Fursa zipi wanazopata madereva wa mabosi?

scatter

JF-Expert Member
Feb 15, 2013
1,565
2,000
Fani ya udereva wa magari imetoa ajira kwa wazee na vijana katika nchi yetu.

Katika kazi hii kuna changamoto mbalimbali wanazopitia ikiwemo kusafiri umbali mrefu.

Kuna mkasa mmoja jamaa alikuwa dereva wa bosi mmoja masharti ya yule bosi lazima dereva awe analala ndani ya gari na pia alimlazimisha awe na itikadi kama zake za kulewa na kurudi usiku wa manane.

Wakuu mikasa wanayopitia madereva ni mingi hebu tushare mikasa hiyo tuweze kujifunza kupitia hapa.
 

Mr. MTUI

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
7,893
2,000
Hapo labda magunia ya mkaa na vyakula vya Bei rahisi Kama nyanya, ndizi, matunda, kuku n.k
 

Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
47,655
2,000
Kuna jamaa mmoja ni dereva wa mkurugenzi taasisi moja ipo chini ya wizara ya fedha.

Yule jamaa alikuwa anasafiri kiasi kwamba alifanikiwa kujenga nyumba kama 4 za kupangisha hapahapa dar.

Madereva wa mabosi wana fursa nzuri sana kama wana akili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom