Fuzzy Mathau Bad Audit: CAG Report

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
4,536
Points
2,000

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
4,536 2,000
Najiuliza ni kiasi gani Spika na maamuzi ya kumsulubu CAG kwa wiki mbili na kulifanya jambo la kujaza kurasa za magazeti kuongelea kauli ya CAG na matumizi ya neno dhaifu..... na sasa ripoti inaonyesha uozo uliokithiri na kukubuhu... Wananchi wanapokeaje hii ripoti ya CAG ambaye waliambiwa ni mtovu wa adabu?
 

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,491
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,491 2,000
Katika mchezo wa soka kuna kujifunga ''own goal''. Katika tennis kuna 'unforced error'' kwamba mchezaji anafanya makosa bila shinikizo la mpinzani wake. Halafu kuna goli la mkono la Nape

Unforced error inatokana na udhaifu wa mchezaji kujipanga kukabiliana na mashambulizi
Own goal hutokea kwa nia njema, kwamba, lengo ni kuokoa mwisho wake ni kujifunga
Goli la mkono ni kulazimisha kufunga kwa njia za haramu

Bunge lilitaka goli la mkono,kwamba, kumsusia CAG kwa neno dhaifu kungemlazimisha ajiuzulu
CAG Prof Assad akaling'amua hilo, hakujiuzulu
Bunge likifanya unforced error kwa kutafuta 'kiroja' na kukifanya hoja. Hakuna aliyeshinikiza hilo

Taarifa ya CAG ipo hadharani na kuondoa shaka juu ya kauli yake. Bunge limeithibitisha kauli hiyo kwa mtindo wa ''own goal''. Nia ya Bunge ilikuwa ''njema' CAG aondoke. Wamejifunga
 

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,491
Points
2,000

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,491 2,000
Mkuu Rev

Taarifa ya Spika kumkagua CAG inamweka yeye na serikali mahali pagumu mbele ya umma
Baada ya kushindwa kumtimua, sasa imesukwa mbinu ili kumweka kwenye kona kwa ukaguzi

Spika anasema taarifa ya Kampuni ya Mangesho aliyopitia inaonyesha kuna ''issue'' na ameitaka kamati ya PAC kuipitia na kumpa taarifa ya issue.
Hapa maana yake tayari kuna kitu alicholenga

Ingawa Spika amelivalia njuga hili jambo, lakini pia linaiweka serikali katika wakati usiohitajika

Hili jambo litaigawa sana jamii. Si suala rahisi ni la kuangalia kwa umakini na uyakinifu

Kuna maneno mazito yanayohusisha hadi mambo mazito ya kijamii na kwamba CAG ni victim tu

Hivi kwanini Spika anawapa hoja wale walio na hoja wanaosubiri uthibitisho?
Serikali yote itaangaliwa kwa jicho ambao huenda likazua mengi zaidi

Anachofanya spika ni kutaka kujifunga goli lingine lakini pia ataiweka serikali katika tatizo kubwa kijamii. Tatizo hilo linaiweza kuigawa nchi!

Hili jambo ni zito siyo rahisi na kama ni rahisi wapite huku vijiweni na mitaani wasikie hoja
 

Forum statistics

Threads 1,390,211
Members 528,114
Posts 34,046,065
Top