Fursa ya Biashara

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,522
5,571
Habari;

Leo nimeona niwashirikishe watu fursa,Wakati nikielezea hii FURSA niweke angalizo kwamba "UKIITIWA FURSA UJUE WEWE NI FURSA" so kama hutaki kuwa fursa basi wewe hii fursa haitakufaa.Baada ya kutoa anagalizo basi niende moja kwa moja kwenye mada ya msingi.

Kama sehemu ya majukumu yangu huwa ninashiriki katika uandaaji wa Business plan na proposals kwa ajili ya matumizi mbalimbali na wateja mbalimbali.Moja kati ya kitu nimejifunza katika kazi hii ni kwamba wengi hutumia BUSINESS PLAN kwa ajili ya kutafuta hamasa na sio kama muongozo wa utekelezaji.Hii hupelekea watu wengi kutaka njia ya mkato yaani uwape ready made business plan ambazo wanaweza kuzisoma na kusimulia wengine.Hata wale ambao ninawapatia customized business plan mara nyingi hawazitumii kuwaongoza isipokuwa tu katika yale maeneo ambayo ni mepesi.

Baada ya kupata ruhusa kutoka kwa wamiliki wa Business plans ambazo nimeandaa kwa ajili ya wateja mbalimbali ya kuwapatia watu wengine fursa pia ya kuingia katika aina ya Biashara wanazofanya nimeonelea nilete kwenu mwaliko wa kupata nafasi ya kutumia fursa hizi za kibiashara ambazo zimefanyiwa utafiti wa kina.Fursa hizi ziko katika maandishi hata hivyo utakapopatiwa utapitia katika mchanganuo wa customization ili uweze kupewa inayoendana na mazingira na mahitaji yako.Hii pia itaepusha wale ambao hupenda tu kuchukua document na kuwa na mafaili wasinitafute.Vile vile Kupata Business plan yenyewe kutakuwa na gharama,kupewa mwongozo na support ya implementation nayo kutakuwa na gharama hivyo ni muhimu sana unitafute iwapo una nia na uwezo wa kutekeleza mradi husika.Miradi itakuwa katika maeneo matatu ambayo ni elimu,kilimo na TEHAMA.Hapa chini ni maelezo mafupi kuhusu mradi husika;

MRADI WA KILIMO

Huu ni mradi utahusisha kilimo cha alizeti kwa kilimo cha umwagiliaji pamoja na usindikaji wa mafuta ya alizeti.Kilimo hiki kinalenga kulima alizeti hekari zaidi ya 5000 kwa kilimo cha umwagiliaji.Eneo limetambuliwa,Mshine za kusindika zimeshatambuliwa pamoja gharama zake,Gharama za ufungashaji na mfumo wa masoko tayari umetafitiwa.Mchanganuo uko kwa lugha ya kiingereza.

MRADI WA ELIMU

Mradi huu unalenga kutoa huduma saidizi za usimamizi na uendeshaji wa shule binafsi.lengo ni kuongeza tija,kupunguza gharama za uendeshaji,kuongeza ubora wa elimu.Utahusisha kuzipatia shule huduma kamili za usimamizi na uendeshaji kwa viwango vya kimataifa.Mradi tayari umetafitiwa na umeshaanza kukelezwa kwa hatua za mwanzoni.

MRADI WA TEHAMA
Mradi huu una aina mbili ya miradi mmoja unahusika na kutoa huduma ya Cloud Computing kwa Biashara ndogo za Tanzania na Mradi wa pili unahusisha utenegenezaji na usambazaji wa mifumo ya ICT. mabyo mingine itakuwa Cloud hosted ni mingine ni self hosted.

Jinsi ya kupata mifumo hii.tuma email kwenda masokotz@yahoo.com ukieleza kwa ufupi unataka kuwekeza katika eneo gani,kiwango chako cha uwekezaji,na eneo ambalo unafikiria kutekeleza mradi huu au mahali ulipo.Utapa mwongozo wa hatu inayofuata baada ya siku 7.Zingatia Vigezo na masharti.

Miradi yote ni bankable(Zipo benki zilizopo tayari kufinance miradi hiyo kwa kuzingatia vigezo na masharti ya mikopo ikiwamo dhamana n.k.) hata hivyo ni lazima uoneshe kuwa una uwezo wa kutekeleza miradi hio.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom