Gangnam Style: Muziki wa Korea Ulioburudisha Dunia Yote

Gangnam Style: Muziki wa Korea Ulioburudisha Dunia Yote

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,132
Reaction score
10,514
Mwaka 2012, dunia ilishuhudia tukio la kipekee katika historia ya muziki wa kimataifa. Wimbo wa “Gangnam Style” ulioimbwa na msanii wa Korea Kusini, PSY, ulivutia hisia na kujenga wimbi kubwa la furaha, kucheka, na kuigiza mtindo ya kipekee wa kucheza ambayo ulipendwa na dunia nzima. Hata bila kuelewa maneno ya Kikorea, mamilioni ya watu waliupenda wimbo, wakaimba, na kucheza wimbo huo.
images (72).jpeg

Wimbo huu ulitoka chini ya YG Entertainment, moja ya studio maarufu zaidi za muziki Korea Kusini. Hawa YG Entertainment ni kampuni maarufu kwa kugundua na kukuza vipaji vya muziki wa K-pop, na imekuwa na historia ya kutengeneza wasanii wenye sauti ya kipekee na mtindo wa kipekee wa muziki. PSY akiwa mmoja wa wasanii ambao walipata nafasi ya kusaidiwa kimuziki na YG Entertainment.
images (71).jpeg

Mmoja wa watu wa muhimu zajdi waliochangia mafanikio ya “Gangnam Style” ni Cho Soo-hyun, mkurugenzi maarufu wa video za K-pop ambaye alichanganya ubunifu, vituko, na mtindo wa kipekee wa aina ya uchezaji.
images (70).jpeg

Video hiyo ilionyesha maisha ya kifahari ya mtaa wa Gangnam, Seoul, na mtindo wa kucheza wa “horse-riding” iliyokuwa kipekee na rahisi kuigiza. Usimamizi na uongozi wa maudhui wa studio ya YG Entertainment vilifanya video hii kuleta kitu kisichokuwa cha kawaida katika muziki haswa kutoka Korea Kusini.
images (69).jpeg

Hapa ndipo wimbo huu ulipochukua kipimo cha ulimwengu. PSY na YG Entertainment walitumia mitandao ya kijamii kama YouTube, Facebook, na Twitter kufanikisha kuwa wa wimbo huu unasambaa mbali zaidi ya Bara la Asia. Video ilipata mamilioni ya “views” ndani ya wiki chache, na maelfu ya watu walijitahidi kuiga dansi ya kipekee ya “horse-riding”.
images (68).jpeg

Wimbo huu ulipita mipaka ya Korea Kusini na kufika Amerika, Ulaya, Afrika, na Asia yote. “Gangnam Style” ilikuwa video ya kwanza kufikisha views bilioni kwenye YouTube, jambo ambalo halijawahi kutokea hapo awali.
images (67).jpeg

Kwa hivyo, miaka zaidi ya kumi baada ya “Gangnam Style” kuachiwa, wimbo huu bado unaendelea kuwa mfano wa mafanikio ya muziki wa kimataifa, ukiendelea kuhamasisha wasanii na mashabiki wa muziki duniani kote.
images (64).jpeg
 
Back
Top Bottom