MSEZA MKULU
JF-Expert Member
- Jul 22, 2011
- 3,763
- 5,605

Baada ya miaka 22 madarakani hivi karibuni rais wa Gambia alishindwa uchaguzi wa kidemokrasia.
Cha ajabu hadi sasa ajakubali kushindwa, Majeshi ya nchi za afrika magharibi yakiongozwa na Senegal yanawekwa standby asipokubali mazungumzo ya kuachia madaraka kwa amani wamtoe kwa nguvu ya jeshi.
Kiongozi wa ECOWAS Marcel de Souza anasema, Kama anapenda wananchi wake, Yahya Jammeh atakabidhi nchi kwa amani, Vinginevyo Senegal wataongoza kikosi cha kumtoa kwa nguvu kijeshi
Mshindi wa uchaguzi BARROW anasema ataapishwa kuwa Rais na anategemea Marais wa afrika magharibi waudhurie bila kujali Yahya Jammeh atakuwa na position gani wakati huo.
Hii ndio afrika yetu.
Source:Forces on standby to oust Gambian president Yahya Jammeh