Gaddafi calls black africans "ignorant"

Gaddafi calls black africans "ignorant"

Br. juma ,

Hakuna mkimbizi anayependa hali ya ukimbizi. It is a matter of being between a stone and a hard surface, ndio unakuta mtu anatoka alipotoka kwenda nchi ya mbali asioijua kwa matumaini ya hali bora. Suluhisho ni kuondoa sababu ya hawa watu kuondoka huko walipo na kwenda nchi nyingine na kuhatarisha maisha yao. Hicho ndio cha msingi.

Inabidi Africa ianze kwa kuondoa viongozi wote walioshindwa kuongoza (tukianza na CCM), hawa ni mzigo mkubwa kwa sababu ndio kama magavana wa ukoloni (na umaskini), na bila kuondoa hawa Afrika itaendelea kuwa maskini wa kutupa na kuendelea kuzalisha wahamiaji (wa kisiasa na kiuchumi) kwa miongo mingi sana ijayo. Kuendelea kuwa na hawa wafidhuli ni kwamba a common mwananchis wataendelea kutokuwa na sauti wala mtetezi.

Pili lazima dunia iangalie mgawanyo wa rasilimali. Wazungu lazima waache kuitumilia Afrika kama chanzo cha malighafi nafuu na kuturudishia kama bidhaa kwa bei zaidi ya mara 10 ya malighafi tuliyowapa kupitia mikataba feki na udhibiti hafifu wa watawala wetu ambao ni magavana wa kikoloni. Lazima dunia iangalie jinsi ya ku-balance baina ya masoko, bei, mazao na malighafi pamoja na labour force. Kusipokuwa na balance, lazima watu wanaoona kuwa wapo compromised na kupigika na maisha wataenda kule kwenye neema, hivo ndivyo ilivyo..sayansi inatuambia kukiwa na mabadiliko system itajiaadjust ili kuondoa effect ya mabadiliko, hamna mwenye uwezo wa kuzuia hayo mabadiliko ya system..hata huyo mwarabu koko Gadafi.
 
huyu ndiyo alitaka kuwa raisi wa africa? USA [united states of Africa]???
 
Abdulhalim,

Kaka unayosema ni ukweli usiopingika mvuto mkubwa wa uhamiaji ni watu kutaka kwenda kujiboreshea 'life chances' mahala pengine, na wakati mwingine siasa za ukandamizaji huwa ni push factor in case of war torn regions or where tribalism is highly associated with people's chances. On the surface inaonekana kwetu tukitoa viongozi wa sasa tutapata suluhisho lakini truth is somehow very far in my opinion.

Narudia hii broad definition of politics ambayo binafsi nimeipenda,' Siasa inakuja kwa kuwa sisi binadamu ni watu wa kuishi kimakundi. Kwa hivyo amna budi hili kuwe na maelewano katika utumiaji wa rasimali unahitajika uongozi wa kuhakikisha haki zinatendeka na kwa kuwa kwenye upungufu wa mahitaji mara nyingi uzuka mfarakano. Hivyo ni muhimu kuwa na uongozi wenye busara na kujua jinsi ya kugawa au kusambaza kilichopo kunafaisha Umma wote na kujaribu kumridhisha kila mwanajamii'.

Hapo ndio mtego wenyewe ulipo na sisi waafrica ndipo tunapokwama especially kuweza kuongeza kilichopo hili watu wanufaike na waridhike hiwe elimu, chakula, maisha bora na mahitaji mengine yote unayoyajua you name it.

Africans in general bado atujaanza siasa za jamii, bado tupo kama tunatumiwa at national level na hawa viongozi the likes of Lowassa kwa manufaa yao and at the world level by western preys. Na under Kikwete ndio tunawaambia mnasubiri nini kuja kutumaliza, ambapo kama unavyosema resources zinahitajika globally. Sasa tusitegemee eti mzungu, mchina, muhundi au mwarabu; iko siku wata tuhurumia au watakuja na fair approaches kwenye maslahi ya taifa lao wakati wana negotiate na sisi, its never going to happen. Kwa mtaji huo kama tunataka siasa safi kutoa CCM ni mwanzo tu bali pia tunahitaji kuweka viongozi wenye uwezo wa ku-deal na mawazo ya dunia hili walinde interest ya taifa letu, tunahitaji watu watakao weza kuja na ubunifu wa kuongeza tulichonacho mfano chakula, technological development, home produce, elimu ya maana, afya (usijenge mihospitali wakati amna ma experts) yaani tunahitaji watu walioenda shule kisawa sawa na wazalendo wa kweli wenye kiburi hili tuweze kufanya lolote la maana. Tukipata mzalendo asiwe na uwezo bado ni tatizo na tukipata msomi asiye mzalendo ni tatizo that is my take.

Hivyo kuwaridhisha waafrica hadi kuwatoa kwenye wimbi la umaskini is a mammoth asking, na kwa jinsi navyosoma siasa za nyumbani huwa sioni light at end of the tunnel. Naona hadithi tu nyingi na kelele mi binafisi naamini wale ambao wamesoma na wanataabika ndio wanatakiwa na sio hawa ma Dr.JK and the likes. Yaani kaka kuelezea hii issue ni kitabu najua wewe unaelewa hilo lakini kuna waafrica kibao ambao hii ni kama hadithi tuu. Embu imagine kuna post watu wanatuma humu ndani ya JF great thinker ajui hata serikali ni nani anakwambia eti serikali imefanya hivi kwa nini JK ajisifu ndio hapo naposemaga binafsi tuna safari ndefu kama hawa ndio wasomi wetu.

Majuzi nimesoma gazeti moja shares za kampuni moja ambayo inafanya oil exploration (Tullow) in Uganda zinaanguka, kwa sababu the Ugandan government inadelay the drilling process na shareholders wanalalamika wengi itawachukua muda kuvuna kipato kwanza amna hata pipes za kupeleka mafuta mmpaka port.

Embu imagine this fools are already moaning about delays on their investment in an african resource. Kibaya zaidi nasikia huko mafuto yalipo ni kabila ambapo museveni kawatosa kabisa, mganda mmoja ananiambia bora hayo mafuta yasingekuwepo kwa maana this is a civil war in waiting kama Museveni is not going to change his ways. Hilo ni wimbi la refugees ambalo tanzania not long would have to deal with if the politics of uganda doesnt change.

The same thing happens in africa siasa mbovu na viongozi wasiojua kulinda maslahi ya taifa. Chocolate is a very cheap luxury in the west kwa kuwa mkulima wa cocoa in Ghana can not even send his kids to school jinsi market inavyo mmbana. Sasa mpaka tutapojifunza kujitegemea umaskini wa africa si wa kuisha leo, na mpaka tutapowapa nafasi wasomi its all a joke.

Angalia just after loosing the election Gordon Brown went to uganda to lobby for that oil. Ingawa serikali aipo directly involved wala 'Labour' hawaundi serikali lakini alienda huko kwa kuwa the firm would pays british tax.

Na kama ulivyoona mzozo wa BP na America kumbe ugomvi wenyewe ni yule Mlibya alie achiwa sio kwa kuwa kaachiwa tu. Bali BP waliwa piku american firms kwenye deal ya mafuta ambayo wanadai serikali hili make a bargain hili 'BP' kupata hiyo contract, kumbuka ni kipindi kile under Bush 'Condoleeza' alienda Libya akajidai eti Libya inataka kubadilika ikubalike by international community now kama unavyowasikia tone yao wamarekani imebadilika about the country.

In short tusitegemee waafrica kubadilika leo wala kesho na amna kitakacho tendeka miaka mianane mmpaka nchi zetu zitapo ongozwa na watu wenye uwezo na elimu ya kuendesha taifa. Wawe watu walio watanzania kwanza kabla ya ukabila, sijui udini, au colour of their skins ni watanzania wenye interest ya Tanzania at heart first and they know what the're doing.

Its a world full of clever people outside our boundries. Even kenya is outwitting us itakuwa the global village ndio ujue tunajipa optimism ambayo hipo mbali na ukweli wenyewe, well niishie hapa nimwache m(w)od aje kuedit hii post.
 
This was a good one. Nimeeleezea siku za nyuma kuhusu huyu bwana nikashambuliwa sana hapa. Lakini ni huyu huyu. Gaddafi.
ni kweli kabisa watu wengi tu wenye mtindio wa ubongo humuona huyu kama mtu wa maana,
lakini ni jitu fulani lisilofaa kabisa hata kuwa lamaonesho kwenye banda
 
Juma Contena, baada ya kuangalia hii video ya kusikitisha unazo guts za kuendelea kusema kama signature yako isemavyo kuwa our beloved Mwalimu failed us miserably? SHAME on YOU nad The likes of YOU!:mad2::mad2::mad2::mad2::mad2::mad2::mad2::mad2:
 
Nimepata ghazabu sana kusikia maneno ya mmanga Gaddafi. Kesho nikikutana na mmanga popote pale lazima nimchape makofi. Ole wao.
 
Labda fidia iingizwe katika kila account ya Mtz binafsi vinginevyo hatuwezi faidi lolote na ufisadi huu!

Tungeuliza kwanza chenge ya Raddar iko wapi, tukipata majibu then tunaweza kuanza kudai fidia. Otherwise ni afadhari tusidai tutaumia zaidi na kuaibika zaidi.
 
He is not only ignorant but also a fool!

it seems that fools and ignorants are at least more honest than those who we have in power in our country today. NI kweli most of those who go to Europe(not all) are starving ignorants, otherwise they would have stayed. Kwa hapa Tanzania most of who go overseas are the best and the worst, but the best mostly return and become even better, wengine ambao ni worst wanabaki huko huko na kuvuruga systems za huko, wengine wanabadilika kuwa wezi. Actually some of us are happy because wanapunguza matatizo nyumbani, same kama unigereza walivyoamua kuexport wezi kwenye Australia na New zealand. Lakini on the other hand tunasikitika kwa wale best wanaoamua kukaa huko kutokana na uozo wa hapa nyumbani.
 
Br.Juma,

Tupo kwene same page. Nakubaliana na wewe kwamba Africa haitopata unafuu wowote tukiendelea kuwakumbatia viongozi wabovu who lack knowledge and zeal for the people of this continent. Ni kweli kama ulivyosema the mzungus will not change their approach to our resources kwa sababu kama nilivyokwisha kusema wanajua wakitupa nafasi tupumue tutakuwa competitors wao na hapo itawabidi wao na sisi tukae meza moja ktk equal terms..hicho kitu katu hawawezi kukikubali.

Sasa wanachofanya ni kuhakikisha uongozi mbovu unashamiri barani Afrika. Viongozi hawa wabovu mfano wa akina Abacha na CCM hawana utu wala regard to African people ndio maana wanaingia mikataba ya hovyohovyo na kuabudu wageni kwa kisingizio cha uwekezaji hata kama wanatumia pesa wavuja jasho kama mtaji! ni aibu kwa kweli. Viongozi hawa wa hovyohovyo katu hawawezi kuiendeleza Africa kupitia mageuzi ya kiviwanda na kibiashara..maana its either hawana knowledge au uchungu na Africa. Fikra zao hazizidi za mlo wao na watoto wao na vimada wao.
 
Lakini mbona viongizi wa ki-afrika kina Museveni na Rais wa zamani Thabo Mbeki wanamwona Ghadaffi kama msanii fulani. Nobodybtakes him seriously, so to speak.
 
kwani amekosea nini, we are ignorant and stupid people at least from the rule of simple majority!
 
hehehe sasa waafrica tumezidi mnataka ghadafi aache nchi yake itume kama uchochoro wa kuzamia! ofcoz those wazamiaji ni ignorants! kwani uongo!? na support kabisa! kwa nini watu wasitumie njia halali kuingia nchi nyingine badala yake mnatumia njia za panya! najuwa wabeba mabox waliotumia hizo njia mtaanza kuniponda ila ukweli ndio huo! "igorants" ama wapumbavu kwa kiswahili sahihi! fateni sheria:glasses-nerdy:
 
Back
Top Bottom