Utajiri wa Jenerali Nguema aliyempindua binamu yake Ali Bongo. Wajinga ndio waliwao

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,114
49,840
Huyu ndio wale vijana maskini walikuwa wanashangilia eti ni Mzalendo kampindua binamu yake 🤣🤣🤣🤣

"Gabon's new Head of State, Brice Nguema is a cousin of former President Ali Bongo. He owns three homes in USA worth over $1 million according to OCCRP. Gabon's opposition leader, Albert Ondo Ossa says the coup is a family affair aimed at keeping the Bongo Family in power."

Screenshot 2023-09-03 144338.png


My Take
Masikini mtaendelea kutumiwa na hao Wanasiasa hadi mkome, hakuna Mwanasiasa anakupigania maisha yako.
 
ndomana ndgu zetu na zile VXR huwaambii kitu. Sema kuna raha jani yale maisha daaah......shida inakuja mambo yakigeuka, utaelewa kwanini uswizi sio chimbo tena....tumehamaa
 
Huyu ndio wale vijana maskini walikuwa wanashangilia eti ni Mzalendo kampindua binamu yake 🤣🤣🤣🤣

"Gabon's new Head of State, Brice Nguema is a cousin of former President Ali Bongo. He owns three homes in USA worth over $1 million according to OCCRP. Gabon's opposition leader, Albert Ondo Ossa says the coup is a family affair aimed at keeping the Bongo Family in power."

View attachment 2737580

My Take
Masikini mtaendelea kutumiwa na hao Wanasiasa hadi mkome, hakuna Mwanasiasa anakupigania maisha yako.
hiyo ni hela ndogo sana kwa mtu aliyekuwa karibu na utawala, ni ya kawaida. nyumba ya 1m usd? hao kina manji huko canada na marekani wanamiliki hizo nyingi tu. wangeniambia ana utajiri wa over 1b usd, ningeshtuka.
 
Vijana endeleeni kuwa Wazalendo wakati wenzenu wanavuna

Kuna watu wa aina mbili kwny jamii za watu linapokuja swala la rasilimali za nchi.

Kuna wale ambao hujali matumbo yao na familia zao tu. Na watu wa aina hii, na wapambe wao hawafikirii kesho ya wajukuu zao ama watoto wa wajukuu wao. Na ikiwa wao ni viongozi ama wapo karibu na viongozi, mara nyingi nafasi hizo hutokana na kupewa fadhila kwa kubebwa na mfumo au waliotokana na mfumo. Watu wa aina hii hawafai na hawakufaa kuwa viongozi ama karibu na uongozi...
Kwa watu wa aina hii, huwaza kujilimbikizia wao, na huabudu uongozi kwakua yy mapato yake ni kubebwa na huo uongozi.

Kundi la pili ni lile ambalo huamini mali na rasilimali za taifa ni kwa manufaa ya wote hadi watoto vilembwe vijavyo. Hueshimu haki ya kila mtu na usawa katika mapato yatokanayo na keki ya taifa. Kundi hili la pili huchukiwa na kundi la kwanza, utetezi wao kwa mali na rasilimali za taifa huonekana kama uadui wa kuwaonea wivu kundi la kwanza linapopora mali za wote kwa manufaa ya wote. Kundi hili la pili ndiyo lile lenye viongozi mashujaa wa Africa, kama akina Nyrere na wengine, maana wao wangekuwa kama lile kundi la kwanza hii leo tunapoongea kutumiwa kwa vijana, kila kitu wangekuwa wameshakiuza wao kwa manufaa ya wao na familia zao.

Viongozi wengi wa Africa hata wakistaafu, bado nchi huendelea kuwatunza wao na familia zao hadi mwisho wao, unajiuliza pamoja na kubebwa hivi na nchi, roho ya kujilimbikizia na kupora mali za wananchi wanaipata wapi?
 
Bora huyo wa nyumba tatu......baba ake ali bongo nyumba 35 ufaransa........account 17 za banki ........ferrari 6 na bugatti moja..........nini nyumba tatu
 
Huwa sihangaiki na siasa uchwara Wala siwezi kuwa mgongo wao,nakomaa on my own.

Ukiniona kweysiasa ujue ni maslahi ya gu ila ukae ukijua hakuna anaekupigania wewe.


unajua ulicho andika??? siasa huwezi ikwepa kwanza ulicho andika ni siasa au ni udaku?

nyumba ya 2 bil+ ni hela ya kawaida mkuu wengi hasa watanzania wananazo tena kwa nje ya nchi hiyoo ni nyumba ya kawaida sana.
 
Hayo ni mapinduzi ya ngozi nyeusi,😄😄😄

Jamaa anataka na yeye awe na mke mzungu 😄😄

Unacheza na pesa wewe...
 

Attachments

  • Screenshot_20230830-173630_1.jpg
    Screenshot_20230830-173630_1.jpg
    55 KB · Views: 3
Back
Top Bottom