Fursa za uwekezaji nchi ya Tanzani

MWANALUGALI

JF-Expert Member
Feb 1, 2010
601
34
Makampuni ya Kenya yamechangamkia sana fursa za ushirikianao wa afrika ya mashariki, sasa Arusha imekuwa ni eneo maalum kwa uwekezaji kwa wakenya, lakini Tanzania hakuna tulalofanya labda nielimishwe hapa JF.

Kwa nini Shirika la bandari lisifungue ofisi zake huko Kigali, Kampala, Bujumbura, Lubumbashi, Lusaka na Lilongwe? kwa nini wasifuate biashara huko huko na kuwafanya waagizaji wa nchi hizo kutumia bandari ya dar es salaam? Wenzao wa KPA wanazo ofisi kampala na Kigali na wanajitahidi sana Bandari ya nchi kavu ya Isaka ifungwe. Sijui kinachotokea kwa watanzania , utafikiri tumelogwa. hatuko aggressive as a country kuhakikisha fursa zozote zinazo jitokeza tunazichangamkia.

Hivi sasa Rwanda wanajitahidi ICTR ihamishiwe kwao, Kenya waliisha wahi kusema kuwa wanataka makao Makuu ya Jumuiya yapelekwe Nairobi kutoka Arusha. Kuna kila jitihada ya wenzetu kupigania kila kitu ili uchumi wao uimarishwe au mambo ya kijamii ya nchi zao yapate ahuweni.

Jamani tuchangamke, CRDB waende Rwanda, Burundi na DRC kufungua Matawi, wafanye biashara na hawa watu wanaotegemea nchi yetu, Mengi aimarishe Channel 5, TRL na ATC yafufuliwa na kuweka macho yao huko. Jamani tuwafumbue macho hawa watanzania wenzetu watumie fursa zilizoko
 
Back
Top Bottom