Gabon: Jeshi lamtangaza Jen. Nguema kuwa Rais wa Mpito, alikuwa Kiongozi wa Kikosi cha Ulinzi wa Rais

Victoire

JF-Expert Member
Jul 4, 2008
24,148
56,611
1693425792844.png

Haya kumekucha Gabon, Brice ambae ndo alikuwa mkuu wa ulinzi wa Rais ndo kawa Rais.

Kwa uchunguzi wangu ,huyu Nguema ni binamu wa Ali Bongo. Na Ali Bongo alimpa kazi maalum ya kumuandaa mtoto wa kwanza wa Ali Bongo anaeitwa Valentin ili aje kuwa Rais.

Naona Brice kaamua, no way kwanini aandae mto wakati yeye mwenyewe Général anaweza?

Pia Soma:
-
Gabon: Jeshi limechukua madaraka baada ya Ali Bongo kutangazwa mshindi wa Urais

==========

The leaders of the coup in Gabon on Wednesday named Republican Guard chief General Brice Oligui Nguema transitional president, according to a TV statement, after the military seized control in the wake of elections.

“General Oligui Nguema Brice was unanimously appointed chairman of the Committee for the Transition and Restoration of Institutions, chairman of the transition,” declared an officer in the presence of dozens of senior officers, according to the press release read out on Gabon 24.
 
Wanajeshi saba wamefanya mapinduzi huko gaboni sisi sijui tunakwama wapi

Mimi naamini kikosi kimoja tu nchi hii kikitangaza kufanya mapinduzi hakuna mwanajeshi atayeendelea kulinda utawala huu
Kufanya mapinduzi si machezo,hao wanajeshi wamefanikiwa sababu mkuu wa ulinzi wa Rais ndo alikuwa nyuma ya haya mapinduzi. Na yeye ndo kawa Rais wa mpito kwa kumpindua binamu yake.
Kumbuka pia mkuu wa Ulinzi wa zamani Frédéric Omar Bongo ni mdogo wa Ali Bongo wakichangia Baba.
Ali Bongo alimuondoa mdogo wake kwenye hiyo nafasi ndo akamuweka huyu binamu yake ambae nae ndo leo kamsaliti.
 
Haya kumekucha Gabon,Brice ambae ndo alikuwa mkuu wa ulinzi.wa Rais ndo kawa Rais.

Kwa uchunguzi wangu ,huyu Nguema ni binamu wa Ali Bongo. Na Ali Bongo alimpa kazi maalum ya kumuandaa mtoto wa kwanza wa Ali Bongo anaeitwa Valentin ili aje kuwa Rais.

Naona Brice kaamua, no way kwanini aandae mto wakati yeye mwenyewe Général anaweza?View attachment 2733956
Naona babu kampindua kibabu

Kwa jamii ya intelejensia fahamu hapo kuwa haya mapinduzi yamefanyika kama.kakati wakuinasa Niger.

Nimeshaanza kunusa uvundo hapo
 
Haya kumekucha Gabon,Brice ambae ndo alikuwa mkuu wa ulinzi.wa Rais ndo kawa Rais.

Kwa uchunguzi wangu ,huyu Nguema ni binamu wa Ali Bongo. Na Ali Bongo alimpa kazi maalum ya kumuandaa mtoto wa kwanza wa Ali Bongo anaeitwa Valentin ili aje kuwa Rais.

Naona Brice kaamua, no way kwanini aandae mto wakati yeye mwenyewe Général anaweza?View attachment 2733956
Zaidi ya jukumu lake la kijeshi, ubia wa Nguema ulijumuisha misheni ya kidiplomasia nchini Morocco na Senegal. Alijulikana pia kwa moyo wake wa ujasiriamali na aliripotiwa kujilimbikizia mali nyingi, na kumfanya kuwa milionea ndani ya duru za Gabon. Uchunguzi wa The Organised Crime and Corruption Reporting Project (OCCRP) ulifichua uwekezaji wa Nguema katika mali isiyohamishika huko Marekani, hasa kununua majengo kwa malipo makubwa ya pesa taslimu.
 
Kina kipindifkani akiwa katika mahojiano na gazeti la kila siku la Ufaransa la Le Monde mwaka 2023, Nguema alionyesha kutoridhika na utawala wa Rais Bongo. Alikosoa ukiukwaji wa katiba ulioruhusu Bongo kuwania muhula wa tatu na kusisitiza uamuzi wa jeshi kuwajibika kwa hali hiyo. Nguema alipendekeza kuwa Bongo inafaa kustaafu, kuruhusu nchi kusonga mbele chini ya uongozi mpya.
 
Kuna vituko hatari,huyu Rais wa mpito kuna kipindi alinunua majumba huko Maryland USA ya mabilioni. Any way raia wanafurahia tu jina Bongo kuondoka. Ila huyu nae ni binamu wa Ali ambae kaamua kumsaliti binamu yake.
Mkuu ni kazy kweli kweli, afrika kuna ujinga mkubwa sana mtu anafanya lavish spending huku wananchi wanaona ni bora yeye kuliko aliyepita kumbe wote ni The same.
 
Kuna vituko hatari,huyu Rais wa mpito kuna kipindi alinunua majumba huko Maryland USA ya mabilioni. Any way raia wanafurahia tu jina Bongo kuondoka. Ila huyu nae ni binamu wa Ali ambae kaamua kumsaliti binamu yake.
Nilitaka kushangaa kwamba familia ya Bongo ikae madarakani miaka mingi halafu iwe haijaweka ukoo wao madarakani!? Ile Gabon ni mali ya ukoo wa Bongo, hakuna jipya

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Kuna vituko hatari,huyu Rais wa mpito kuna kipindi alinunua majumba huko Maryland USA ya mabilioni. Any way raia wanafurahia tu jina Bongo kuondoka. Ila huyu nae ni binamu wa Ali ambae kaamua kumsaliti binamu yake.
Naye atapinduliwa Kama bwana Danube alivyopinduliwa na Ibrahim traore wakiona nae anafanya upumbavu Ni suala la muda tu ,au we Ni chawa wa Ali bongo😁
 
Back
Top Bottom