Gari la CCM likiwa na Mama Makamba lapata ajali

siku zote tutambue malipo ni hapa hapa duniani,lisipotendeka kwako litatendeka kwa watoto auukoo wako,kitendo cha kutumia Bilblia wakati yeye ni fisadi sio jambo nzuri ile Biblia ni takatifu
 
kama kuna majeruhi basi Mungu awanusuru na kifo na awape huruma yake, kwani si kila baya litalipwa kwa baya.
Mnakumbuka Mungu alimruhusu mtumishi wake mmoja aoe kahaba ili kudhihirisha machukizo aliyofanyiwa na wana wa israel?

Sote ni binadamu hatuombeani ajali,kama ni kweli Mungu awape nafuu na kuwatangulia kwa nguvu zake! Tunawapenda
 
Taarifa kutoka ofisi ya CCM mkoa wa Dar es Salaam zinaonyesha kwamba gari mpya kabisa aina ya land cruiser ya CCM mkoa wa dsm imepata ajali na kupinduka na kuwa write off wakati ikiwa safarini kumpeleka mke wa Yusuph Makamba - katibu mkuu wa CCM mkoani Tanga kwenye mapumziko ya mwisho wa mwaka.

Inadaiwa kuwa Makamba alichukua gari hilo la CCM mkoa kibabe kwa kutumia cheo chake. Kama angefuata utaratibu CCM makao makuu inayo magari mengi ambayo yangefaa kwa shughuli hiyo, badala ya kujichukulia gari la mkoa ambalo sasa limepata ajali na kuharibika kabisa.

naomba kuwasilisha

Anawake kama wanne hivi ni yupi unamsema wewe
 
Mama habebi dhambi za mumewe, kama ni kweli hii habari, tuwaombee uzima. kama ni uongo; mtoa mada ushindwe na ulegee.
 
Miili iko Muhimbili tayari au wameshaazika sawa na waafu wetu Omari na Denisi wa kule Arusha? RIP Makamba family!!
 
Back
Top Bottom