Gabon ni Nchi tajiri kwa rasimali, ni Nchi ya tano kwa wingi wa mafuta Afrika

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
Ameandika John heche,

Afrika ina viongozi wengi wajinga mno. Na matokeo ya ujinga huo unaambukizwa mpaka kwa Wananchi.

Gabon ni Nchi yenye kilometa za mraba 267,667 ina idadi ya watu milioni 2,349,000. Yaani hata mkoa wa Kagera una watu wengi kuliko wao. Gabon ni Nchi tajiri kwa rasimali ni Nchi ya tano kwa wingi wa mafuta Afrika, ina dhahabu, ina chuma, ina urani misitu na mbao.

Ina watu wachache tu, kwa wingi wa mafuta yanayochotwa pale Gabon Nchi hii ilipaswa iwe inawalipa Wananchi wakiwa nyumbani hata bila kufanya kazi lakini hii ni Nchi imejaa watu masikini, wengine walala njaa, matibabu majanga kama ilivyo sehemu kubwa ya Afrika.

Umeme mpaka leo wana megawatt 750, kumbuka urani yao inawasha umeme Ulaya wao wakiwa gizani. Mafuta Total ya Ufaransa inamiliki zaidi ya 61% familia ya Bongo 20%, Nchi 19% katikati ya utajiri huu vijana hawana ajira hawana matumaini.

Kwenye ardhi nzuri kama hii ambayo kuna mvua za kutosha wanaagiza mpaka nyanya na matunda kutoka nje. Hii Nchi na zingine nyingi Afrika zingekua na viongozi ingekua kimbilio la Waafrika wengi kwenda kutafuta maisha, lakini kila mara vijana wanakufa baharini wakijaribu kuzamia kwenda kutafuta maisha Ulaya.

Bob Marley kwenye wimbo wake wa Rat Race anasema “In the abundance of water, the fool is thirsty.” Katikati ya maji mengi mjinga ana kiu.Kuacha mshahara kitu gani? Wajinga watashangilia na kumuona Mzalendo!

Mshahara wa mtu mmoja utasaidia nini? Sisi tunataka ufanye kazi yetu vizuri simamia rasilimali zetu vizuri jilipe mshahara hata kama ni bilioni 10. Simamia rasimali za Nchi, Pitia mikataba iwe na manufaa kwa Umma, tengeneza kilimo kikubwa cha kisasa wape watu umeme, maji, Elimu, hospital bora, demokrasia dhibiti ufisadi na rushwa.

Kula mshahara mkubwa hakuna ataekuhoji kwasababu unaufanyia kazi. Hizi stunt za kutafuta umaarufu “populist” ni za madikteta tu. Viongozi wa Afrika wanawajua watu wetu, wanashughulika na tuvitu tudogo tudogo huku mambo makubwa ya kiangamiza watu.

Huu ni udanganyifu na uharifu.
View attachment 2787090
 
Back
Top Bottom