Crashwise
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 22,227
- 8,760
Akiwa anaekekea nyumbani kwake Mbunge Wa Arusha Mjini Mhe. Godbles Lema ameshambuliea na vijana wa uvccm maeneo ya clock Tower,..kuna watu wameumia katika tukio hilo ambalo vijana wa ccm walimvamia lema wakiwa na mashoka, panga na mipini..
===============
===============
Chanzo: NipasheLema: Machokoraa waliotumwa na CCM walitaka kuniua
Siku moja kabla ya uchaguzi wa wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Mbunge wa Arusha, Godbless Lema, amesema amenusurika kuuawa baada ya kuvamiwa na vijana wa mitaani waliokuwa na mapanga, marungu na mafyekeo.
Alisema tukio hilo lilitokea jirani na kituo kimoja cha mafuta kilichopo eneo la mzunguko wa Mnara wa Saa majira ya saa 1:30 jioni, wakati kundi hilo alilodai kuwa ni machokora linalotumiwa na CCM kutaka kuvuruga uchaguzi.
Alisema alipofika maeneo hayo alishuka kwenye gari lake kwa lengo la kumsaidia mtu aliyekuwa amevamiwa akipigwa na vibaka hao na ndipo walipomgeukia na kusema kuwa ndiye waliyekuwa wamkitafuta.
"Mimi nimekuwa mhanga wa uvamizi wa kundi hili na polisi walishuhudia kundi hili likiwa na mapanga, marungu na silaha mbalimbali zinazoweza kutumika kwa kudhuru na kuharibu mali na maisha ya binadamu.
"Ni watoto wa mitaani, wanaolala kwenye takataka, pembeni mwa uwanja wa mpira na maeneo mengine…hao ndio wanaotumiwa na CCM sasa hivi ili kuleta vurugu.
"Nililazimika kupiga risasi tatu hewani lakini bado walikuwa wakinifuata, nikajitahidi kujinusuru lakini walifanikiwa kuharibu gari langu kwa kuvunja kioo cha nyuma," alisema na kuongeza alitoa taarifa ya tukio hilo polisi na kufunguliwa faili namba AR/RB/16/681/14.
Alisema vijana hawa wasipodhibitiwa uchaguzi huo utakuwa na vurugu.
"Mimi mbunge naomba kutoa tahadhari kwamba genge hili lisipodhibitiwa sasa, ninaona mashaka na hatari kubwa itakayoweza kutokea 14/Desemba/2014 na kusababisha mauaji makubwa," alisema.
Alisema maeneo yote ya Arusha yanahitaji ulinzi wa hali ya juu lakini maeneo kama Sekei, Ngarenaro, Sombetini, Elerai, Unga Ltd, Daraja Mbili, Olasiti, Sokoni 1, Murriet, Kaloleni na Kata ya Kati yanahitaji uangalizi maalum wa kiulinzi juu ya tetesi na mipango mibaya inayopangwa huko.
Akizungumzia tuhuma za Lema, Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha, Feruzi Bano, alisema chama chake katu hakiwezi kuwatumia vijana machokoraa kumdhuru mbunge huyo.
"Huyu ni mbunge wetu hatuna shida naye, huu ni uchaguzi wa Serikali za Mitaa, sasa kwa nini tuwe na nia ya kumdhuru…unajua huyo kila unapokuja uchaguzi anazua mambo na tuhuma hizi sio za kweli kabisa," alisema.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daud Felix Ntibenda, alisema suala la madai ya kuvamiwa kwa mbunge Lema, linashughulikiwa na vyombo vya usalama.