Futari ya ndizi malindi na nyama ya ng’ombe

Futari ya ndizi malindi na nyama ya ng’ombe

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,073
Reaction score
34,844


Recipe/Pishi la Raphia Hussein


Mahitaji


  • Ndizi Malindi 5
  • Nyama ya Ng'ombe½ kilo
  • Vitunguu maji 2
  • Vitunguu saumu kijiko 1 cha chai
  • Nyanya 3
  • Binzari ½ kijiko cha chai
  • Chumvi kwa kiasi chako
  • Hoho 1
  • Karoti 2
  • Tui la nazi vikombe 2
  • Mafuta ya kula kiasi kidogo

Njia

1.shachemsha ndizi kuondoa ubichi mwaga maji weka pembeni.

2.kaanga vitungu maji adi viianza kuwa brown, ongeza vitunguu saumu, kisha nyanya na nyama. acha ichemke maji ya nyanya yakikaribia kukauka weka binzari kidogo ,chumvi,hoho. karoti na ndizi ulizochemsha , koroga na kaanga pamoja ili viungo vishikane na ndizi.


3.Weka tui jingi kiasi acha zichemke hadi ziive vizuri,Epua ndizi jikoni zikiwa na mchuzi (tui) mwingi,zisikauke sana kwani jinsi inavozidi kukaa mchuzi unaganda


4.Mpaka hapo Futari tayari
 
Hapo ukitumia utumbo utamu wake balaa ila ukiupika harufu yangu ndio yanikera

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom