Garden za kuchezea watoto

Garden za kuchezea watoto

CHE GUEVARA-II

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2010
Posts
571
Reaction score
157
Wadau, habari zenu?
Naomba mnisaidie kunielekeza mahali ambapo naweza kuwapeleka wanangu wafurahie na wenzao wakati wa sherehe (birthday) ya mwanangu.
Nahitaji sehemu zinazopatikana maeneo ya karibu na Pugu, Gongolamboto, Chanika n.k.

Niko Viwege-Majohe

Mnipatie na contacts ikiwezekana ili nipate details za eneo husika.

Asanteni.
 
CHE GUEVARA-II

Teh teh het tee eti garden watengenezee tu hapo kwako mjomba vinginevyo safiri mpaka nairobi hivyo vitu utavipata kwa tanzania bado kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Teh teh het tee eti garden watengenezee tu hapo kwako mjomba vinginevyo safiri mpaka nairobi hivyo vitu utavipata kwa tanzania bado kabisa.

Tanzania hamna kitu kama hicho! sanasana watu wamewatengenezea majumbani mwao watoto wao!
 
CHE GUEVARA-II

kwanini usiende Kwa Mzungu/Kiota? Kama unaenda Stakishari Polisi banana, garden swimming pool nzuri,namba zao sina bahati mbaya, bila shaka hutapotea.
 
Last edited by a moderator:
Teh teh het tee eti garden watengenezee tu hapo kwako mjomba vinginevyo safiri mpaka nairobi hivyo vitu utavipata kwa tanzania bado kabisa.
sema anakotaka hakuna ila kama anamudu safari, basi Dar Live pangemfaa..
 
Teh teh het tee eti garden watengenezee tu hapo kwako mjomba vinginevyo safiri mpaka nairobi hivyo vitu utavipata kwa tanzania bado kabisa.

Una uhakika Tz hakuna mkuu? Mbona zipo Sema kwa location aliyosema hakuna hujatembea ukaona usipende kuidharau bongo yetu.
 
Tanzania hamna kitu kama hicho! sanasana watu wamewatengenezea majumbani mwao watoto wao!

Msiidharau nchi yenu kiasi hicho,garden zipo mseme hamzijui tu. Na pia hayo maeneo alotaja sina hakika kama zipo.
Mfano tabata GBF ni karibu kwake pia kuna garden nzuri sana kwa watoto.
 
Mimi serikali ya SMZ nimeipendea hapo tu wamejitahidi kujali watoto ki ukweli.....Kuna garden za kutosha....Forodhani,Kariakooo,jamuhuri na ni free of charge isipokuwa kariakoo kwa vile kuna kila aina ya vifaa ambavyo vitamfanya mtoto a enjoy ila kwa Dar ukienda sehemu kama hizo sharti uwe na fungu mfukoni na ni za kutafuta na tochi pia nyingi zipo kwenye ma hoteli.
 
sema anakotaka hakuna ila kama anamudu safari, basi Dar Live pangemfaa..

Dar live fujo tu maana ya garden ni sehemu tulivu mauwa mazuri penye ukijani na hewa safi ya Mungu na muziki mwororo wa ndege hapa ndipi unapowezapata chakula cha ubongo ukiwauliza wenzetu wanaojua maana watakuambia uzuri wake sio huku kwetu ofisin stress, nyumbani baba mwenye nyumba shida, usafiri wa mawazo, pesa zenyewe kila uchwao zashuka samani ukitaka kupumzisha akili uende dar live full makelele halafu uniambia watu wanaoongea wenyewe barabarani watapungua thuubuutuu.
 
Kama hutojali njoo huku Kigamboni Fun City kwa watoto ndo mwisho wa reli.
 
Segerea mwisho kina garden nzuri kwa watoto, kila kichwa buku3 kuenjoy hapo
 
Huku kwetu zamani kulikuwepo garden na kulikuwa na be mbna etc ila kwa sasa maeneo yote ya wazi ya watoto kucheza tena ilikuwa bure hulipi kitu ...zote zimeuzwa.
 
Mkuu, naomba directions au contacts.
Huko Fun City niliwapeleka mwaka 2013.
Mwaka huu nilitaka niwapeleke Dar-es-salaam Zoo (Kigamboni), lkn nimewasiliana na wahusika hapo Zoo wameniambia tarehe 19 June hawatakuwepo kikazi (watafunga kwa muda ktk kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhan).

Nyumbani kuna garden na bembea, lkn sehemu moja inachosha!
 
@CHE GUEVARA-II

kwanini usiende Kwa Mzungu/Kiota? Kama unaenda Stakishari Polisi banana, garden swimming pool nzuri,namba zao sina bahati mbaya, bila shaka hutapotea.

Kiongozi, naomba unisaidie directions ma/ au unisaidie kupata contacts za hiyo sehemu.
 
Yaani Dar ni fun city na Zoo tu,wapeleke sadani wakaone na wanyama

Asante kwa ushauri.

Nahitaji sehemu ya kwenda siku moja na kurudi siku hiyo hiyo.
Isiwe mbaaali sana na nyumbani.
Kama hazipo sehemu za hivyo maeneo ya karibu basi.

Huko Sadani, Mikumi, Serengeti, Ngorongoro na sehemu zingine zinazofanana na hizo zinafaa wakati wa VACATION (annually),
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom