Mbeya rice 2300-2600Hivi bei ya mchele kwa Zenji ni kiasi gani kwa kilo...?
Makadirio.
Wako kwa Shilawadu na Kimambi .Fully trapped by " Instagram syndrome " .Following and liking Bullshit craps all day long .Hiv kwann watu hawachangii mada nzur ka hii
Matikiti zenji yamezagaa, wanauza kwenye Virukuu, moja 1000 tuInaonyesha unaijua vizuri zenji wewe nataka niwe naleta matikti yangu huko mzee yapi yanasogea?
thanks ila tunasafari ndefuKuna wakati nilikuwa z'bar nikaenda kwenye hoteli moja ya kitalii, nilikuta watu wakishusha mizigo kwenye gari moja kubwa hapo hotelini, moja ya mizigo hiyo ilikuwa ni mayai na vinywaji vikali (mvinyo).
Nilijaribu kumdadisi mhudumu mmoja pale akaniambia vitu vile vinatoka nje ya nchi, nikashangaa sana, yani hata mayai ya kisasa wanaagiza toka nje ya nchi?
Nilipodadisi zaidi niligundua 90% ya bidhaa zinazotumiwa pale hotelini zinatoka nje ya nchi, sio kwamba hapa tz hazipo hapana! ni kwasababu wabongo wengi ni 'wababaishaji' yan kama amepewa tenda ya mayai 1000 kila wiki, basi atapeleka kwa wiki mbili then wiki ya tatu atakuwa ameishiwa au ataanza kusuasua, hii ndio shida(commitment).
Ukweli ni kwamba kuna fursa za biashara ni nyingi kwenye mahoteli makubwa z'bar wanahitaji bidhaa nyingi mfano vinywaji, matunda,nyama,mayai,
mbogamboga tena kwa bei nzuri sana ila wanahitaji watu committed mf;kuna jamaa alikuwa anawauzia nyama ya
'mbuzi katoliki' sh 17,000@kg
Pia kipindi cha Ramadhan watu wanopeleka nyama ya Kuku,mbuzi ng'ombe wanapiga sana pesa(hii sio hotelini hata mtaani tu).
Tatizo watz tumelala
mpaka toothpick zinaingizwa kutoka nje, hii ni aibu!!
Magogo yanazalishwa Iringa mpaka yanasafirishwa nje tunashindwaje kutafuta/kuagiza mashine ya kutengeneza toothpick? tuamke tuchangamkie fursa wakuu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Vipi kuusu viazi vitamu zenji ?Mambo mengine au ukitaka kujua fursa za kibiashara Zenji muwe mnauliza wenyeji msiende kichwa ngumu na kufanya Survey zenu pekee na kujiridhisha tu, ohoo mtakuja kupoteza mitaji yenu na kujutia baadae
Viazi vitamu zenji vinalimwa. Cha kupeleka Zenji kibiashara ni viazi mviringo, mchele, mafuta ya alizeti, ufuta, karanga.Vipi kuusu viazi vitamu zenji ?
Kuna tatizo pia kuhusu elimu ya jinsi ya kuanza biashara. Masoko ya mitaji, mifumo ya kodi, changamoto sokoni. Mfano: wanaotoa elimu kuhusu fursa za kilimo Hakuna anayezungumzia changamoto kubwa Kwa mkulima mwenye mtaji mdogo: source of sustainable labour(wafanyakazi WA uhakika) mifumo ya masoko yetu(changamoto za madalali na ushuru usioangalia Hali ya soko) na kadhalika. Hivyo basi na Huku watu waelimishwe. Watu wanaogopa changamoto za kuanguka kimitaji pia.Hawataki fursa,
Wanataka kumjadili wema katengeneza sha au laa,
Wana-interviews zao kule na muosha rungu,
Mapenzi ndio mijadal yai( sio mbaya mapenzi yana run dunia),
Wameajiriwa yes hawataki kabisa kwenda nje ya box(in kingwangala articles),
Wanajadili makinikia kwanza mkuu jana si umesikia tumelipwa Au hujui
Mijadala ya kuhegedana ndo tunaipenda mkuu
Tatizo kodi..yaani jinsi ya kupitisha mzigo kuupeleka mpaka zanzbr...TRAThread ambayo haina kichwa cha habari chenye haya maneno huwezi kupata wachangiaji
-Mbowe kufanya press
-Magufuli atumbua
-Dawa ya kuongeza nguvu za kiume kwa bei chee
-Njia ya kuacha punyeto
-Makonda
-Ccm kuhonga madiwana wa Chadema
-Natafuta jimama
etc....
Yaani shida tupu.... Zanzibar wana uhitaji mkubwa sana wa Nyanya na wale wanao lima Mpunga kipindi cha sikuku na kipindi cha kawaida kuna uhitaji wa Mchele