GAMONDI: Yanga haina kikosi kipana

franckkimm

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
440
852
Kocha mkuu wa Yanga amesema:

Kumekuwa na maneno mengi kuwa sifanyi mabadiliko ya kikosi kwa wachezaji. Nilianza kufanya hivyo nilipata matokeo mabaya dhidi ya Ihefu FC katika mechi ya Ligi Kuu tulipofungwa mabao 2-1. Nilipoona matokeo sio rafiki nikaendelea na mfumo wangu mashabiki waliendelea kuzungumza,” .

“Kwenye Mapinduzi nimetoa nafasi kwa wachezaji wote kucheza, lakini sioni wakipambana. Sina budi kusema ni kweli nina kikosi bora, lakini sio kipana. Hii ni kutokana na ubora wa wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza kuwa juu zaidi kuliko ninaowatumia kwenye mashindano haya.” .

“Wachezaji wanashindwa kujituma na hawapambani kama matarajio ya wengi yalivyo, hivyo ana kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha kila mmoja anawajibika ili kuipambania timu.” alisema Gamondi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wabongo wengi tafsiri ya kikosi kipana bado imekuwa ni tatizo.

Wengi wanaamini kuwa na idadi kubwa ya wachezaji ndio maana halisi ya kikosi kipana wakati katika kundi hilo kubwa ni wachache tu ndio tegemeo.

Sasa una wakina Mkude, Skudu, Konkoni, Farid Mussa, Nkane, Kibabage nk ambao wote hao wanapata nafasi ya kucheza ikiwa wachezaji wenzao wanaopewa nafasi katika hizo position wana majeraha

Kwa Tanzania hapa bado sana kusema tuna timu zenye vikosi vipana.
 
Kazi imemshimda huyu kichwa papai, tutamrudisha huko kwao akaendelee na kazi yake ya kulima matikiti maji
 
Wabongo wengi tafsiri ya kikosi kipana bado imekuwa ni tatizo.

Wengi wanaamini kuwa na idadi kubwa ya wachezaji ndio maana halisi ya kikosi kipana wakati katika kundi hilo kubwa ni wachache tu ndio tegemeo.

Sasa una wakina Mkude, Skudu, Konkoni, Farid Mussa, Nkane, Kibabage nk ambao wote hao wanapata nafasi ya kucheza ikiwa wachezaji wenzao wanaopewa nafasi katika hizo position wana majeraha

Kwa Tanzania hapa bado sana kusema tuna timu zenye vikosi vipana.
Ila kibabage naona anazidi kuimarika kadiri anavyopata muda wa kucheza. Hao wengine uliowataja kwa kweli waondoke tu hata sasa hivi.
 
Jana Gamond kaingia na mfumo wa 4 2 4 lengo lake likiwa ni kukabia mbele kilichotokea sasa ndo nilichoka , wale wanne wa mbele wakawa wanakabia kwa macho wanasubiri mipira itoke nyuma ikiwafikia wakaipoteza hawajui kukaba matokeo yake mabeki wakawa wanakula kazi ya ziada kuzuia mipira isilete madhara wakati mwingine ikawalazimu wawe wanapanda kushambulia maana walioko mbele ni ziro, ktk wale madogo wa zenji mchezaji ni shekhan tu yule TAMILA ni kiazi haswa
 
Kocha mkuu wa Yanga amesema:

Kumekuwa na maneno mengi kuwa sifanyi mabadiliko ya kikosi kwa wachezaji. Nilianza kufanya hivyo nilipata matokeo mabaya dhidi ya Ihefu FC katika mechi ya Ligi Kuu tulipofungwa mabao 2-1. Nilipoona matokeo sio rafiki nikaendelea na mfumo wangu mashabiki waliendelea kuzungumza,” .

“Kwenye Mapinduzi nimetoa nafasi kwa wachezaji wote kucheza, lakini sioni wakipambana. Sina budi kusema ni kweli nina kikosi bora, lakini sio kipana. Hii ni kutokana na ubora wa wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza kuwa juu zaidi kuliko ninaowatumia kwenye mashindano haya.” .

“Wachezaji wanashindwa kujituma na hawapambani kama matarajio ya wengi yalivyo, hivyo ana kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha kila mmoja anawajibika ili kuipambania timu.” alisema Gamondi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Gamondi naye alishindwa kuja na mfumo mzuri wa kuwatumia hawa wachezaji wasiocheza mara kwa mara. Huu mfumo wa kucheza kwa taratibu na wa pasi nyingi (nyingi zikiwa back passes) nao ni changamoto nyingine.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Bongo kazi sana. Kwahiyo akiulizwa awe anakaa kimya? Au kuna siku ameongea bila kuulizwa?
Mashabiki wa mpira Tanzania tunagubu, hila, wivu, ujuaji, sana. Ndio maana mtu ana comment bila kushirikisha ubongo wake ili mradi tu akosoe taaluma ya kocha.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom