiku huo basi wawaachie kazi
hiyo waifanye wao wenyewe kuhakikisha kabla
hakujakucha watu wote wametiwa nguvuni kwasababu
wanajulikana!

Mpaka Blog hii inaondoka kituoni hakukuwa na
kukamatwa kwa mtu yeyeote zaidi ya askari Polisi na
viongozi wa Chadema kusaidiana kutafuta maganda ya
risasi eneo la tukio.

Polisi bado hawajatoa taarifa yeyote kuthibitisha tukio hilo
 
Kwa kupiga risasi hewani LEMA alisababisha hasara kubwa sana na usumbufu kwa raia wa Tanzania na wa kigeni waliokuwa wamepumzika Hotelini NEW ARUSHA.

Pia watalii waliokuwa maeneo hayo wameondoka wakiwa na taswira mbaya sana kuhusu Arusha!

LEMA wakati mwingine tumia busara. Kumiliki bastola sio lazima urushe rushe risasi ovyo!
 
Maccm wanaozipiga risasi na mabomu na kung'oa kucha na meno kila kukicha wanaleta taswira nzuri kwa watalii?
 
Kwa kupiga risasi hewani LEMA alisababisha hasara kubwa sana na usumbufu kwa raia wa Tanzania na wa kigeni waliokuwa wamepumzika Hotelini NEW ARUSHA.

Pia watalii waliokuwa maeneo hayo wameondoka wakiwa na taswira mbaya sana kuhusu Arusha!

LEMA wakati mwingine tumia busara. Kumiliki bastola sio lazima urushe rushe risasi ovyo!
Unavurugwa
 
Kwa kupiga risasi hewani LEMA alisababisha hasara kubwa sana na usumbufu kwa raia wa Tanzania na wa kigeni waliokuwa wamepumzika Hotelini NEW ARUSHA.

Pia watalii waliokuwa maeneo hayo wameondoka wakiwa na taswira mbaya sana kuhusu Arusha!

LEMA wakati mwingine tumia busara. Kumiliki bastola sio lazima urushe rushe risasi ovyo!

Maccm wanaopiga risasi, mabomu na kung'oa kucha za watu bila kusahau ufisadi kila kukicha. Je, wao wanaleta taswira nzuri kwa watalii?
 
Maccm wanaozipiga risasi na mabomu na kung'oa kucha na meno kila kukicha wanaleta taswira nzuri kwa watalii?

Sio kwa ajili anamiliki bastola ndio awaonee wananchi wanyonge kwa kuwatishia kuwapiga risasi.
 
Sio kwa ajili anamiliki bastola ndio awaonee wananchi wanyonge kwa kuwatishia kuwapiga risasi.

Na nyie sio kwa kuwa mnamiliki dola ndio mtuonee wananchi kwa kutung'oa meno na kucha.
 
lema kila ianapokaribia
uchaguzi lazima afanye kituko kutafuta sympathy ya kura, ameshaona watu
wa arusha wanadanganyika kwa mbinu zake, ipo siku atajipiga risasi na
kusingizia sisiem ili aonewe huruma, this guy is a disgrace,
apuuzwe

I salute you! Truth has to be said!
 
We mangi ndo umepitwa na wakati kweli kweli! nikutizama kifikra tu nakuona umevaa kaunda suti na raba, unaendesha toyota staut old model, na christmas hii utapandisha milimani na makochi kwe staut yako na baada ya sherehe utarudi nayo mjini.We hujui hata escrow kuwa haimhusu Lema wala Chagadema, nikukumbushe tu.
1.Mtoa hoja Kafulila-alifukuzwa chadema.
2.Mwenyekiti PAC-Mhe.Zitto, alifukuzwa chagadema.
3.CAG aliyefichua uozo-kateuliwa na serikali ya ccm.
4.wajumbe Filikunjombe,Kigwangala,Lugola,Mpina na wengine zaidi ya nusu ni wa ccm!
Sasa kwa wenzio wameshastuka kuitumia escrow kama mtaji wa chagadema bali wewe bado hujitambui! escrow haikuletwa na chadema.na sio ajenda ya kuleta maendeleo kwa wagombea wenu waseme vision yao ya 2015-2020. usimshabikie jambazi LEMA hana ishu zaidi ya maandamano na wizi wa magari.

Katika post yangu hakuna mahali nimesema kuwa Kafulila ni CDM. Pili yeyote yule akifanya jambo la kitaifa siangalii uchama. Kwa taarifa yako tu ni kwamba mimi sina chama cha siasa hata kidogo, hata kadi sina. Na lingine mimi si mchaga hata kwa kuchanjwa. Naona wewe uko katika akili za kushambualia CDM na wachaga tu. By the waya matokeo ya chaguzi serikali za mitaa unayo?? CDM imeongoza mikoa kadhaa na maeneo mengi mno nako ni uchagani huko? Hata huyo Kafulila na Zitto pamoja na kukalia suala la Esrow koo but wamepata viti vingapi ? Cha msingi watanzania wa leo si wale wa juzi, jana na leo!!! Wa kesho ni hatari zaidi!! Pole sana, ukabila na uchama hautakufikisha popote!! Let us look at our lovely Tanzania ni totality when it comes to crucial and sensitive national matters.
 
Back
Top Bottom