G.Lema: Tulaani sote tukio la Polisi kuuawa

Godbless J Lema

Arusha MP
Sep 28, 2013
92
2,205
Tukio la kuuwawa askari wa Jeshi la Polisi linapaswa kulaaniwa kwa nguvu zote na kila Raia wa Taifa letu , hii ni dalili mbaya sana kwa ustawi wa amani ya Taifa letu . Hata hivyo ninamuomba Mungu awatie nguvu , ndugu , rafiki na familia zote za marehemu waliofikwa na msiba huu mbaya sana na mzito .

Polisi wameuwawa wakiwa kwenye wajibu wao wa kulinda raia na mali zao ni muhimu sasa kwa vyombo vya usalama kuwatia nguvuni na kuthibiti kwa weledi matendo kama haya yanayoendelea kushamiri kwa kasi sana , ni muhimu pia idara za ulinzi na usalama kufanya utafiti wa kina kujua ni nini haswa sababu za matukio kama haya.

Hatuwezi kuishi kwa amani bila ya kuwa na Jeshi la Polisi imara na ili tuwe na Jeshi la Polisi imara , tunapsawa kuwa na jamii inayotoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi haswa kwenye nyakati ngumu kama hizi , hivyo ni matumaini yangu kuwa Wananchi wote hususani wa maeneo hayo yalipotokea mauaji watakuwa tiyari kutoa ushirikiano ili kuwabaini wahusika wa tukio hili baya.

Godbless Lema ( MB)
Waziri Kivuli Mambo ya Ndani.
 
Umenena vyema sana kamanda kuwa suala la kuuawa kwa askari wetu huko Mkuranga ni jambo linalopaswa kulaaniwa na kila mwananchi wa nchi hii....

Hata hivyo hiyo pia iwe Meseji hususani kwa watawala wetu na wabunge wengi wa CCM ambao kwenye kikao kinachoendelea cha Bunge, waligoma Bunge liahirishe shughuli zake na kujadili hali tete ya usalama wa nchi kwa hivi sasa na badala yake wakadai hilo jambo halina umuhimu wa kiasi hicho kufanya Bunge ilijadili katika hali ya dharura.

Hata hivyo sitawashangaa wabunge hao hao wa CCM siku ya jumanne ijayo, wakaahirisha shughuli zote za Bunge na kulijadili suala hilo la mauaji wa Polisi!

Kumbe mkuki mzuri kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu!?
 
Pole kwa wafiwa,ila hii ni nchi ya Isidingo,bandika bandua so saa nyingine mambo yanakuwa location ili kuhamisha mijadala,next week bunge halitazizima tena na utekaji na hii ni 'njia' zaidi kuonyesha huko mtaani sio raia tu wanadhuliwa na TISIIII kuwa nchi hii ina magaidi!!

Cha ajabu wale masheikh wa UAMSHO waliokamatwa kwa kesi za ugaidi hadi leo miaka mitano almost uchunguzi unaendelea tu!!
 
Tukio la kuuwawa askari wa Jeshi la Polisi linapaswa kulaaniwa kwa nguvu zote na kila Raia wa Taifa letu , hii ni dalili mbaya sana kwa ustawi wa amani ya Taifa letu . Hata hivyo ninamuomba Mungu awatie nguvu , ndugu , rafiki na familia zote za marehemu waliofikwa na msiba huu mbaya sana na mzito .

Polisi wameuwawa wakiwa kwenye wajibu wao wa kulinda raia na mali zao ni muhimu sasa kwa vyombo vya usalama kuwatia nguvuni na kuthibiti kwa weledi matendo kama haya yanayoendelea kushamiri kwa kasi sana , ni muhimu pia idara za ulinzi na usalama kufanya utafiti wa kina kujua ni nini haswa sababu za matukio kama haya.

Hatuwezi kuishi kwa amani bila ya kuwa na Jeshi la Polisi imara na ili tuwe na Jeshi la Polisi imara , tunapsawa kuwa na jamii inayotoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi haswa kwenye nyakati ngumu kama hizi , hivyo ni matumaini yangu kuwa Wananchi wote hususani wa maeneo hayo yalipotokea mauaji watakuwa tiyari kutoa ushirikiano ili kuwabaini wahusika wa tukio hili baya.

Godbless Lema ( MB)
Waziri Kivuli Mambo ya Ndani.
Mh Lema naungana na wewe katika kulaani vikali Hili tukio, waliouliwa walikuwa katika kutekeleza wajibu wao ambao ni kulinda raia na Mali zao.Na Kama tulivyolaani wabunge, wasanii, ma doctors na wafanyabiashara kuingiliwa au kuzuiwa kutekeleza majukumu Yao ya kila siku Ndio tunavyolaani Hili tukio, Hili tukio halijazuia tu Askari wetu kutekeleza wajibu wao , tukio Hili limewachukulia haki yao kubwa ya msingi ambayo ni kuishi

.lakini kuhusu suala la wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vyetu vya ulinzi nadhani itakuwa haiwezekani , mh RAIS alisema anataka jeshi la polisi liogopwe sasa raia wa kawaida ataanzaje kwenda kutoa ushirikiano kwa mtu (taasisi) ambayo anatakiwa kuigopa?!

Lakini Nataka nikutoe hofu ukiwa Kama waziri wa mambo ya ndani kuwa Kama ambavyo walipatikana wakina Roma baada ya kutekwa Na majambazi/magaidi yasiyojulika basi Na hawa majambazi/magaidi yasiyojulikana na vyombo vya ulinzi ambayo yameua Askari wetu yatapatikana kabla ya JUMAPILI.formula iliyotumika kwa kuhakikisha wakina Roma wanaachiwa Na majambazi yasiyojulikana Ndio itakayotumika kuwakamata au kuwaua hawa .
 
Kwa masikitiko makubwa nalaani kwa nguvu zote ukatili huu wa kuuawa kwa polisi wetu,kwa hili tuamke sote tushirikiane raia wema na majeshi yetu sote tuwasake wauaji hawa na silaha zote walizochukua turudishe kwenye mikono salama kwani wakibaki nazo sote hatutakuwa salama siku za usoni r.i.p vijana wetu.
 
Back
Top Bottom