Gari kunguruma sana

relis

JF-Expert Member
May 24, 2015
3,332
5,212
Habari!

Msaada kwa mwenye ujuzi/uzoefu gari yangu Premio e ina engen aina ya 7a_fe,cc 1800 kinachonitatiza ikitokea nikanyaga mafuta mengi mpaka rpm ikafika kwenye nne engen hunguruma sana na sauti kama mruzi na mlio wake huusikia mpaka ndani ya gari, lakini ni nikisikiliza gari nyingine zenye ukubwa wa aina hiyo ya cc1800 kwa ukanyaji huo sioni hicho kitu na engen zao huwa kimya eg.VVTI engen msaada.
 
Vipi mkuu ulishajaribu kulipeleka kwa Mafundi baada ya hilo tatizo kuanza??
 
Muungurumo mkubwa huletwa nayafuatayo! Jaribu kuipandisha juu gereji uchungulie chini
1. Ekisosi inaweza kuwa inavuja sehemu, tundu dogo au kreki ndogo inaweza sababisha muungurumo ukawa mkubwa ...kachomelee bei ni elfu 10000/tu.
2. Mounting ya ekisosi ikikatika au kuchoka pia huchangia mlio.
3. Engine mounting...hii si sana lakini huchangia
4. Plug ambazo zimechoka au zisizofaa husambabisha combustion kufail, kiasi kwamba hadi uganyage sana ndiyo ina burn.
.MWISHO,
Kutokana na barabara zetu ebu cheki ekisosi yawezekana ndiyo imepasuka...ndiyo maana wanaotaka milio mikubwa hutoboa ekisosi..
(NIMETUMIA LUGHA RAHISI ILI UELEWE)
 
Muffler huenda imeziba imapitisha hewa kidogo. Au exhaust inacrack. Ukikanyaga sana kama hadi exhaust pipe inatetemeka check muffler.
 
Kuna mengi yanaweza pelekea tatizo hilo.
Mpaka unafika 4 kwenye RPM inamaanisha unakua ushavuka ile alama ya kijani ambayo kikawaida ndio sehemu ambapo mshale wako watakiwa kucheza.
Sasa tatizo laweza kua
A-Gear box
B-Fanbelt
C-engine ipo loose

Ni vizuri u describe hizo kelele ili iwe rahisi kubadilishana mawazo.
 
Kuna mengi yanaweza pelekea tatizo hilo.
Mpaka unafika 4 kwenye RPM inamaanisha unakua ushavuka ile alama ya kijani ambayo kikawaida ndio sehemu ambapo mshale wako watakiwa kucheza.
Sasa tatizo laweza kua
A-Gear box
B-Fanbelt
C-engine ipo loose

Ni vizuri u describe hizo kelele ili iwe rahisi kubadilishana mawazo.
Hapo kwenye giabox sina shaka sana naomba elimu kuhusu feni belt,na hiyo engen kuwa loose inakuwaje Mkuu,asante
 
Kawaida,hata Mimi Nina Carina si 7A,ina shida hiyo lkn hainisumbui,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom