Fursa za kazi za Ujenzi, Pwani Tanzania

Abdul Ghafur

JF-Expert Member
Sep 18, 2017
610
733
Fursa fursa fursa za kazi.
Alhamdulillah hapa Abraar Complex Kuna fursa kadhaa za kazi zimejitokeza.
Tunahitaji:
1) Mafundi ujenzi (waashi) wazoefu.
2) wasimamizi wa ujenzi (site foreman).
3) Mafundi seremala wazoefu.
4) Mafundi bomba wazoefu.
5) Fundi welder.
6) Wahasibu wasaidizi.
7) Wasaidizi na au wanafunzi Kwa vitendo wa fani zote hizo.
Kazi hizo zote zipo Misugusugu, Kibaha, Mkoa wa Pwani. Mtaa wa Vitendo. Anaehitaji fursa hizo akubali kuhamia karibu na kituo cha kazi, mafunzo, atachopangiwa.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Abdul Ghafur 0625249605.
 
Aliyetufikisha huku sijui anastahili adhabu gani...
Nimeshangaa sana kuona hii, kama unatoa msaada toa msaada tu bila kutegemea chochote na kama huna uwezo wa kutoa kaa utulie sio dhambi maana Mungu pia anaona huna

Sio utumie maskin kama mtaji!
 
Mimi niko mkoa wa mbali natamani kuja kwan inahitajika nini na nini? Halafu nikija kama kesho kazi zipo au nasikilizia
 
Fursa fursa fursa za kazi.
Alhamdulillah hapa Abraar Complex Kuna fursa kadhaa za kazi zimejitokeza.
Tunahitaji:
1) Mafundi ujenzi (waashi) wazoefu.
2) wasimamizi wa ujenzi (site foreman).
3) Mafundi seremala wazoefu.
4) Mafundi bomba wazoefu.
5) Fundi welder.
6) Wahasibu wasaidizi.
7) Wasaidizi na au wanafunzi Kwa vitendo wa fani zote hizo.
Kazi hizo zote zipo Misugusugu, Kibaha, Mkoa wa Pwani. Mtaa wa Vitendo. Anaehitaji fursa hizo akubali kuhamia karibu na kituo cha kazi, mafunzo, atachopangiwa.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Abdul Ghafur 0625249605.
Kazi ya ajira au deiwaka tu malipo kila siku au mwisho wa wiki tangazo liweke vizuri ili kusiwe na maswali mengi.
 
Mungu akubariki sana kwa kutoa fursa kwa watu mbalimbali.

Nina swali kuhusu chakula mtu anayekaa hapo, mnampa chakula au anajinunulia yeye?

Vipi kuhusu malazi kwa watu wanaotoka mbalimbali na uwezo wa kupanga hawana?

Pia kwa mwanafunzi wa vitendo malipo yake yanafika laki 2 kwa mwezi?

Baada ya miezi sita au mwaka huwa mnatoa vyeti kwa wahitimu?
 
Amiin na ahsente sana kwa dua njema kabisa. Atubariki sote kwa kila jema tufanyalo, natumai mema zaidi ni ya kutumikia binaadam wentezu kwa nguvu zetu zote na uwezo wetu wote bila ya kutegemea malipo. Amiin.

Kuhusu chakula, hivi sasa tunatoa posho ya kula kwa kila siku kwa wanaochukua mafunzo hapa. Wapo kina mama nao wanajipatia riziki zao kwa kuwauzia chakula kwa bei nafuu na kizuri, pia kuna wengine wameamua wajipikie wenyewe. Yote yanawezekana na In Shaa Allah tunahakikisha mtu anatosheka kwa milo mitatu ya kila siku. In shaa Allah hivi karibuni tuna mpango wa kuanzisha darasa la mapishi, tumeshaanza kuongea na wahitimu wa hotel management wa VETA tunatazama jinsi tunavyowezza kushirikiana nao kuanzishi darala la mapishi na kazi za "hospitality" kwa vitendo.

Wanafunzi wa vitendo hawalipi kitu bali wao wanalipwa. Mafunzo yetu yametayarishwa kia aina ya kipekee, mwanafunzi anajifuna aina moja ya kazi kwa siku mbili tu ikizidi hapo anakua ni saidia fundi na analipwa kama saidia fundi, magundi anaosaidia wakiona kishapata uzoefu na anapowezwa kuachiwa kazi akaifanya mwenyewe kwa siku tatu bila kusimamiwa, Mwalimu akiikagua akaiona ipo afi na imezingatia ubora na miiko ya ufundi bai kwa kazi hiyo anakuwa amekwiha fuzu. Akipewa kazi hiyo tena inakuwa aidha kuwafundiha wenzake (Mwaalimu) au fundi wa kulipwa kama funzi.

Hapa kwetu tuna mpango wa kipekee, haujawahi kufanywa na chuo chochote Tanzania. Tunmpa aliefuzu zaidi ya cheti, tunamdhamini kazi zake popote atapoenda kuzifanya Tanzania.

Wasialana nami kwa maelezo zaidi 0625249605. Abdul Ghafur.
Safi sana. Kwa upande wako unapambana sana kutoa ujuzi kwa vijana.
Natamani na watu wengi zaidi wajitokeze kutoa msaada kama huu.
 
Unalosema linawezekana na tupo tayari kushirikiana kupeana Uzoefu tunaoupata na yeyote yule, pia tunatamani sana proffessionals wa kazi na shughuli mbali mbali iwe sheria, uhasibu, utawala, biashara, ujasiriamali, siasa na ufundi wa kila aina wajitokeze tubadilishane mawazo kwa kuitumikia jamii.


Kwa dini yeyote ile, kuitumikia jamii ni kumtumikia Mwenyezi Mungu.

Yeyote mwenye lake lolote liwe ushauri, maswali, kutoa ujuzi, kutafuta ujuzi, awasiliane nami kwa whatsapp au simu kwa namba 0625249605


Kwa sasa tuna uhitaji wa mtu wa utawala anaeweza kufanya kazi za human resorces kwa ufanisi, bila kusimamiwa.
Habari mkuu

Kwa upande wa mtu wa utawala mnahitaji alosomea mambo hayo au yoyote tu wenye elimu tofauti anaweza kufanya?
 
Back
Top Bottom