Fursa ya ujinga na matrix katika mfumo wa maisha ya kisasa

Fursa ya ujinga na matrix katika mfumo wa maisha ya kisasa

Mimi nakunywa bia au wine na nina lewa niombe msamaha mkuu๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…
Niwie radhi mkuu, sijamaanisha hivyo, ila kunywa kistaarabu kwani pombe hazina mwenyewe.
 
Habarini waungwana,

Ni ukweli usio na shaka kwamba asilimia kubwa ya watu duniani wana ujinga, ndiyo, ni wajinga.

Ndoto zangu siku nitengeneze pesa kwa kutumia huu ujinga, au nitumie matrix kama fursa.

Wengi mnafahamu matrix ni nini, kwa ufupi ni mfumo ambao binadamu wanauishi katika maisha yao ya kila siku, yani gereza huru.

Addictions, uvivu, kupenda mteremko ni sifa kuu ya walimwengu wa sasa, pamoja na kupenda kutumia pesa kwenye mambo ya kufurahisha macho na masikio.

Sasa ndoto yangu ni kwamba, ipo siku nitatumia fursa hii kutengeneza pesa nyingi, na naamini nitafanikiwa kikubwa Mungu anipe Uzima.

Naona wengi wanatengeneza pesa kwa kutumia ujinga wa watu, na mimi sitakubali fursa hii iniptie, pia kila siku wajinga wanaongezeka na hawatoisha kamwe.

Hili ni wazo tu nililo nalo, bado natafakari ni idara gani au njia gani nipite ili kuwanasa wajinga, na hii ndio ndoto yangu, hatakama sio leo wala kesho, lakini ipo siku itatimia.

NOTE: sitofanya utapeli, sitaonea au kudhulumu mtu, sitaiba au kurubuni watu, bali nitabuni njia ambayo najua wajinga wengi watanipa hela, hata kama ni kidogo kidogo lakini zitajaa.

Ujinga ni mtaji, ujinga ni pesa.
Ujinga mmoja wapo ni kuzalisha takataka alafu unamlipa mtu kwenda kutupa dampo,
 
Back
Top Bottom