Bob Manson
JF-Expert Member
- May 16, 2021
- 4,543
- 8,754
Habarini waungwana,
Ni ukweli usio na shaka kwamba asilimia kubwa ya watu duniani wana ujinga, ndiyo, ni wajinga.
Ndoto zangu siku nitengeneze pesa kwa kutumia huu ujinga, au nitumie matrix kama fursa.
Wengi mnafahamu matrix ni nini, kwa ufupi ni mfumo ambao binadamu wanauishi katika maisha yao ya kila siku, yani gereza huru.
Addictions, uvivu, kupenda mteremko ni sifa kuu ya walimwengu wa sasa, pamoja na kupenda kutumia pesa kwenye mambo ya kufurahisha macho na masikio.
Sasa ndoto yangu ni kwamba, ipo siku nitatumia fursa hii kutengeneza pesa nyingi, na naamini nitafanikiwa kikubwa Mungu anipe Uzima.
Naona wengi wanatengeneza pesa kwa kutumia ujinga wa watu, na mimi sitakubali fursa hii iniptie, pia kila siku wajinga wanaongezeka na hawatoisha kamwe.
Hili ni wazo tu nililo nalo, bado natafakari ni idara gani au njia gani nipite ili kuwanasa wajinga, na hii ndio ndoto yangu, hatakama sio leo wala kesho, lakini ipo siku itatimia.
NOTE: sitofanya utapeli, sitaonea au kudhulumu mtu, sitaiba au kurubuni watu, bali nitabuni njia ambayo najua wajinga wengi watanipa hela, hata kama ni kidogo kidogo lakini zitajaa.
Ujinga ni mtaji, ujinga ni pesa.