Fursa za biashara Zanzibar

Zillion

JF-Expert Member
May 15, 2017
1,358
1,807
Kuna wakati nilikuwa z'bar nikaenda kwenye hoteli moja ya kitalii, nilikuta watu wakishusha mizigo kwenye gari moja kubwa hapo hotelini, moja ya mizigo hiyo ilikuwa ni mayai na vinywaji vikali (mvinyo).
Nilijaribu kumdadisi mhudumu mmoja pale akaniambia vitu vile vinatoka nje ya nchi, nikashangaa sana, yani hata mayai ya kisasa wanaagiza toka nje ya nchi?
Nilipodadisi zaidi niligundua 90% ya bidhaa zinazotumiwa pale hotelini zinatoka nje ya nchi, sio kwamba hapa tz hazipo hapana! ni kwasababu wabongo wengi ni 'wababaishaji' yan kama amepewa tenda ya mayai 1000 kila wiki, basi atapeleka kwa wiki mbili then wiki ya tatu atakuwa ameishiwa au ataanza kusuasua, hii ndio shida(commitment).
Ukweli ni kwamba kuna fursa za biashara ni nyingi kwenye mahoteli makubwa z'bar wanahitaji bidhaa nyingi mfano vinywaji, matunda,nyama,mayai,
mbogamboga tena kwa bei nzuri sana ila wanahitaji watu committed mf;kuna jamaa alikuwa anawauzia nyama ya
'mbuzi katoliki' sh 17,000@kg
Pia kipindi cha Ramadhan watu wanopeleka nyama ya Kuku,mbuzi ng'ombe wanapiga sana pesa(hii sio hotelini hata mtaani tu).
Tatizo watz tumelala
mpaka toothpick zinaingizwa kutoka nje, hii ni aibu!!
Magogo yanazalishwa Iringa mpaka yanasafirishwa nje tunashindwaje kutafuta/kuagiza mashine ya kutengeneza toothpick? tuamke tuchangamkie fursa wakuu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Ni kweli lakini tatizo ni connection...

Mkuu sio kweli kwamba tatizo ni connection,

Tatizo ni sisi watanzania kuwa serious na kazi,

Labda nikuulize swali dogo tu umewahi kufanya survey zanzibar au kutafuta masoko ukakosa? Na kama ulikosa ulichukia hatua gani kupata hayo masoko?

Tuwenk serious na biashara wakuu na naamini pia zanzibar kuna opportunity kubwa sana nataka niweke kama week nzima nikapige misele hasa ya matunda
 
Hiv kwann watu hawachangii mada nzur ka hii
Hawataki fursa,

Wanataka kumjadili wema katengeneza sha au laa,

Wana-interviews zao kule na muosha rungu,

Mapenzi ndio mijadal yai( sio mbaya mapenzi yana run dunia),

Wameajiriwa yes hawataki kabisa kwenda nje ya box(in kingwangala articles),

Wanajadili makinikia kwanza mkuu jana si umesikia tumelipwa Au hujui

Mijadala ya kuhegedana ndo tunaipenda mkuu
 
Thread ambayo haina kichwa cha habari chenye haya maneno huwezi kupata wachangiaji

-Mbowe kufanya press
-Magufuli atumbua
-Dawa ya kuongeza nguvu za kiume kwa bei chee
-Njia ya kuacha punyeto
-Makonda
-Ccm kuhonga madiwana wa Chadema
-Natafuta jimama
etc....

Yaani shida tupu.... Zanzibar wana uhitaji mkubwa sana wa Nyanya na wale wanao lima Mpunga kipindi cha sikuku na kipindi cha kawaida kuna uhitaji wa Mchele
 
Kuna wakati nilikuwa z'bar nikaenda kwenye hoteli moja ya kitalii, nilikuta watu wakishusha mizigo kwenye gari moja kubwa hapo hotelini, moja ya mizigo hiyo ilikuwa ni mayai na vinywaji vikali (mvinyo).
Nilijaribu kumdadisi mhudumu mmoja pale akaniambia vitu vile vinatoka nje ya nchi, nikashangaa sana, yani hata mayai ya kisasa wanaagiza toka nje ya nchi?
Nilipodadisi zaidi niligundua 90% ya bidhaa zinazotumiwa pale hotelini zinatoka nje ya nchi, sio kwamba hapa tz hazipo hapana! ni kwasababu wabongo wengi ni 'wababaishaji' yan kama amepewa tenda ya mayai 1000 kila wiki, basi atapeleka kwa wiki mbili then wiki ya tatu atakuwa ameishiwa au ataanza kusuasua, hii ndio shida(commitment).
Ukweli ni kwamba kuna fursa za biashara ni nyingi kwenye mahoteli makubwa z'bar wanahitaji bidhaa nyingi mfano vinywaji, matunda,nyama,mayai,
mbogamboga tena kwa bei nzuri sana ila wanahitaji watu committed mf;kuna jamaa alikuwa anawauzia nyama ya
'mbuzi katoliki' sh 17,000@kg
Pia kipindi cha Ramadhan watu wanopeleka nyama ya Kuku,mbuzi ng'ombe wanapiga sana pesa(hii sio hotelini hata mtaani tu).
Tatizo watz tumelala
mpaka toothpick zinaingizwa kutoka nje, hii ni aibu!!
Magogo yanazalishwa Iringa mpaka yanasafirishwa nje tunashindwaje kutafuta/kuagiza mashine ya kutengeneza toothpick? tuamke tuchangamkie fursa wakuu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Mkuu wewe umefanya nini?
 
Thread ambayo haina kichwa cha habari chenye haya maneno huwezi kupata wachangiaji

-Mbowe kufanya press
-Magufuli atumbua
-Dawa ya kuongeza nguvu za kiume kwa bei chee
-Njia ya kuacha punyeto
-Makonda
-Ccm kuhonga madiwana wa Chadema
-Natafuta jimama
etc....

Yaani shida tupu.... Zanzibar wana uhitaji mkubwa sana wa Nyanya na wale wanao lima Mpunga kipindi cha sikuku na kipindi cha kawaida kuna uhitaji wa Mchele

Hivi bei ya mchele kwa Zenji ni kiasi gani kwa kilo...?

Makadirio.
 
Thread ambayo haina kichwa cha habari chenye haya maneno huwezi kupata wachangiaji

-Mbowe kufanya press
-Magufuli atumbua
-Dawa ya kuongeza nguvu za kiume kwa bei chee
-Njia ya kuacha punyeto
-Makonda
-Ccm kuhonga madiwana wa Chadema
-Natafuta jimama
etc....

Yaani shida tupu.... Zanzibar wana uhitaji mkubwa sana wa Nyanya na wale wanao lima Mpunga kipindi cha sikuku na kipindi cha kawaida kuna uhitaji wa Mchele
Inaonyesha unaijua vizuri zenji wewe nataka niwe naleta matikti yangu huko mzee yapi yanasogea?
 
Si kwamba Watanzania hawaoni fursa,tatizo mahotel mengi ni matapeli, unapeleka mzigo mara ya kwanza watakulipa on time,wakikuzoea tuu,utapigwa dana dana hadi ujute!! Mtu anauza mayai afu unamlipa baada ya miezi 3,unatarajia atapata wapi pesa za kuendesha biashara? Hapo ndio wengi hukata tamaa.Huwezi supply vegetables au samaki afu ulipwe after 3 -6 month,na saingine wanajifanya invoice zimepotea. Ni kukaza roho tu.
 
Hapo wewe ulienda ukahadithiwa tu ila uhalisia ni balaaa,utajuta kuzika mtaji wako mahotel,sababu hotel nyingi zinanunua on credit basis, Hotel nyengine hawalipi hadi mmepelekana mahakamani.Wao wanataka uwapelekee chakula,walishe wageni wao ila likija swala la malipo inakua mshike mshike
 
Hawataki fursa,

Wanataka kumjadili wema katengeneza sha au laa,

Wana-interviews zao kule na muosha rungu,

Mapenzi ndio mijadal yai( sio mbaya mapenzi yana run dunia),

Wameajiriwa yes hawataki kabisa kwenda nje ya box(in kingwangala articles),

Wanajadili makinikia kwanza mkuu jana si umesikia tumelipwa Au hujui

Mijadala ya kuhegedana ndo tunaipenda mkuu
Huu ndio ukweli uliowazi kabisaaa bila kumung'unya maneno.
 
Back
Top Bottom