FURSA - Mtu wa kuistall software anahitajika

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,129
7,896
Nimejaribu kwa muda mrefu kuistall software ya Autodesk Maya na Autodesk MotionBuilder kwenye Bootcamp (Windows pertition ya Mac), ila nimehangaika sana bila mafanikio.

Ninazo installation files aina kama mbili tofauti ila zote zinaleta error message wakati wa kuistall. Sidhani kama tatizo ni file zenyewe za kuinstall.

Kama kuna mtu mwenye utaalamu huu anipe tafu. Nahitaji msaada huu haraka iwezekanavyo.
 
Kama uko Dar,Mwanza au Mara tuwasiliane nikuunganishe na wataalam mkuu.
Pole sana lakini...
 
Nipo Dar wakuu. Mlatinoh king, usiwe na shaka, hela ya nauli na soda ipo! Mimi mtu fair sana siwezi kumfanyisha mtu kazi nikamuacha kama alivyokuja. Kama vipi, tunaweza kukubaliana kabla mtu hajaja. Wadau, naomba tuongee PM. Yeyote aliye tayari kuja hata kesho mimi nipo tayari.
 
Nimeshapata msaada niliokuwa nauhitaji. Kuna mmoja kutoka humu amenisaidia remotely, sijamjua ni nani kwa ID ya JF. Yuko vizuri sana.
 
Nimejaribu kwa muda mrefu kuistall software ya Autodesk Maya na Autodesk MotionBuilder kwenye Bootcamp (Windows pertition ya Mac), ila nimehangaika sana bila mafanikio.

Ninazo installation files aina kama mbili tofauti ila zote zinaleta error message wakati wa kuistall. Sidhani kama tatizo ni file zenyewe za kuinstall.

Kama kuna mtu mwenye utaalamu huu anipe tafu. Nahitaji msaada huu haraka iwezekanavyo.

Tumia youtube... andika tatizo lako search watakupa tutorials za jinsi ya kuinstall
 
Nimeshapata msaada niliokuwa nauhitaji. Kuna mmoja kutoka humu amenisaidia remotely, sijamjua ni nani kwa ID ya JF. Yuko vizuri sana.
Itakuwa ni mimi mkuu:), kama ulivyoona ilikuwa inagoma kutumia normal temp folder kwenye computer yako wakati wa installation yake hivyo nikacreate another temporary folder la kulipa all permissions then nikadirect installation kwenda huko na ikakubali, baada ya installation tukarudisha settings kama zilivyokuwa.
Issue ni kwamba hizi software zinatoka versions tofauti kila siku(upgrades) na Operating Systems pia vilevile( Windows 7, 8 , 10 etc) hivyo ni rahisi kabisa kukawa na vitu vidogovidogo ambavyo haviendani. ndio maana inabidi utumie akili kidogo kuidanganya:):):)

I think mods wangehamishia huu uzi kule TECH
 
Nalirudisha ombi langu tena. Kama mnavyoona zoezi lilifanikiwa mara ya mwisho ila computer imepata matatizo fulani nalazimika kurudia huu mpango mzima. Sasa hivi siwezi hata kulog in, napata black screen tu hivyo sasa nalazimika kuistall upya Windows.

Kama kuna mtu anaweza kuifanya hii kazi naomba tuwasiliane haraka tafadhali. Unaweza ukafuata maelezo ya https://www.jamiiforums.com/members/islam005.12418/ hapo juu jinsi ya kufanya. Aliweza kuimaliza hii kazi ndani ya dakika 20. Bahati mbaya kuna hatua sikutilia maanani alikuwa anafanya nini otherwise ningeweza kuifanya hii kazi mwenyewe.
 
Back
Top Bottom