The Finest
JF-Expert Member
- Jul 14, 2010
- 21,605
- 6,097
Najiuliza War Crimes gani ambazo Gaddafi kafanya???
Huu unafiki wa akina Ocampo na washkaji zake unakera, unasikitisha na unatia hasira mnoooooooooo. Kimsingi Gaddafi kama kiongozi ana matatizo yake and so is Obama, Cameron, Sarkozy and there friends, Kwa hiyo nashindwa kuelewa walitarajia kitu gani walipoamua kumpiga mabomu. All in all huenda Gaddafi ana kesi ya kujibu lakini hivi ni kweli Crimes against humanity kafanya Gaddafi tu peke yake. Mbona hawajamshtaki Bush, Blair, yule bwana wa australia, na washirika wao kwa makosa kama hayo waliyofanya kule Iraq na Afghanistan. Halafu hivi hii mahakama ni kwa ajili ya viongozi wa Africa tuu!!!!!!!!!!!!! Yaani tunarudishwa kwenye UTUMWA MBAYA sana bila sisi wenyewe kujua na huku wengine tukishangilia. Huwa ninasema na leo ninasisitiza waafrika inabidi tusimame na kushughulikia matatizo yetu wenyewe, Inabidi ifikie mahali watu tukubali kulipa gharama ya mageuzi. Sio kukaa kunung'unika na kutegemea Ocampo aje kumuondoa Museveni and the like.
Nina hasira sana na ubeberu wa hawa jamaa.
I used to LOVE ICC lakini Moreno Ocampo is taking us in a wrong direction! Let his term end and we get a new Prosecutor (hopefully he/she will do a better job). This man has become a complete liability with lack of professionalism kabisa. I hope ICC supporters will have to sit down and do some soul-searching on the future of this important institution. Ocampo can indict all African tyrants, but he can be sure that without positive image of the Court among these Africans, the Court will achieve nothing. He is really kinda of patronizing the continent. I hate these dictators we have, but..Africa is bigger than personalities and this is what Ocampo and his European supporters miss. Why should he be controlled by western agendas? Well, let us wait and see the end game of Ocampo and Africa.
This would not be a problem if he was doing his job appropriately.The another problem with Mr Ocampo is his love to media. He sounds like a publicity secretary to ICC not as a chief prosecutor
Huu unafiki wa akina Ocampo na washkaji zake unakera, unasikitisha na unatia hasira mnoooooooooo. Kimsingi Gaddafi kama kiongozi ana matatizo yake and so is Obama, Cameron, Sarkozy and there friends, Kwa hiyo nashindwa kuelewa walitarajia kitu gani walipoamua kumpiga mabomu. All in all huenda Gaddafi ana kesi ya kujibu lakini hivi ni kweli Crimes against humanity kafanya Gaddafi tu peke yake. Mbona hawajamshtaki Bush, Blair, yule bwana wa australia, na washirika wao kwa makosa kama hayo waliyofanya kule Iraq na Afghanistan. Halafu hivi hii mahakama ni kwa ajili ya viongozi wa Africa tuu!!!!!!!!!!!!! Yaani tunarudishwa kwenye UTUMWA MBAYA sana bila sisi wenyewe kujua na huku wengine tukishangilia. Huwa ninasema na leo ninasisitiza waafrika inabidi tusimame na kushughulikia matatizo yetu wenyewe, Inabidi ifikie mahali watu tukubali kulipa gharama ya mageuzi. Sio kukaa kunung'unika na kutegemea Ocampo aje kumuondoa Museveni and the like.
Nina hasira sana na ubeberu wa hawa jamaa.
jana moreno ocampo ametangaza kuomba arrest warrant ya kumkamata gadafi na wanawe,gadafi anaua watu wake kwa kuwa yeye analinda madaraka yake,waasi wanaua askali wa gadafi kwa kuwa wao wanataka madaraka, je kumshitaki gadafi peke yake waasi ni watu gani au ni halali kuasi?
Hapo ndo unaona Double-Standards za dunia yetu. Ghadaffi anatolewa arrest warranty for crimes against humanity, lakini counterparts wa Syria na Bahrain au Yemen hao wala hata hawaongelewi licha ya kwamba uhalifu wao "against humanity" ni mbaya hata kuliko Ghadaffi. Bado jamaa wanampa makombora ya nguvu kutoka NATO, wanawatrain na kuwa-finance the so called liberators/ waasi. Je hao wa Yemen, Syria au Bahrain sio binadamu kwenye standards za Ocampo au ni kwa sababu West haina economic interests huko?
Mwenzio Gaddaffi, ana mawazo kama hayo, na misimamo yake iliikuwa wazi...! Wakubwa wa hii dunia hawakupenda kumuona anaelekea kwenye mafanikio na kutokuwa tegemezi, amekuwa ni hatari kwa maslahi yao na sasa ona kinachompata.Kuna tatizo kubwa zaidi la kimfumo na namna tunavyochukulia mambo kama waafrika. Wengi tumekaa tunasubiri wamarekani watuletee haki na maendeleo, ni kitu ambacho hakiwezi kutokea. Kifupi ni kwamba tukiendelea hivi hawa jamaa wataendelea kutuendesha kama gari bovu. Halafu mimi huwa nashindwa kuelewa ni kwanini tunalalamika sana, kwa sababu nachowapendea wamarekani, wala huwa hawafichi malengo yao. Wameshasema kuwa wao mahali popote pale duniani wanachoangalia ni maslahi yao tu.
Mimi nadhani ifike wakati tuache kulalama na tufikirie ni namna gani tutajikwamua kutoka kwenye minyororo ya ubeberu na utumwa unaoanza kurudi kwa kasi sana. Ni kweli kuwa Marekani ni taifa lenye nguvu lakini pia ni kweli kama unaamini uwepo wa M'mungu utakubaliana na mimi kuwa mungu hana upendeleo. Tukifanya kazi kwa bidii na mipango na kutambua nafasi yetu katika dunia hii, nina imani na hakika kuwa M'mungu atatufikisha kama alivyowafikisha wengine.
Jana Moreno Ocampo ametangaza kuomba arrest warrant ya kumkamata Gadafi na wanawe, Gadafi anaua watu wake kwa kuwa yeye analinda madaraka yake. Waasi wanaua askari wa Gadafi kwa kuwa wao wanataka madaraka, je kumshitaki Gadafi peke yake waasi ni watu gani au ni halali kuasi?
Double Standards at its best.
Kama ICC sio kanyaboya kwa nini USA haja-edorse mkataba kuikubali???
Imenigusa,
Yatia mashaka sana katika haya mambo ya international agreements na vyombo vyao kama NATO, EU, UN SECURITY COUNCIL etc, vipo wasmi kwa maslahi ya wamagharibi na si ktk kuwatendea haki viumbe wa dunia hii. Hawatendi haki kabisa, mnyonge mnyongeni lakini HAKI YAKE MPENI.
- Bahrain wameuliwa sana raia wakisaidiwa na vibaraka Saudia...Ocampo hakunena,
- Yemen yule rais pale kaua raia wengi lakini...ocampo hakunena,
- Bashar al-Assad anaendeleza vitu vyake pale Syria lakini...Ocampo haneni,
- Israel tawala zao zote zawaua na kuwakandamiza Palestinians lakini...ICC haipazi sauti,
- USA pale Afghanistan inazidi kuua raia na mara kadhaa (kwa bahati mbaya kuua raia na si Taliban) lakini hata baraza la usalama halipazi sauti.
- Ivory Coast Gbabo & Ouatara wameuua raia wengi ktk mbio zao za madaraka lakini...Ocampo hajatoa warranty kwao.